pmwasyoke
JF-Expert Member
- May 27, 2010
- 4,593
- 2,978
Bond fund - hii inafaa zaidi kwa mtu mwenye fedha nyingi atakaye kuziweka mahali kisha awe anakula faida yake kila mwezi au kila miezi mitatu. Mfano mtu anapata kiinua mgongo cha milioni 100 na hana mpango wa kuziingiza kwenye biashara yoyote. Akiziweka bond fund na kuchagua mpango wa malipo kila mwezi anakuwa sawa na mtu mwenye mshahara.Asante mkuu, nazidi kujifunza, nielezee kdg kuhusu bond fund mkuu.
Wanaiita bond fund kwa sababu wao wanawekeza sehemu kubwa ya fedha za mfuko huu katika bond za serikali, hasa za muda mrefu ambako wanapata riba za over 15%. Na ndio maana wanaweza kutoa faida za around 11 - 12% per annum kwa wanachama wao.