Je, ni mambo yote unaweza kumwambia rafiki yako?

Turnoff

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
632
1,000
Vitu vingine unajinyamazia tuu,mpaka wamefikia kuoana yamkini waridhiana na wsko tayari kuvumiliana kwenye shida na raha,maudhi na karaha!
 

Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
63,869
2,000
Unakutana na rafiki yako mnakwenda kwenye kitchen party. Kwakuwa wewe ndiye best man. Unamuona bibi harusi kwa mara ya kwanza lakini sura yake si ngeni. Unakumbuka mlikutana kwenye hoteli uliyofikia. Kumbe bibie alikwenda kuagana na mpenzi wake wa zamani. Uliwaons kwenye corridor wakiwa kwenye mahaba mazito.

Ukiwa kama mwanaume utachukua uamuzi gani hapa?
Wanaume wanampenda kitchen Party ni hatari sana.
Hata usipokuwa mwanaume, mambo ya umbea ya nini?
Tujifunze kuwa Na upendo Na hekima. Hekima itakuongoza kwenye nini cha kuongea Na upendo utakuongoza kwenye kusamehe.
Huwezi kujua, huenda hata huyo Bwana harusi amelala kwa mpenzi wa zamani wakiagana.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
54,814
2,000
Kuna rafiki yangu alijua HIV status ya bibi harusi one day before marriage! Unajua kilichoendelea
Alisema? Lakini bibie alikua mchawi, mtu unaeenda kushirikiana nae kwa shida na raha humfichi status
 

narumuk

JF-Expert Member
Feb 10, 2018
1,943
2,000
Alisema? Lakini bibie alikua mchawi, mtu unaeenda kushirikiana nae kwa shida na raha humfichi status
Hapana ni kuwa hata bibi harusi hakujua. Ila waliamua kuendelea na harusi kwa vile hata send-off ilishafanyika alhamisi na ilikuwa ijumaa majibu yalipotolewa. Maisha !!!
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
54,814
2,000
Hapana ni kuwa hata bibi harusi hakujua. Ila waliamua kuendelea na harusi kwa vile hata send-off ilishafanyika alhamisi na ilikuwa ijumaa majibu yalipotolewa. Maisha !!!
Na kuambikizana si ajabu walishaambukizana
 

Prince Kunta

JF-Expert Member
Mar 27, 2014
19,403
2,000
Unafiki mbaya

Kama ni rafiki yangu sana namwambia vizuri sana tu ila kwa evidence

Ili kuepusha usumbufu na fedhea baadae kuombwa ushauri wa mahusiano na rafiki

Ndoa iheshimiwe
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
50,661
2,000
Nimesoma comments zote.

Wanawake wanatetea huo uzinzi alioufanya huyo mwanamke mwenzao.

Ila wanaume wanajua maana halisi ya urafiki, hawawezi kukubali kuona rafiki yake aangamie wakiona.

Binafsi nitamwambia jamaa picha nzima. Ila baada ya kitchen party.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom