Je ni mambo gani yanawatofautisha Watanzania na waafrica wengine toka nchi zinazoishinda Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni mambo gani yanawatofautisha Watanzania na waafrica wengine toka nchi zinazoishinda Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Dec 15, 2011.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Watanzania tumerithishwa na tunajua ili tuendelee tunahitaji mambo makuu 3 ambayo ni:- watu, siasa safi na uongozi bora.Mara nyingi tumekuwa tunajadili kuhusu mapungufu ya kisiasa na kiuongozi kama matatizo yetu makuu lakini tumekuwa tunaacha kujadili juu ya 'watu'........yaani watanzania.Tumekuwa mara nyingi tunasema.....watu tz si shida kwani wapo.....tumeacha kabisa kuwajadili..je watanzania ni watu wa namna gani??...maana kuwa na watu haitoshi....

  Leo naomba nianzishe mjadala juu ya watu wa Tanzania....maana baada ya hii miaka 50 tunabidi kukaa na kutafakari kwa kina juu ya matatizo yanayotufanya tuwe hapa tulipo......yaani hatusongi mbele huku tukiona wenzetu tuliokuwa nao sawa kipindi cha uhuru wakiwa mbali kimaendeleo........na wengine tunawazidi kwa raslimali....na wako humu humu africa.....e.g Cape verde,Mauritious,Botswana,..hata Kenya....na Rwanda ...n.k....

  Kwa kuanza....nitoe maoni yangu juu ya wa tz...alafu mtaendeleza kila mtu kwa maoni yake.......je watanzania ni watu wa aina gani???

  A]Hawana uzalendo na ni wabinafsi:-..........hili suala kwa kweli limewaathiri wa tz kwa kiwango kikubwa na linachangia kwa kiasi kikubwa umaskini wa nchi hii.Ni jambo la kawaida kuona mtanzania (haswa viongozi)anamiliki gari ya mil.200 huku barabara nchini......na kwenye majumba yao hazipitiki, mashule hayana vitabu, hospitali hazina vifaa....n.k...Ni jambo la kawaida kuona watanzania na viongozi wao wakijenga mahekalu mijini (haswa dar) na kukimbia vijijini wanakotoka ambako kumejaa umaskini.Ni jambo la kawaida kuona watanzania wakichangishana mapesa tele kwa ajili ya sherehe na tafrija za masaa kadhaa huku hao hao wakishindwa kupeleka watoto wao shule za maana.......Ni kawaida pia kuona watanzania waliopewa dhamana ya uongozi wakiwaibia watanzania wenzao jumla.......yaani mtu anaona bora kiwanda kife ,au barabara isijengwe ili yeye apate.....kuna mifano mingi.........tuendelee kuchangia..........

  B]Wanafiki:-.......hili suala kwa kweli ni unique kuhusu wa tz...wa tz wanasumbuliwa na unafiki kwa kiwango kikubwa na hili limechangia kutufikisha hapa tulipo.......mnafiki ni yule anaetenda tofauti na anavyosema.....hii imechangia sana umaskini wa tz....haswa kwa viongozi wetu.Viongozi wanakwenda vijijini kuwaomba maskini kura alafu wanawakimbia........wanaishi na kuwekeza mijini....tafiti zimeonyesha kuwa asilimia 80% ya wa tz hawaaminiani....watanzania wanaishi kinafikinafiki tu.....watu wanachekeana kama ndugu lakini hao hao wanamalizana..........hili lipo kwa jamii nzima ya mtanzania.....na limejiingiza kwenye uongozi na kutuletea balaa kubwa kwani ni kawaida kwa viongoi wetu kupiga kelele za kinafiki kuwa wanawajali raia wao lakini wayatendayo ni tofauti na wayasemayo.......mifano ni mingi........hata juzi tumeona wanataka kupandishiana posho huku wakijua watanzani wameelemewa na umaskini.......tuendelee kuchangia......

  C]Ombaomba:-.......hili tatizo ni sugu kwa mtanzania na limechangia sana kutufikisha hapa tulipo kwani kwa kuwa jamii na viongozi wake imezoea kuombaomba basi watu hawajitumi kabisa kwani wanajua wakishindwa wataomba........hata tumemsikia rais akikimbia huku na kule kuomba.......nchi inaomba, viongozi wanaomba na hata raia wanaomba.....yaani huu ugonjwa wa kuomba ni sugu tz.....hata bajeti ya nchi inategemea kuomba......raia nao wanaomba.....utamsikia Juma akikwama maisha anamwomba Ali amsaidie(mfano)............utasikia hata bungeni wabunge wakichangia mijadala...wanasema tunaiomba serikali itusaidie hiki na kile....yaani wanaiomba serikali iwasaidie kutekeleza majukumu yake!!! nchi hii watu hata haki zao wanaziomba.........wamesahau kuwa haki haiombwi bali hudaiwa......kwa kweli watanzania!!mh.......utamsikia mtanzania anaenda dukani na pesa yake akifika anasema anaomba kitu fulani (wakati hela anatoa yeye!!).....kila mahali ni kuombaomba tu......watu wanaomba huduma ambazo wanazilipia.....kila mahali tz hii kitu ipo....yaani imeshakuwa ni culture ya tz.......utamwona mtu anamkopesha mtu pesa...alafu anamfuata ili alipe anamwambia......aisee...naomba unilipe ile hela yangu....mh!!!!......kuna mifano mingi......tuchangie....

  D]Ushirikina:-.....Sikatai kuwa ushirikina haupo sehemu nyingine kwa wenzetu ila niseme tu ushirikina unaitafuna sana tz....tumeona ambavyo imani za kishirikina zimehusishwa na harakati za watu kupata uongozi nchi hii....hata bungeni kuna wakati haya mambo yalitokea kuhusisha wabunge......nafasi za uongozi zinapohusishwa na ushirikina sidhani kama hii dhambi inasameheka......Tanzania ni nchi pekee africa iliyopata kuhusishwa na imani za kishirikina wakati yalipotokea mauaji ya albino......tena imani zenyewe zimekuwa zikihusishwa na kusaka utajiri.....watu wanapoteza muda mwingi kwenye ushirikina ili kupata mali au uongozi na kuacha kufanya shughuli za msingi za kujitaftia maendeleo.........ni jambo la kawaida sana tz kusikia mtu akifanyiwa maombi eti kuondoa mapepo........yaani umezuka utitiri wa wasanii wa maombi eti wanajiita manabii!!!wanafanya maombi kuondoa mapepo....watu wanaacha kufanya kazi wanashinda makanisani kutafta faraja.......kisa mapepo.......ushirikina umejaa kwenye jamii ya mtanzania......mifano iko mingi...tuchangie..........

  E]Uswahili(uvivu).........yaani mtanzania anajulikana kwa uswahili na maneno meeengi......watu kazi hawafanyi ...wamezoea short cuts....kazi ni kupiga maneno tu....kwa bla bla tz ndio umefika....kila mahali ni usanii tu.......tuchangie mifano.........

  F]...............................endeleza..

  G].................................


   
Loading...