Je, ni Mambo gani yalikuwa ya kawaida sana miaka ya 1980s - 1990s ambayo Vijana wa sasa hawawezi kuyajua?

Na usisahau kipindi hicho kuangalia ni saa ngapi ilikuwa shughuli pevu. Nazungumzia kabla ya kuja zile saa zisizo na mishale (electronic). Watu wenye saa za uhakika walikuwa ni wachache tena wengi zilikuwa zinapoteza majira kishenzi. Vijijini watu walikuwa wanaamka kwa kutumia majogoo na mchana sehemu zenye makanisa walikuwa wanajua saa kwa kutumia kengele za kanisani.
Hah!!! Hatari sana
 
Tufafanulie sisi vijana wa sasa
  1. Reverse call - Ilikuwa ni huduma ya Posta na Simu ambapo unaomba upige simu na gharama za upigaji wa simu zinalipwa na mopeaji wa simu husika
  2. TMO - Telegraphic Money Order - Hii ilikuwa ni njia ya kutuma pesa kupitia shirika la Posta na Simu, TMO ikija nakwenda kupanga foleni Posta na Simu ili ulipwe pesa yako, iwapo fedha haipo mnabanikwa juani kusubiri mtu akija ku deposit ndipo mlipwe, akikosekana inabidi urudi tena kesho kama vile umekwenda kuomba kazi kumbe unafuata haki yako.
  3. Pass book - Kitabi cha bank ambacho ni utambulisho wako kwa bank husika kuwa una amana yako katika bank hiyo, kwasasa tunatumia card za bank
 
Ilikua ni kawaida sana kufua nguo za shule usiku hasa kama kesho ni ukaguzi wa usafi hapa kwenye 90's
 
Mama aliniomba niandike barua tumtumie bro aliye kua mjini, sasa nimemaliza nimeweka na sahihi mama akadai amesahau kuwapa salamu Ndugu zake wengine akinisihi niendelee kuandika kwa chini, nilimwelewesha wapi hakubali , anadai hawatajisikia vizur, nilipata shida sana.
 
Nakumbuka enzi hizo ilikuwa kawaida kabisa kusibiria kipindi cha muziki mida ya usiku huku ukiwa na kaseti yako, unasuburia wimbo unaoupenda ukifika unaurekodi, Tulikuwa tunasubiria usiku kwa sababu mchana Dj alikiwa anaongea akijisikia wakati mziki unacheza na wimbo anaweza kuukata mapema,

Enzi hizo hakukuwa na chanzo cha taarifa cha haraka kukujibia maswali, mfano unaweza kunywa coca cola ila ukitaka kujua nani alie itengeneza ilikuwa ni shughuli pevu kweli kweli, siku hizi ni mwendo wa google, wikipedia, n.k

Kuwasiliana kwa njia ya barua na watu wa mbali, Nakumbuka barua zikifika kama ni ya mpenzi wako ilikuwa unaoga kabisa na kula kabisa kabla hujaisoma, sikwambie mtu, watu walijua kuongea kupitia maandishi.

Kulikuwa na vijiwe vya kupeana habari na kukutana na washkaji, ukibaki nyumbani utaboreka sana kwanza inakubidi tu utoke nje maana wenzako wote wapo nje, hakukuwa na kubaki ndani unachati, upo instagram, netflix, n.k
 
Back
Top Bottom