Je, ni makosa mimi kuwa mteja wa Tigo?

Desidery

JF-Expert Member
Dec 5, 2012
233
77
Ninatambua kwamba tigo ni kampuni inayojiendesha kibiashara kwa lengo la kupata faida kihalali.
Ninatambua kwamba mimi ni mtanzania ninauhuru wa kuchagua niwe mteja wa kampuni gani ya mawasiliano miongoni mwa makampuni yaliyopo Tanzania....

MWANZO
nimekuwa mteja wa kampuni hii muda mrefu sana namba yangu enzi ile tunatumia malipo ya dola pale majani ya chai.. yaani kabla ya kuanza kutumia vocha.
Nimekuwa mteja mzuri na sijawahi kuwa na tatizo lolote toka kwangu kuelekea wao yaani Tigo.
Nimehama na majina ya kampuni kila walipobadili majina yao kwa mfumo wao wa kubadili majina kila baada ya miaka mi4. sijui kwanini hufanya hivyo sitaki kuingia huko watajua wao.

PILI
Nikaendelea kuitumia kampuni hii kuwa ndio Telephone provider wangu kwa muda mrefu. nikitumia huduma za Blackberry, Tigo bima na nyinginezo
Huduma za Blackberry za malipo ya mwezi mmoja. nikitumia tawi la Tigo la pale Ocean Road....

HATIMAE
Tigo wakanza tabia ya kuwa down nertwork. lakini muda wa siku ya mwisho ukifika wanakata huduma yao on time, ukiwauliza wanasema ni automatic service inayofanya hayo, bila kujali muda wangu ambao network ilikuwa down.. ukiwauliza kuhusu time compensation esksti network ilipokuwa down utaanza kupigwa danadana mpaka utajuta..
binafsi niliamua kuachana kabisa na huduma hiyo.

Kihisu huduma ya Tigo Bima ndio sitaki hata kuielezea maana hakuna asiejua namna watanzania walivyopigwa kwenye huduma hii.

SASA
Pamoja na mambo hayo yote sasa hivi Tigo wameanza kutounganisha huduma za Kabang na mini kabang pale unapoomba. na ukiwapigia hawapokei simu kwa muda mrefu wakijua kwamba wewe ni mteja unapiga simu kwao ukiwa na matatizo. sasa je ikiwa tatizo nilia haraka utapataje msaada?
na ikiwa wanapokea simu nyingi kutoka kwa wateja means wanapata malalamiko mengi// kama wateja wanalalamika sana inamaanisha huduma yako mbovu.

jana mimi nimeomba kuunganishiwa mini KABANG, nikalipa malipo yangu kupitia tigo pesa, nikapata sms kunialifu pesa imekatwa kutoka kwenye akaunt yangulakini sikupata msg ya kutaaalifiwa kuwa nimeunganishwa... nikawa nawapigia simu ili kuomba waniunganishe kwani nilikuwa natakiwa kuwapigia simu ndg zangu kuwafahamisha juu ya ugonjwa wa mjomba wangu.... sikuunganishwa, na simu haikupolewa.
leo jioni yule mgonjwa amefariki, ninapewa lawama sana kwakutotoa taarifa.. nimepiga simu tigo imewachukua dakika 18 kupokea simu yangu. na ilipopokelewa nimeongea na mtu wao akakata simu bila msaada wiowoye...
nikapiga tena ikwawachukua dakika 17 kupokea nikaongea nao wakaniambia jana kulikuwa na matatizo ya kuunganisha huduma za kabang.. nilipouliza sasa inakuwaje? wakakata simu..

sikuchoka nikapiga tena ikachukua dakika 22 kupokea simu. nikalalamika juu ya tatizo la kutounganishiwa muamala niloununua, wakajibu kwamba muamala huo uliunganishwa tangu jana saa 12 jioni wakati jana mimi nilijaribu mara kadhaa kupiga simu ilikataa kwa kudai haikuwa na salio,

NINI HATMA?
naomba kuweka wazi kabisa kuwa Tigo wanaelekea kukosa uaminifu kwa vihela vidogo ambavyo wanatoza kwa huduma kisha hawatoi huduma sahihi...
ni siku chache magazeti hapa Tanzania yaliiandika kuwa Tigo ni wezi ktk huduma ya Tigo Bima.. sasa wamebadili gea wameanza kuiba kwenye huduma za kabang.

Kaeni chonjo na utapeli huu mpya wa Tigo.
 
Haya ndio majipu yanayo stahili kutumbuliwa bila kupoteza muda, mteja anaibiwa, huduma mbovu na hapati haki yake. Serikali pia inahusika hapa kwa kuwaachia hawa kuwa majambazi kiasi hiki. Ni lazima serikali iweke idara ya kuangalia utoaji huduma na malalamiko ya wananchi
 
Ndo maana nikija likizo nyumbani Tanzania ninakuwa sina mawasiliano ya simu manake jinsi kampuni za simu za mkononi wanavyotoa huduma zake hazieleweki kabisa ni tofauti kabisa na mabara (makontineti) mengine, ukinunua ''kifurushi'' mara kimekwisha, network is down n.k
 
hebu ngoja.tigo kampuni la simu au tigo huduma wanazotowa kinadida mtamu?maana maelezo kama risala
 
Ndo maana nikija likizo nyumbani Tanzania ninakuwa sina mawasiliano ya simu manake jinsi kampuni za simu za mkononi wanavyotoa huduma zake hazieleweki kabisa ni tofauti kabisa na mabara (makontineti) mengine, ukinunua ''kifurushi'' mara kimekwisha, network is down n.k
Kijana wa Bukoba.
 
Desdery
1.Mkuu kwanza kubali kabisa wewe ni Jipu
2.Pole kwa kufiwa na Mjomba, Mungu amweke mahala pema peponi

Sasa Mkuu wewe ulishindwa kuwasiliana na ndugu zako juu ya taarifa adhimu za ugonjwa kisa minkabang?

Nadhani haukuwa serious
 
Hawa jamaa hawafai kabisa .makampuni ya simu hapa tanzania yanakenuliwa meno na kuchekewa chekewa na gawa mawaziri wa hi wizara tuaibiwacsana hasa kweywe hii huduma ya bima na huwa hawaweki namba za kuhiondoa .siku moja niliwauliza kwanini internet zao ziko dawn .wakajibu eti wamezidiwa ..sasa kama umezidiwa maanayake unafanya biasgara nzuri kwa hivo unatakiwa kuboresha miundo mbinu yako ila haya makampuni yanapata faida kubwa sana
 
Desdery
1.Mkuu kwanza kubali kabisa wewe ni Jipu
2.Pole kwa kufiwa na Mjomba, Mungu amweke mahala pema peponi

Sasa Mkuu wewe ulishindwa kuwasiliana na ndugu zako juu ya taarifa adhimu za ugonjwa kisa minkabang?

Nadhani haukuwa serious
imagine upo na mgonjwa hospitali, imambo kibao yanatakiwa,,, una simu 2 mkononi unaambua kujiunga kwa simu moja ili uwasiliane na ndg kisha kampuni ya simu inakutapeli ukiwa kwenye kona mbaya kama hiyo. ambapo kila sh, inakuwa na kazi yake, so unaamua kuweka vocha kwenye ,tandao mwingine unaanza kuwasiliana na watu.
hlf mwishowe wanakujibu just simple TULIKUUNGANISHA NA SASA MUDA WAKO UME EXPIRE!!!!!!

TIGO ni jipu linatakiwa kupasuliwa, na tusubiri sijui mwaka huu watabadili jina au itakuwaje?
 
Hawa jamaa hawafai kabisa .makampuni ya simu hapa tanzania yanakenuliwa meno na kuchekewa chekewa na gawa mawaziri wa hi wizara tuaibiwacsana hasa kweywe hii huduma ya bima na huwa hawaweki namba za kuhiondoa .siku moja niliwauliza kwanini internet zao ziko dawn .wakajibu eti wamezidiwa ..sasa kama umezidiwa maanayake unafanya biasgara nzuri kwa hivo unatakiwa kuboresha miundo mbinu yako ila haya makampuni yanapata faida kubwa sana
tatizo hawa jamaa wanadhani kila mteja wao ni mjinga fln, wana boa sana.... ngoja mii nawaangalia wakirudia NITAHAKIKISHA WANASIMAMA MAHAKAMANI wezi sana.. na sms zao sizifuti nitaziweka, wataingia tu kwenye 18,,,,

kuna kitu najifunza hapa toka mitandao ya nje kisha niaangalia TCRA wanasemaje.
wasidhani sheria ya mitandao ni kwetu sisi yu bali hata upande wao,
 
Back
Top Bottom