Je, ni madhara gani yatatokea endapo parking fees itaunganishwa kwenye mafuta?

Exorcist

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
1,236
1,257
Kwanza mafuta yenyewe tayari yameshakuwa too expensive, sioni shida huu usumbufu wa parking nao tukaepukana nao, tulipe hiyo parking fees huko huko kwenye mafuta tujue moja.

Hizo pesa za kuwalipa watu kuzunguka na vimashine nchi nzima kwenye jua kali ni bora wakafanya Sensa tu. Wenye magari wanasumbuliwa sana na watu wengi sana, wapunguziwe usumbufu angalau.

Kwa wale mnaosema hamuendi mjini inabidi mfahamu, hata ukipaki nje ya fensi yako kwenye road reserve huko porini, bado ulitakiwa ulipe parking fees, na sidhani kama unaweza kutumia mafuta halafu usihitaji parking. Tujadili tuone.

FRANCIS DA DON
 
Mkuu, mbona unatoa ushauri unaozidi kutuongezea mzigo? Wewe huu uliobeba sio mzito kwako?

Kuna mtu ana gari, anaenda town(kwenye parking fee areas) once per month au asiende kabisa...
 
Kuongeza kijiko kimoja kwenye pipa sidhani kama ni ishu kubwa sana, wala hutai-feel, mi nachukia haya mambo ya kuja kushtukizw aunaambiwa una deni kuuubwa , eti sijui ulipaki wapi sijui..., ni usumbufu kuanza kukimbizana na network kwenye vimashine vyao eti kujua deni, bado uuhangikie control number, halafu ndio ulipe, hivi ina maana sisi hatuna kazi za kufanya sio? Wanatumia bunduki kuwinda samaki. Napendekeza waiunganishe tu humo humo.., hata kama huendi mjini, ulinunua mafuta ya nini kama hutoki na gari, na hata kama ni porini umepaki kwenye road reserve, bado unatakiwa uilipie...
 
Kwani kila mtu anapaki kwenye public areas?
Na tutajuaje kama haupaki kwenye road reserve kwenye mitaa isiyo na wahudumu wa parking? Ishu ni kuondoa usumbufu wa kulipa lipa micontrol number kila kukicha, kwani hatuna kazi zingine za kufanya? Waunganishe tu humo humo
 
Utawawekea watu bili kwa kufanya guessing?
 
Ni generalisation for the better good, mbona wenye chainsaw wanalipia Roadlicense?
Tunaangalia complication iliyopo katika ulipaji wa hiyo parking, na urahisi wa kuilipia katika mafuta, kumbuka, kwa mwaka mzima kwa kupitia mafuta unaweza jikuta umelipia elfu ishirini tu, maana tunalipa wote. Tofauti na sasa ambapo tunaoenda mjini tu ndio tunabebeshwa mzigo, lakini wanaopaki kwenye road reserve pembezoni mwa jiji ambao nao walipaswa kulipia, wanapata free boat
 
Hatuwezi tukakulipia wewe sisi wa mashambani huku. Watu wanaotumia parking za serikali ni wachache kuliko wanaotumia binafsi. Pambaneni na parking zenu hukohuko.
 
Huko shambani unapaki wapi? Unapoweka mafuta kwenye gari laki unakuwa unaenda wapi? Huko unapoenda haupaki gari? Hakuna road reserves? Tulipe wote nanpia tupunguze usumbufu wa macontrol number. Control number na network zinakera sana!
 
Cha muhimu ni kuunganisha no ya gari ya muhusika,no ya simu na mifumo ya TARURA,tatizo litaisha,ukiandikiwa parking fees unapata sms alert kwenye simu yako,na pia itasaidia kutrace hata gari lililofanya uhalifu.
Naomba Serekali yetu sikivu ilichukue hili wazo.
 
Kuna Uzi ulishaanzishwa huku unafanana na huu,tafadhali mods uunganishen uzi
 
Back
Top Bottom