Je, ni lazima Wakimbiza Mwenge Tanzania wawe kutoka CCM pekee na wakimaliza baadae waje Kuteuliwa kuwa Viongozi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,874
Kuna sababu ambazo nimepewa hadi Mtu kuwa Mkimbiza Mwenge Kitaifa nchini Tanzania ( ambazo baadhi yake si za Kimaadili kabisa ) japo bado naendelea Kuzithibitisha taratibu ila kwa leo naomba tu kujua je, ni lazima ukiwa Mkimbiza Mwenge Mkuu uwe unatoka tu Chama cha Mapinduzi? Kama Jibu ni ndiyo je, Tunu ya Taifa inaweza ikawabagua Watu wa Chama fulani na kuwapendelea wa Chama fulani tu? na je, ni lazima muda wa Kukimbiza Mwenge ukimalizika huyo Mkimbiza Mwenge ateuliwe na Rais kushika Nyadhifa Serikalini?

Mkimaliza Kunipa Majibu yenu nawapeni tena Swali hili la nyongeza kwamba ni kwanini Wakimbiza Mwenge huwa wanaogopwa kuliko na kuanzia Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na hadi kwa Mawaziri? Kuna Waziri Mmoja hivi ana ' PhD ' yake nimebahatika kumuona kupitia TBC1 akiwa na Mwenge huko Jimboni Kwake na nilichobahatika Kukiona kwa haraka haraka ni jinsi yule Mkimbiza Mwenge Mkuu akiwa anamdharau huyu Waziri ( mwenye dhamana ya Wizara ambayo inapendwa mno na wana Simba na Yanga ) na Waziri kuonekana akiwa anatetemeka, anajibalaguza na anamnyenyekea mno huyo Mkimbiza Mwenge Mkuu.

Nitashukuru nikielimishwa juu ya hili na karibuni sana Wandugu.
 
Siti ya kwanza kumumunya ubuyu

Ngoja tuwasubiri sasa Wabobezi wa mambo haya waje Mkuu ili basi Mimi na Wewe tuzidi Kuelimika na pengine tuweze Kuyajua hata yale ambayo tulikuwa hatuyajui kuhusiana na huu Mwenge wetu wa Uhuru ambao naambiwa hata katika Katiba yetu pia nao umejumuishwa na sehemu ya Tunu yetu ya Taifa.
 
1.Sisiem wamejiwekea huo utaratibu,tambua mtumishi ambaye ni mwajiriwa wa serikali haruhusiwi kujihusisha na siasa lakini ukiwa ndani ya CCM ni ruksa,na mambo mengine mengi ambayo imekua utaratibu wa kawaida kwa CCM,yapo mengi yakujiuliza.
2.Wale wakimbiza mwenge wakuu hujua kabisa kua watakufa mara baada yakumaliza shughuli hiyo,na viongozi wa serikali hujua hilo,hivyo hujiona wako juu ya yeyote kasoro rais kwani hujua kila mtu anajua kua wamejitoa sadaka maisha yao.
 
Huwezi kuutenganisha mwenge na ccm, wakuu wa mikoa, wilaya, uteuzi wa hao wakimbizaji kwenye vyeo vya kisiasa, nk.
 
Kwa upande wangu sielewi kabisa mantiki ya mbio za mwenge. Sijui hili suala tumelipata wapi, na nini hasa ilikuwa ni malengo yake ya msingi, na ni nchi ngapi Afrika zinakimbiza mwenge kama sisi.

Ila kwa wale wenye kupenda kuyachunguza maandiko matakatifu, mianga ya moto kama wa mwenge huambatana na ibada za kipagani na sanamu. Na tena huwashwa nyakati za usiku, kwetu sisi hata fomular imekosewa kwa kuwashwa nyakati za mchana. Hii kitu hii kwa kweli ingepelekwa jumba la Makumbusho tu.
 
je, ni lazima ukiwa Mkimbiza Mwenge Mkuu uwe unatoka tu Chama cha Mapinduzi?


"Tungeweza kuwapa nafasi hiyo wapinzani ila kwakuwa wanatupinga ipo hatari ya wao kuuangusha mwenge wetu kwa makusudi kabisa kwakuwa hawautaki"

Alisikika akisema
 
Kuwa mkimbiza Mwenge ni lazima uwe mtu wa chama tawala (CCM), kwa kuwa mwenge kila unapopita Mikoani hutumika katika kuzindua miradi ili kutekeleza ilani ya chama. Sasa wewe ukiwa mtu wa upinzani sizani utaendana na sera za Chama kingine. Ndio sababu wanaoteuliwa kukimbiza mwenge lazima wawe wanafanana na itikadi zao.
 
Write your reply...mwenge ni uchawi na ushirikina mtupu, hakuna lingine! hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuteketeza mabilioni eti kuzindua miradi
Nchi zisizokuwa na utaratibu huo wa kukimbiza moto, miradi yao inazinduliwa na nini?
 
Mfano,Mkuu wa wilaya Mlele,Mkuu wa wilaya Tarime...................................na wengine endeleeni kuwataja
 
Hivi tujiulize, mwenge huwa unafika na kukesha sehemu kama vyuo vya elimu ya juu, makazi ya watu wenye hadhi ndani ya jamii, sehemu zenye ofisi zenye kuheshimika? Ama maeneo yake ni Yale ya Uswazi kwa saaana tu na maeneo mengine ya vijijini yenye ufukara wa kutupwa, ili makabwela wakeshe kwa kuusindikiza kwa kusukumia pombe za kienyeji na ngono zembe?
 
Mwenge ni baadhi ya maagano machafu ya kishirikina ambayo nchi hii imeingia na ni rahisi kushikiliwa na viongozi waliotakea kwenye sehemu zenye ushirikina. Siku tutapata kiongozi asiyeamini ushirikina, huo ndio utakuwa mwisho wa agano hilo chafu ndani ya nchi yetu. Ili hayo yatokee ni lazima ccm itoke madarakani au apatikane rais aliyezaliwa baada ya uhuru, ambaye hajakulia vijijini ambapo imani za kishirikina bado zina nguvu.

Wengi wa watu wanaomini mwenye ni wazee, washirikina, masikini, wana mawazo mgando au ni wafuata mkumbo. Watu wengi wenye uwezo wa kuhoji hawaamini huo ushirikina uitwao mwenge.
 
Mchakato wa kuwapata wakimbiza mwenge Ni Siri,mafunzo yao Ni Siri,ukiachilia mbali kulindwa kwa umakini mkubwa lakini pia kwa kiasi kikubwa hauwashirikishi wananchi wote,wana ccm wamejimilikisha mwenge wa uhuru,halafu anatokea mtu anasema "mwenge ni wa watanzania".Mwenge unatumika Kama kichaka Cha kueneza itikadi za chama Cha mapinduzi na ndiyo maana kila uchwao unapoteza umaarufu na uhalali,hamasa na nguvu Kama hapo awali.
 
Back
Top Bottom