Je ni kweli yanafanyika kwa wakati huo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni kweli yanafanyika kwa wakati huo?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by TaiJike, May 22, 2012.

 1. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Natanguliza samahani kama ntakuwa nimewakwaza baadhi ya wasomaji, lengo langu ni kuelimishwa.

  Kuna mama mmoja ameolewa na kukuta nyumbani hapo kwa mumewe kuna mtoto alizaliwa na mama yake kuachika. Kinachonishangaza ni mama huyu kila anapomwita binti huyu hutumia neno we mwanaharamu, laanakum, bimatrashamsi, nk. nk. ilimradi tu atumie majina yasiyofurahisha badala ya kutumia jina halisi la binti huyo. Na inapotokea amekosea huambiwa ni kwa kuwa hakupigiwa bismillah (wakati wa utungo wa mimba yake), au hakuadhiniwa kipindi anazaliwa.

  Swali: Je ni kweli haya hufanyika wakati wa vitendo hivyo? (kupiga bismillah au kuadhini).
   
 2. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Heee... mimi si muumini wa kiislam hivyo sijui kama huwa wanapiga hiyo bismilahi, lakini hata kama ndivyo ilivyo mtoto huyo hatia yake iko wapi? Ni unyanyasaji wa watoto ambao unazungumzwa kila siku.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  na baba wa mtoto anafurahia tu?

  Huyo mwanamke anatabia mbaya tu....
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye BOLD Kwa lugha ya kwetu ya kanbila la DONKHA linalopatikana kaskazini mashariki mwa TZ, hayo majini ni sifa anayopewa mtu jasiri, hodari, na anayemudu kuishi katika mazingira yoyote hata yakiwa magumu kiasi gani......LOL

  :focus: Huyo mama hayuko sahihi na anachokifanya ni unyanyapaa kwa mtoto, na hiyo itamfanya mtoto asijiamini kabisa.....
  Niliwahi kuandika hapa kwamba hakuna mtoto anayeitwa wa haramu wala kuadhiniwa......... Mtoto hawi mtoto eti mpaka sijui aadhiniwe, apigiwe bismilahi, au afanyiwe sijui mambo ya kimila au ya kidini........ huo ni utashi wa kibinadamu, lakini maumbile hayajui mtoto wa haramu wala wa halali.
   
 5. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ni kweli huu ni ukiukwaji wa haki ya mtoto, hivyo mama huyo anachofanya ni kumuathiri kisaikologia mtoto huyo.
   
 6. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  BADILI TABIA Baba wa mtoto hana ajualo kama unavyoelewa wanaume wengi huwa muda wao mwingi huishia kwenye mihangaiko ya kutafuta mkate wa siku, na binti kutokana na hali ya kutishwa kila siku hana ujasiri wa kumweleza baba yake, au pengine ni ile kuhofia kuvunja ndoa ya baba yake hivyo ameamua kuwa kimya.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  LOL... we Mtambuzi ni kiboko kwamba ni majini yenye sifa za uhodari, ujasiri nk.nk....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  angalau majirani wazungumze na huyo baba.....kumwokoa huyo mtoto
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  BADILI TABIA hizi nyumba za siku hizi mageti mawili mawili na uzio mkubwa hakuna ajuaye isipokuwa wachache wanaoingia ndani nyumba hiyo ndo wanaoweza sadia, nina mpango wa kuzungumza na baba mdogo wa mtoto huyo ili afikishe taarifa kwa kaka yake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  TaiJike una mpango wa kuzungumza na baba mdogo wa mtoto huyo labda we ndiye mama mdogo wa mtoto msaidie chalii atakushukuru sana kwani hana mtetezi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ni wajibu wangu kuwalinda watoto wa tanzania haijalishi ni mama mdogo au mkubwa kinachotakiwa ni haki ya mtoto itendeke kwani mama huyo alimkuta mtoto kabla ye hajaolewa na hata kama angezaliwa baada ya ndoa yake hastahili kutendwa hayo anayotendwa aise.
   
Loading...