Je, ni kweli wenye damu kundi O huwa hawana risk kubwa ya magonjwa ya maambukizi? Hasa ya magonjwa zinaa?

Kuna chakula cha asili umepewa tangu udogo na ni antibiotics ila huijui
Maana kuna wanyama wengine huwa hawaugui hivyo kwa majani wanayokula
Mtaalamu wa miti shamba akitokea anabadilisha taaluma kuwa na kuitwa mchawi, hapo ndio tatizo la kukosa wataalamu linaanza


Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Umenena Vyema Mkuu
 
ama kweli ashukuruwe aliye umba mpaka magroup ya damu hakika nimekaa nikawaza mno faida za haya magroup katika kundeleza uhai wa viumbe hapa duniani..

kwa hakika katika kila blood groups kuna faida zao na hasara zao...

kuna mkuu katoa sifa za hayo magrupu hebu atupe sifa za makundi yaliyo baki tujue ..wengie tuna tafuta wake huku ila kigezo lazima tuangalie na makundi aliyo nayo .. unaweza sikia kuwa kundi A ni weupe, na O ni weusi
UHUSIANO KATI YA DAMU NA TABIA

Je unajua kuwa tabia ulizonazo ni kutokana na kundi lako la damu?

Kwa kawaida kila binadamu yuko kwenye kundi mojawapo la damu kati ya makundi manne A,B,AB na O.

Makundi haya yanaweza kutumika kufahamu tabia za binadamu na jinsi hii yaweza kuwa rahisi na ya karibu zaidi kuliko kutumia nyota “astrology” kama ambavyo wengi wanafanya, na wataalamu wanasema tabia kwa uhusiano na kundi la damu ina uhakika zaidi kuliko wenye vyanzo vingine. Mbali na tabia, ukweli ni kwamba makundi yetu ya damu yanaweza kutuonyesha pia vile mtu anavyopendelea na asivyopendelea,
kazi anazopendelea, watu anaowapendelea na hata vyakula. Baadhi ya watafiti nchini korea wamebainisha kuwa hata namna tunavyopendelea kuketi hutegemea sana na makundi yetu ya damu, sasa tuangalie uhusiano huu
Damu kundi “A”
Hawa watu maranyingi huwa mifano ya kuigwa na wengi kwasababu ya kiu zao na upiganaji wao kwenye mafanikio, ni watu wema,wapole na wenye tabia njema. Pamoja na hayo ni rahisi sana watu hawa kupata msongo wa mawazo “stress” na kufikiria sana vitu. Wakiamua kujitoa kwa ajili ya kumsaidia mtu basi wanazama kabisa na wanaweza hata kujisahau wao.
Mazuri yao
Ni watu wanaopenda vitu vikamilike katika hali ya juu “perfectionists”, wanapenda mpangilio maalumu, wanapenda na wanaweza kuchambua mambo sawia, wanawajibika na kubeba majukumu yao,wana huruma na wako tayari kusaidia, waaminifu, ni wagunduzi, wanamaanisha, wavumilivu, na wenye tabia njema.
Mapungufu yao
Wasumbufu,wana hisia kali hata kwenye vitu vya kawaida, wakitaka kitu wametaka, wengine wana aibu,wengine wakimya zaidi na wanaopenda kujichanganya.
Kwenye maisha ya kijamii
Ni mtu ambaye unaweza kumwamini na kumtegemea
Anajali na kumaanisha
Wakati wote huepuka shari,misuguano na magomvi
Maranyingi hawapendezwi wala kufurahia sherehe zenye makelele na shangwe za ajabu ajabu,wanapendelea ukimya na utulivu.
Kazini
Unaweza kumwamini na kumtegemea katika majukumu
Wanapenda ufanisi wa kiwango cha juu kwahiyo kazi zao mara nyingi ni bora sana.
Bahati mbaya wanajali sana hata vitu vilivyo vidogo nahii huwafanya kuwa na msongo wa mawazo kirahisi.
Wasio waelewa vema watu wa kundi hili wanaweza kupata shida kufanya nao kazi
Kwenye mahusiano na mapenzi
Ni ngumu kidogo wao kufunguka na kushirikisha mambo yao.
Wanaweza kuonekana wenye aibu, au waoga.
Ukitaka kumchumbia au kuchumbiwa na mtu wa kundi ‘A’ unahitaji uvumilivu.
Wakiamua kupenda utawafahamu wakati wote na ingawa watakuruhusu ufahamu tu yale maeneoa ya maishani mwao ambayo wanajua unahusika, hawawi wazi katika kila eneo.
Ukweli mwingine kuhusu watu wa kundi ‘A’
Ni watu wabunifu na wenye ujuzi wa usanii “artists”
Wanalewa kirahisi sana, kilevi kidogo tu kitampelekesha sana
Wengi wao hupendelea kula mboga mboga “vegetarians”
Damu kundi “B”
Watu wa kundi hili maranyingi ni wenye tabia za kuasi na ni ngumu kuwazuia au kuwatuliza. Wanandoto na maono makubwa,wanasukumwa kwa kasi na kiu zao ingawa wanaweza kuwa wakali na wasumbufu na mara nyingine ngumu kukaa na kuzoeana nao. Wanakisimamia sana kile wanachokiamini hata kama ulimwengu mzima usimame kinyume nao.
Mazuri yao
Wanasukumwa katika kufikia malengo yao, wako kasi kiutendaji,wanapenda raha,wana hisia nzito , wanayatazama maisha katika mtazamo chanya , wanaweza kujisimamia na kujitegemea na hawahitaji ushirika au kukubaliwa na wengine.
Mapungufu yao
Wabinafsi sana,mara nyingine wanakwepa majukumu yao,wagumu sana kusamehe,wasumbufu,wanaweza kuwa wakatitili na wenye hasira za haraka.
Maisha yao kijamii
Maranyingine ni ngumu kushirikiana nao au kuwa nao maana wanapenda kufanya mambo yao wenyewe.
Kazini
Ingawa wanaweza kuwa na malengo mengi na maono pia lakini wanaweza kuwa wasumbufu na wagumu katika kushirikiana nao kazini. Ni ngumu kufanya nao kazi maana wanataka kufanya pekeyao.
Mahusiano na mapenzi
Unaweza kufurahi nao sana kwenye mapenzi lakini uwe tayari kuvumilia hasira zao kali na za ghafla. Vumilia hali yao ya kukwepa majukumu pia,fahamu kuwa wanaweza kuwa wakali, wakatili na wasio maanisha kile wanachokisema.
Baadhi ya ukweli wa kitafiti kuhusu watu wa kundi B.
Wanatabia ya utukutu.
Pamoja na baadhi ya mazuri yao bado wanaweza wasiwe watu wazuri kwenye kuwa mume, au kuwa wapenzi wazuri kwa wasichana wao. Hii ni kutokana na urahisi wa tabia za kukosa uaminifu kimapenzi na urahisi wa kuumiza mioyo ya wengine.
Wanatabia ya kupenda wanyama “they love pets”
Wana kinga kubwa na imara ya mwili katika kujikinga na magonjwa.
Wanafurahia zaidi vyakula vitokanavyo na wanyama kama vile maziwa “dairy products” n.k
Damu kundi “AB”
Kundi hili ni watu wenye haiba mchanganyiko, hawa huwa na tabia tofauti kuanzia kuwa waoga na wenye aibu hadi wengine ni wapenda mitoko na wacheshi,wako wanafanya mambo kwa kuongozwa na mawazo na wengine hawawazi kabisa kile wanacho taka kukifanya,hii inafanya watu wa kundi hili kuwa watu wa kushangaza sana mara unapokuwa nao.
Mazuri yao
Ni rahisi sana kuwa rafiki nao.
Wanachukuliana na mazingira haraka na kwa urahisi.
Wenye kufurahisha unapokuwa nao ingawa ni watu wasiotabirika.
Wana mawazo,wana akili sana,hupenda kuweka mambo yao kwa vitendo na pia huongozwa na misimamo ya kifikra.
Mapungufu yao
Wagumu katika kufanya maamuzi.
Wanasahau sana
Ni wenye hisia za kayumba “mood swing”, mara wana furaha mara wamekasirika.
Sio waaminifu.
Ni wapinzani,wabishi na wakosaji.
Ni watu wabinafsi.
Maisha ya kijamii
Wanaweza kuwa marafiki wazuri na wenye kufurahisha.
Maongezi yao ni yenye kuhamasisha nayenye akili na kufikiria kwa hali ya juu.
Kwa kutokuwa wenye kutabirika, wengine huhofia kuumizwa kihisia au kukatishwa tamaa au kuumizwa moyo na watu hawa, hususani pale wanapokuwa sio waaminifu.
Kazini
Wanaweza kuwafurahisha na kuwapa burudani mnapofanya kazi nao lakini sio watu wa kuwategemea sana,wanaweza kukuangusha kirahisi.
Mahusiano ya mapenzi
Kuwa katika mahusiano na mtu wa kundi la damu la AB kunaweza kuwa kwenye kufurahisha,unaweza usiwena nyakati nyingi za upweke. Pamoja na haya fahamu kwamba watu hawa wanaweza kuwa wabishi na wakosoaji na maranyingine maneno yao yanaumiza. Mpenzi wa mtu au watu wa hivi lazima aelewe jinsi hisia zao zilivyo na zinavyobadilika mara kwa mara,na pale inapobidi basi uwetayari kuwapa nafasi wanayostahili ili usijiumize sana.
Baadhi ya ukweli wa kiutafiti kuhusu watu wa kundi hili.
Ni watu wazuri kwenye mambo yahusuyo fedha.
Maranyingi wanajihusisha na wanaopendendelea shuhuli za kisanaa au mambo yenye sanaa ‘arts’
Ni watu wanaoaminika kuwa wabinafsi zaidi hata katika uchangiaji wa damu,watu hawa wanaweza kupewa damu na mtu mwingine yeyote ila wao hawawezi kumpa damu yeyote isipokuwa mwenzao wa AB.
Kama walivyo watu wa kundi ‘A’ na kundi ‘B’,watu wa kundi la damu ‘AB’ hupendelea vyakula vya mboga mboga “vegetables” na pia vyakula vitokanavyo na wanyama “dairy products”
Kundi la damu aina ya O.
Hawa maranyingi wanajitahidi kuwa mahodari na mashujaa katika mambo tofauti. Mara zote kiu yao ni kuwafurahisha na kuwapendeza watu wengine ni wenye moyo wa uongozi wenye kiu ya kuwaona rafiki zao wakiwa wenye furaha wakati wote. Sio wagumu wa mabadiliko, wako tayari kubadilika, ni wenye mawazo mapana naya wazi, sio wagumu kifikra na ni marafiki wazuri.
Faida zao
Ni wenye ujasiri, wanashindana katika mambo mengi mfano mambo ya maendeleo, hufanya kazi sana na kwa bidii, ni waaminifu, wanaweza kujieleza, ni marafiki wazuri, wanasamehe, mitazamo yao ni chanya, huweza kuhisi au kuonamambo hata kabla hayajatokea,wanakiu ya kufahamu na kudadisi na pia niwatu wema na watoaji.
Mapungufu yao
Maranyingine wanaweza kuwa wenye fujo, wanaopenda sifa, wanavutia vitu upande wao, wanaepuka au kukwepa majukumu,unaweza kuona hawa wanaigiza mambo, wakitaka wametaka hadi wapate na nirahisi kuwaondoa kwenye kile wanachokifanya “easy to be distracted”.
Maisha ya kijamii
Ni marafiki wazuri na unaoweza kuwategemea, ni waaminifu, ni wawazi,ingawa mara nyingine wanaweza kukuudhi, pia wakati mwingine wanatamani kusikilizwa wao tu.
Kazini
Wana kiu ya mafanikio, hufanya kazi kwa bidii ingawa kukatishwa tamaa na kupoteza hamasa ya kazi kirahisi sana. Mara nyingine ili wafikie malengo ni vema wakisimamiwa kwenye kazi wanayo fanya badala ya kuachwa wafanye wenyewe..
Mahusiano ya mapenzi
Ni watu wenye mvuto wa kimahaba pia watu hawa wana hisia Kali za kimapenzi wanaweza kuonyesha mapenzi kwa wale wanaowapenda ila ni vema ukafahamu kuwa watu hawa hutarajia upendo wa jinsi ile ile wao wanavyoonyesha upendo kwako bila hivyo utakosana nao.
Ukweli wa kitafiti kuhusu watu hawa
HAWAPATI MARADHI KIRAHISI
Kwanza ifahamike kuwa watu wenye damu kundi hili wamegawanyika mara mbili ambazo ni damu kundi “O” chanya (O positive) na kundi “O” hasi (“O” negative) mgawanyo huu umetokana na mgawanyo wa kitaalamu ambao huitwa “rhesus factors” ambao ndio unaotumika kugawanya makundi ya damu.
Kwa ujumla kundi hili la damu liwe hasi au chanya halina proteins maalumu zilizomo ndani ya damu ambazo huitwa “antigens” ambazo ndizo mara nyingi ni rahisi kushika magonjwa isipokuwa lina “antibody” ambazo ndizo kinga mwili zinazopambana na maradhi ndiyo maana damu kundi “O” linaitwa “Universal Donor” damu kundi lolote linapokea.
Na kwa wakati fulani maradhi yanayowasumbua watu wenye damu kundi hili ni malaria, kichwa na mafua na wengine husumbuliwa sana na ugonjwa wa kutoka damu za pua (Rhinits) au wengine huita kambaku ambao husababishwa na kula nyama yenye lehemu nyingi (cholestrolel) ambazo ni nyama ya ng’ombe, kondoo, samaki aina ya dagaa, uwono na mboga ya majani inayoitwa kisamvu na wakati mwingine maziwa ya ng’ombe au kutembea kwenye jua kali sana au kutumia manukato yenye harufu kali.
NI WAPENDA NGONO
Watu wenye damu kundi hili wana hisia kali sana za mapenzi hii ni kutokana wana homoni nyingi, hali hii inawapelekea kupenda sana ngono na vile vile huwa wakizaa wanafanana sana na watoto wao iwe sura, tabia au mwendo iwe mwanamke au mwanaume
Watu hawa Mara nyingi huwashwa masikio yao kwa ndani hivyo Mara nyingi wanajikuna masikio
Wanaaminika huwa na tabia za kijeshi.
Wengi wao kwa asili ni watu wa kupenda michezo.
Wanaaminika kuwa watu wema na waliotayari kusaidia mtu yeyote, hata katika uchangiaji wa damu ‘watu wa kundi ‘O’, wanaweza kumpa damu mtu mwingine yeyote.
Wanapendelea na kujisikia raha wanapokula nyama “meet lovers”.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Ushimen,
Ha ha ha haaa ha ha haaa
LOh! Umeua Kwakweli
Yaaani Sema Sasa Mimi Nimeoa Unajua Mke Wangu Mrefu Mweupe Afu Mimi Mweusi
Yaani amejaazia na Kajigawa Kisawasawa yaani Mpaka Nikitembea Naye Najikuta Ninazo Hata Kama Sina.

Tunawatoto Watatu lakini Naona Bado Kama Ndio kwaaanza Nimemtoa Ukweni Leo Asubuhi Tyuu
sasa Nawaza Ninunue Hata kapaso Kamoja Kwakweli Ili Niwe Namficha Maana Nikaamua Kujiajili Maana kazi Ya Kuajiriwa Nilikuwa nasafiri sana.

Nikaona Isiwe Kesi Wacha Nijiajiri mwenyewe nijilindie vyangu.

Yaani Umenikosha Japo samo fac naona Nikweli Na Zingine ni dondoo Tyuuu
niunganishe kwa mdogo ake wa kike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Damu kundi "O" limegawanyika katika makundi mawili ambayo ni "O" Negative(Hasi) na "O" Positive (Chanya).


Katika kundi hilo wenye kundi Chanya wana Tabia nyingi sana amabzo weyewe hawajijui kama tabia hizo ni asili ya damu kudi hilo.

1.WENGI NI WAPENDA NGONO

Asilimia kubwa ya watu wenye kundi hili la damu wanapenda sana ngono kuliko kitu kingine,haswa wanaume wenye damu kundi hili wanapenda wanawake wenye makalio makubwa, wao hawaangalii sura,ili mwanamke amaye amejazia nyuma ndio wanavutiwa zaidi.

Kwa wanawake wenye damu kundi hili pia nao wanapenda sana mchezo huu,wana mvuto wa kupendwa nna wanaume.

2.NI WASEMAJI SANA

Asilimia kubwa ya watu wenye damu kundi hili wanapenda sana kusema(ni wachangamfu) haswa katika jamii ya watu.

3.NI WATOAJI WAZURI

Wengi wa watu wenye kundi hili wana moyo wa kutoa kuliko kupokea,huwa hawapendi wenzao wapate shida ila wengi wana asili ya kuutangaza msaada wao ukiwaudhi.

4.MARADHI.

Maradhi makubwa yanayowasumbua ni malaria,kichwa kuuma upande mmoja(kipanda uso),mafua au kutoka damu za pua haswa wanapokula nyama,maziwa.

5.NGIRI
Kwa wanaume wenye damu kundi hili asilimia kubwa wana maradhi ya tumbo kujaa gesi haswa wanapokula baadhi ya vyakula haswa chipsi.

6.WANAFANANA NA WATOTO WAO
Wengi wakizaa huwa wanafanana sana na watoto wao iwe sura,tabia au mwendo na mara nyingi katika maisha yao huishi au kuzaa na mpenzi zaidi ya mmoja.

ALAMA ZAO
Alama kubwa za watu wenye damu kundi hili ni kuwasha na masikio kwa ndani,fangasi za vidole vya miguu kwa wanaume na kwa wanawake vidole vya mikono haswa wakifua,pua kuwasha kwa ndani.

Na Mwangaza Blog
Daaaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom