Je, ni kweli watu weusi tuna akili ndogo?

Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
3,971
2,000
Utakubalije kutekwa kiakili na mzungu ? Waĺikuja Afrika na kutudanganya na dini zao , ni kwa nini na wewe mwafrika usingeenda kwao na kuwadanganya ? Na kama ulivumbua kitu ulishidwaje kutetea hoja yako ? Wametuzidï !!! Ulïpoambiwa Yesu alifufuka huko kwao si ulikubali bila kuhoji ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
2,173
2,000
Interior design was Benz ni mweusi,
Mweusi?

Hata hivo Siasa za nchi zenu hazitabiriki, hakuna siasa bora Barani kote! wacha waende tu, wakatanue uzunguni hata ningekuwa mimi naenda kweli!! hapa watakupiga majungu, uchoyo wa fedha, kijicho, dharau! hata kutupiwa majini ukafie Baharini huko! utafikia kuacha kazi ukatafute Waganga au uzunguke makanisani kuombewa kila uchao!

Kipindi cha Industrial revolution nchi zote za Ulaya, ilikuwa Rhuksa tena kwa msisitizo wa serikali na pesa juu unapewa, kwa kubembelezwa na kupewa mbinu pia Mafunzo mwanana ''nendeni vijana wetu mkalete Maarifa mapya'' kuiba utaalamu popote pale Ndani na nje ya nchi!

Walifanikiwa sana hata kuiba utaalamu wote wa Misri ya kale wakapeleka Ulaya, kumbukumbu za Africa zote ziko Ulaya, wakatunga na sheria wao ndiyo wenye hati miliki wa Egyptology excavations mpaka leo, ajili ya roho za kutu km jiwe. mwizi wa vyeti fake maarufu kutokea Misri alikuwa Aristotle na kundi lake kubwa sana tuliwapa tukawanyima Wa Africa wenzetu, km leo Wahindi wenye vyeti fake wanapeta weusi wanalia njaa!

Angalia watu wenye ubongo mweusi, wana waita majina ya hovyo wataalamu wao! eti '' Vyeti fake'', na wengine wamesukumwa tu kwa chuki na wananchi weusi wanashangilia kweli kweli, na kumuunga mkono, hapohapo kuna kundi lingine analitetea eti hawa hkn haja ya kuwasema sababu wana Bunduki. Mtu kwa kutumia cheti fake amekuwa, Daktari, Mwanasheria, au Engineer wa miundo mbinu miaka bwena! hivi nchi haimuhitaji mtu km huyu anazalilishwa ajili ya karatasi ya form four fake? kweli?

Anaye fanya hayo ameiba kura kuingia Ikulu! yaani ni fake juu ya fakes, na hawa wa hivi ni mazao ya watanzania hao! hao! wamesoma hapo hapo kwenu UDSM. ndiyo kimetoa haya makapi yasiyojua kuongea English Fasaha!

Viongozi wengi wazuri wa Africa waliokuwa na moyo hasa wa kuinua nchi zao na watu wake kwa hali na Mali ni zao la Wazungu walikuwepo miaka ya 60 kurudi nyuma. Hawa wa leo ni viranja wale wa secondary wakurupukaji, watemi kama wale wa Nyakato secondary Bukoba. Maarufu kama INDUNA.
 
bheri

Member
Mar 1, 2018
51
125
Mtazamo wangu, utofauti tunaoupata kwenye mfumo wa elimu, mpaka kesho sijawahi kukubaliana na elimu inayotolewa hapa Tanzania unakuwa tuna mainjinia lakini hawawezi kuunda hata kusolve matatizo ya Barbara za mitaa kujaa maji. Pili ni mfumo wetu was utawala nao una matatizo makubwa Sana hawako siliasi wako Kwa ajili ya kuridhisha matumbo yao na ndugu zao hawawazi kuhusu future ya Muafrika iweje wanawazia familia zao zaidi. Ngoja Kwanza niishie hapa
 
Below 40

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
306
500
Kwanza kabisa binaadamu wote tumewekewa ubongo sawa, nikimaanisha kua kilakitu nilichonacho kwenye ubongo wangu basi nawewe unacho na mwanasayansi Leonardo da vinci alikua nacho.

Sasa kwanini inaonekana da vinci alikua na akili kuuubwa kuliko wengine? kinachotutofautisha ni jinsi ubongo wetu tunavyoutumia katika kufikiria, pia vipaumbele vya matumizi ya ubongo wetu. Lakin kuuubwa zaidi tulilotofautiana na mwanasayansi da vinci ni kujaliwa karama/vipaji vingii katika uwezo wa hali ya juu, na hapo ndipo alipotupiga bao da vinci.

(aliitumia akili yake vizuri pia alijaliwa karama nyiingi) leo hii mimi nawewe tunaweza kufuata nyendo za da vinci tukamfikia na kumpita mbali kabisa mfano Arristotle alimuona Plato ni mtu mwenye uwezo wa hali ya juu na kweli plato alikua na akili kuubwa sana ila mwanafunzi wake arristotle aliweka commitment hadi akamshinda mwalimu wake plato uwezo.
sasa kama tunazo na hatuzitumii kuna tofauti gani na kutokua nazo tu.
 
LexPaulsen

Senior Member
Jul 30, 2018
172
500
Akili ni nini? Ni ubongo ndani ya kichwa au matokeo ya kile ubongo unaweza kufanya?

Ubongo wa binadamu wote ni sawa ukiachilia mbali wale kama wa milembe waliokatika fuse kadhaa.

Kitu pekee kinachosababisha ubongo wa kundi flani la watu ulete matokeo makubwa kuliko kundi lingine ni "Utamaduni" aka CULTURE. Najua tutachukulia culture ni vitu rahisi kma mavazi, lugha, chakula etc lakini utamaduni wa kundi flani unacontrol karibia kila nyanja ya maisha kuanzia ustaarabu(civilization), kupokea na kutumia maarifa(knowledge assimilation), uvumbuzi(innovativeness) etc.

In general, culture ina determine namna na approach ya kufikiri na kibaya zaidi ni kwamba culture unazaliwa kwayo, unaikuta unaishi humo unafundishwa na babayo na mamayo, it becomes part of you.

Conclusion ni hii "Compare and contrast African culture versus Western Culture katika maeneo tofauti utagundua kitu. Tuna ubongo sawa ila fikra sio sawia kutokana na tamaduni zetu kufunga au kufungua milango ya kifikra tangu ukiwa mtoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Blackman

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
752
250
Binafsi naamini wote tuna akili sawa; I mean, generally hakuna mwenye akili ndogo wala kubwa kati ya mtu mweusi na mtu mweupe. Isipokuwa nitakubaliana na yule atakaesema sisi watu weusi akili zetu hatuzitumii ipasavyo, kwa uwezo wake unaotakiwa. We don't usually unlock our fully mental capabilities ila akili tunazo sawa tu na whites.

Sasa swali ni kwanini hatuzitumii akili zetu ipasavyo? Ukiniuliza mimi nitakwambia ni matokeo ya kimkakati ya waliotutawala. Walihakikisha wanatubadili kiakili kwanza, once and for all, ndo maana walitumia mbinu za kiimani, kupandikiza hofu. It's all about mind game. Walijua mtu mwenye hofu ni rahisi sana kumpeleka kama unavyotaka.

Ukitaka kuamini kuwa ni mchezo wa akili tu - Chunguza utagundua kuwa South Africans wanajiona bora kuliko mataifa ya nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, North African wanajiona bora kuliko South Africans, Waingereza wanajiona bora kuliko Wamarekani, Wajapan wanajiona bora kuliko Wakorea and the list goes on. Na sababu si kwamba wana akili kubwa... naaaaah... - bali ni maendeleo. Baada ya kutawaliwa kiakili tulishindwa kufanya maendeleo na tunashindwa kufanya maendeleo kwasababu nyingi. Mfano walituletea dini ili tuwe submissive; matokeo yake mpaka leo watu tuko busy na dini ambazo wao waliozileta hawana habari nazo. Wao wako busy viwandani wanaunda magari, sisi tuko busy makanisani tunaomba miujiza ya magari. Wao wako busy na cloud seeding sisi tunaamini mvua inaletwa au kuzuiwa na mwenyezi Mungu.

Sisi mtu ana PhD lakini bado anaenda kwa mganga wa kienyeji ili mambo yake yaende,... tatizo hapo sio akili ndogo bali matumizi ya akili ni madogo. Kama unabisha... tuingie mtaani leo tufanye utafiti ni Watanzania wangapi wanaamini kuwa wanaweza kutegemea akili zao kwa 100% pasipo kutegemea kitu kingine chochote katika kufanikisha mambo yao. I am sure, wengi wana ile 'hofu ya Mungu' waliyofundishwa kanisani ambayo sote tunajua inakukataza usizitegemee akili zako. Now, do you expect mtu mwenye imani hii ataitumia akili yake sawasawa? Never.

Kafanye utafiti huo huo kwa whites; kawaulize kama wanaweza kutegemea akili zao kwa 100% pasipo kutegemea kitu kingine chochote katika kufanikisha mambo yao. You'll be surprised brother.

Kwa hiyo, hii notion itabadilika siku tuki-catch up to their speed of development. Otherwise sisi wenyewe tutaendelea kujidharau hata kabla wao hawajatudharau. Jiulize, kwanini kila kitu kinachoonekana ni bora tunakiita 'cha kizungu' - yaani mpaka kuna panzi wa kizungu eti... seriously?!!!!???

Tuache woga, tutumie akili zetu sawa sawa. It is "THINK AND GROW RICH"... sijawahi sikia "BELIEVE AND GROW RICH" au "PRAY AND GROW RICH". Sisemi watu wasisali au kuamini, ila ni vyema tukatumia akili zetu hata katika imani pia.

They are not born better than us, but they use their minds to the max to become better than us. So it's NURTURE not NATURE.
walio tutawala sisi si ndio walio litawala hata bara la ASIA? Je ASIA hawakupeleka dini kule?
 
Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
5,696
2,000
Waafrika wengi wanasumbuliwa na msongo wa mawazo na ukosefu wa furaha mfano Tanzania. Hivyo vitu viwili kamwe haviwezi kukufanya ukawa bright katika utendaji kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
boufer

Member
May 9, 2014
26
45
James Watson,mwanasayansi maarufu duniani na mshindi wa nishani ya noble katika tiba mwaka 1962, ameleta mjadala mkubwa kwa madai kwamba inaelekea mtu mweusi ana akili ndogo kuliko mtu mweupe. Kauli hiyo imeshikiliwa bango na wapinzani wa ubaguzi wa rangi kwa madai kwamba inamdhalilisha mtu mweusi.

Hata hivyo Watson si mtu wa kwanza kusema hivyo isipokuwa yeye kaisema kisayansi zaidi. Siku za nyuma Waziri Mkuu mmoja wa Japan alipata kusema maneno kama hayo kwamba anatilia mashaka uwezo wa mtu mweusi. Waziri mwingine pia alishanukuliwa anasema hivyo. Wote baadaye waliomba radhi ila ujumbe ulifika.

Chika Onyeani katika kitabu chake cha The Capitalist Nigger naye anashangaa ni kwanini Mwafrika atukanwe namna hiyo na mawaziri wa Japan, lakini bado waendelee kununua bidhaa kutoka japan. Pia anasema jamii nyingi za watu Weusi zinafanana kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano ukikutana na Muamerika mweusi aliyezaliwa marekani au carribean au afrika kwenyewe bado wanatabia zilezile ambazo zinatia shaka kama kweli akili za mtu mweusi si ndogo kwa kiasi fulani.

Ukianza kuangalia matokeo mbalimbali yaliyotokea Afrika enzi za miaka ya nyuma utaanza kuwa na wasiwasi kuhusu hali ya uelewa wa mtu mweusi.Historia inaonyesha kwamba ,hadi karne ya 16 kiwango cha maendeleo kati ya nchi za Afrika na ulaya kilikuwa sawa

Tunaambiwa pia kwamba miaka ya 1960 baadhi ya nchi za Afrika zilikuwa zimeendelea kimaendeleo au sawa na nchi za Asia ambazo leo ziko mbali kimaendeleo.Bado unajiuliza ni wapi kwenye matatizo? Kwanini waafrika tuachwe kila leo?

Ripoti za umaskini duniani zinaonesha kwamba umaskini umepungua kwa kiasi kikubwa lakini kwa Afrika unaonyesha kuongezeka.Mbaya zaidi maskini wa Afrika wapo kwenye dimbwi zito ambalo si rahisi kujinasua.Utafiti huu unafanywa kulinganisha na nchi za India na China ambazo zina idadi kubwa sana ya watu

Ukipima baadhi ya kauli za hawa tunaowaita wabaguzi utagundua kuna ujumbe wanawasilisha.Ukichukua Tanzania kama mwakilishi wa Afrika utaweza kugundua haya.Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi lakini si nufaishi kwa mwananchi wake isipokuwa wawekezaji wanakuwa na mamlaka makubwa juu ya rasilimali hizi.Kuna mito,Madini na misimu lakini bado tunaagizia dawa kutoka nje.SHAME!!

Watu wanajilundikia mabilioni ya Fedha kwenye akaunti zao za benki zilizopo nchini au hata nje ulaya wakati shule ya AZANIA iliyoko katikati ya jiji kuu la nchi ina wastani wa tundu moja la choo kwa wanafunzi 300

Bado tunazipa likizo ya kodi kampuni kubwa huku tukifuatilia vikodi vidogo vidogo.Kampuni kubwa zinaruhusiwa kubeba hasara na kuipeleka kwenye mahesabu ya mwaka ujao kwa miaka KADHAA lakini hiyo hiyo kampuni inaendelea kufanya biashara.Hapa sisi ni wakusanyaji wazuri wa kodi au wakwepaji wazuri wa makampuni makubwa?

Inafaa tujiulize kunani kwenye akili zetu?Tunasema tuna mafuta lakini tukitaka kuyachimba tunamwita mzungu japokuwa tumekuwa tukizalisha wakandarasi na wanajiorojia kila mwaka.Lazima tujiulize kama elimu yetu ina mushikeli au la!Sasa hivi tunajigamba kuwa na vyuo vikuu 30 lakini bado tunaagizia vijiti vya kuchokonolea meno toka Malaysia. Kweli??

Kabla ya kushika mabango na kuwalaani wabaguzi wa rangi lazima tujiulize kwanza ni wapi tumekosea na sababu za kukwama kwetu.Tusikimbilie kulaumu wazungu kwa kuleta ukoloni na ukoloni mambo leo.Malaysia na Ghana zote zilikuwa koloni za muingereza na zilipata uhuru mwaka 1957 kwa pamoja lakini leo hali ni tofauti.

Wamalaysia walikuwa wanakwenda Ghana kujifunza kilimo cha mawese. Leo hii Ghana wanajifunza kila kitu toka Malaysia kikiwemo kilimo cha mawese.Wazungu wanaopinga kauli za WATSON sio kwamba wanasikitika sana bali wanaonesha kukasirika usoni lakini moyoni wanasema ni kweli hawa wanaujinga wao mkubwa.Wanatutetea ili waendelee kutuvuna.Hawataki tukaechini na kujitathmini tulipoenda mrama.

Nachukia kuitwa kiumbe dhaifu hasa kiakili.Nachukia kwa sababu naupenda uafrika na WEUSI wangu.Nawapenda waafrika wenzangu.Nachukia wanapoambiwa kwamba wanaubongo dhaifu. Lakini nahisi kuna mahali kama watu WEUSI tumekosea

Kama mtu anaiba mabilioni ya fedha za umma kwenye nchi maskini na kuyaweka ulaya au kewekeza mahali popote,huku kukiwa na wananchi wanakufa kwa kukosa madawa hospitalini basi kuna ulazima wa kujiuliza tuliko na kasoro.Kama viongozi wanawaibia wananchi wao waliowachagua kuwawakilisha bila aibu yoyote inabidi tuhoji akili zetu.Kama wananchi wanaridhika na hila za viongozi wao bila ya kuchukua hatua madhubuti basi tuhoji akili zetu

JE? Watson aombe radhi

Hata kama Watson ataomba radhi kama mawaziri wa Japan atakuwa amepeleka ujumbe mzito kwa watu WEUSI kujichunguza.Huu ni ujumbe mzito kwa taifa letu la Tanzania.Mimi ni miongoni mwa wasioamini upuuzi wa James Watson, kwamba waafrika tuna akili ndogo.

Historia inaonyesha kwamba chuo kikuu cha kwanza duniani kilikuwa Afrika,kule Mali.Uvumbuzi wa hisabati ulitoka Afrika,hata mtu wa kwanza duniani anaaminika kuishi Afrika.Pia MAAJABU mengi yapo kule misri (pyramids)

Wapo waliokwenda mbali na kusema kwamba hata YESU KRISTO alikuwa mtu mweusi wa misri na kwamba ndiyo sababu SIMON WA KRENE,ambaye alikuwa mtu mweusi alimsaidia YESU kubeba msalaba.Ilikuwa ni huruma ya kuona mtu mweusi mwezake anateswa.

Jamani ni wapi tumekosea??

Sasa je,ni kweli watu WEUSI tuna akili ndogo?? View attachment 1314061

Sent using Jamii Forums mobile app
Absolutely,watu Weus tuna akili ndogo wala si uongo kwa sababu lukuki na baadhi ni hzo ulizozitaja
 
boufer

Member
May 9, 2014
26
45
Binafsi naamini wote tuna akili sawa; I mean, generally hakuna mwenye akili ndogo wala kubwa kati ya mtu mweusi na mtu mweupe. Isipokuwa nitakubaliana na yule atakaesema sisi watu weusi akili zetu hatuzitumii ipasavyo, kwa uwezo wake unaotakiwa. We don't usually unlock our fully mental capabilities ila akili tunazo sawa tu na whites.

Sasa swali ni kwanini hatuzitumii akili zetu ipasavyo? Ukiniuliza mimi nitakwambia ni matokeo ya kimkakati ya waliotutawala. Walihakikisha wanatubadili kiakili kwanza, once and for all, ndo maana walitumia mbinu za kiimani, kupandikiza hofu. It's all about mind game. Walijua mtu mwenye hofu ni rahisi sana kumpeleka kama unavyotaka.

Ukitaka kuamini kuwa ni mchezo wa akili tu - Chunguza utagundua kuwa South Africans wanajiona bora kuliko mataifa ya nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, North African wanajiona bora kuliko South Africans, Waingereza wanajiona bora kuliko Wamarekani, Wajapan wanajiona bora kuliko Wakorea and the list goes on. Na sababu si kwamba wana akili kubwa... naaaaah... - bali ni maendeleo. Baada ya kutawaliwa kiakili tulishindwa kufanya maendeleo na tunashindwa kufanya maendeleo kwasababu nyingi. Mfano walituletea dini ili tuwe submissive; matokeo yake mpaka leo watu tuko busy na dini ambazo wao waliozileta hawana habari nazo. Wao wako busy viwandani wanaunda magari, sisi tuko busy makanisani tunaomba miujiza ya magari. Wao wako busy na cloud seeding sisi tunaamini mvua inaletwa au kuzuiwa na mwenyezi Mungu.

Sisi mtu ana PhD lakini bado anaenda kwa mganga wa kienyeji ili mambo yake yaende,... tatizo hapo sio akili ndogo bali matumizi ya akili ni madogo. Kama unabisha... tuingie mtaani leo tufanye utafiti ni Watanzania wangapi wanaamini kuwa wanaweza kutegemea akili zao kwa 100% pasipo kutegemea kitu kingine chochote katika kufanikisha mambo yao. I am sure, wengi wana ile 'hofu ya Mungu' waliyofundishwa kanisani ambayo sote tunajua inakukataza usizitegemee akili zako. Now, do you expect mtu mwenye imani hii ataitumia akili yake sawasawa? Never.

Kafanye utafiti huo huo kwa whites; kawaulize kama wanaweza kutegemea akili zao kwa 100% pasipo kutegemea kitu kingine chochote katika kufanikisha mambo yao. You'll be surprised brother.

Kwa hiyo, hii notion itabadilika siku tuki-catch up to their speed of development. Otherwise sisi wenyewe tutaendelea kujidharau hata kabla wao hawajatudharau. Jiulize, kwanini kila kitu kinachoonekana ni bora tunakiita 'cha kizungu' - yaani mpaka kuna panzi wa kizungu eti... seriously?!!!!???

Tuache woga, tutumie akili zetu sawa sawa. It is "THINK AND GROW RICH"... sijawahi sikia "BELIEVE AND GROW RICH" au "PRAY AND GROW RICH". Sisemi watu wasisali au kuamini, ila ni vyema tukatumia akili zetu hata katika imani pia.

They are not born better than us, but they use their minds to the max to become better than us. So it's NURTURE not NATURE.
Mkuu licha ya kututawala sis hatuwez fana akil na mzungu,yeye ndo alichkua bot akaja hku na si sisi kwend kwao,jiulize kwanin afikirie kuja hku na sio sis kwenda kule?na hyo karne ya 16 mnayosem tulfanana kmaendeleo si kweli,huwez kuwa na mshale ukajfananish na mweny gobole eti kis tu zote ni silaha,akil zetu ni ndog hlo alina ubshi na wala wazung hawajahuska na kufany akil yet iwe ndog ila ni la mda mref tu
 
Computer Virus

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
343
1,000

Siwezi kukukatalia ikiwa wewe unajiona una akili ndogo. Lakini hiyo haitufanyi sisi sote tuwe na akili ndogo - acha uvivu, pitia historia sawasawa halafu angalia kwanini walikuja huku kwetu... nini kiliwafanya waje huku, na wakati wanakuja, kule kwao hali ilikuwaje ukilinganisha na kwetu huku n.k Kama sio mvivu wa kusoma nakuhakikishia utapata majibu yote hayo. Jibu rahisi nakupa - hatukwenda kwao kwasababu hatukuwa na haja ya kwenda; twende kufanya nini wakati tulikuwa tunajitosheleza kwa kila kitu???🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️

Labda kwasababu akili tunayoiongelea haionekani ndo maana watu mmegoma kuelewa, lakini ngoja nijaribu hivi: Bila shaka unaufahamu muda (time) si ndio?. Dunia nzima tumepewa masaa 24 kwa siku haijalishi wewe ni mzungu au black; Sasa, tunakubaliana kuwa kuna watu wanayatumia vyema hayo hayo masaa hayo 24 ambayo kila mtu kapewa na wanafanikiwa sana, wakati huo huo kuna watu kila siku wanalalamika kuwa 'muda hautoshi'!! Kwa hiyo kama muda ungekuwa hauonekani kama jinsi akili ilivyo, nina uhakika watu mngesema mzungu kapewa masaa mengi kuliko mtu mweusi!!! 😂 😂 😂

Labda nikupe hii: Historia iliandikwa upya ili kuficha ukweli wa mambo. Vitabu vya Historia vingi ni vile ambavyo vimeandikwa na wazungu, na wao wanaandika kwa makusudi maalumu.... wanajua mkifundishwa tangu mkiwa wadogo kuwa wazungu walitutawala itawadidimiza kiakili; hamtataka tena kuumiza ubongo kuwa wabunifu zaidi yao n.k. Ukijumlisha na mifumo kandamizi waliyoijenga, ndo kabisa - tunapata watu kama wewe ambao milele wataamini mzungu ana akili kuliko sisi.

Siku tukiacha huu ujinga, tutafika mbali sana. Na ndio maana nitakapokuwa Rais, haraka sana nitafuta somo la Historia au la sivyo nitabadilisha aina ya Historia tunayosoma. Eee si ndio, asa unanifundisha kuwa mzungu alinitawala - kwa hiyo??🤷‍♂️ Inanisaidiaje katika ubunifu, inanisaidiaje katika kutafuta mafanikio, inanisaidiaje katika kujenga uchumi .... sana sana inazalisha wanasiasa wa hovyo tu.
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
1,594
2,000
Mimi ni miongoni mwa wasioamini upuuzi wa James Watson, kwamba waafrika tuna akili ndogo.
Kwa nini huamini wakati ukweli haufichiki?

Mfano Nyerer alitufundisha sana uzalendo na Uafrika wa kudumisha utamaduni wetu.
Sasa nenda Kule Bungeni ukaone liledude linaloitwa SIWA , utamaduni wa Muengereza ,tumeshindawaje kuondokana nalo jidubwana lile na kubuni kutu chetu wenyewe ?.

Nenda Mahakamani utakuta Sheria za Muingereza ndio hutumika kule, Tunashindwaje kuwa na Aina ya mfumo wa sheria za kiafrika? zisizokuwa na mfumoule wa Kikoloni?

Nenda Msunbiji, hadi leo wantumia lugha ya Kireno wamshindwaje kukuza lugha zao z Asili na kuwa na lugha za taifa za asili ya Afrika.

Nenda chuo kikuu DSM na wizara ya elimu Tanzania, tunasoma elimu kwa lugha ya kigeni hadi leo miaaka 60 baada ya uhuru

wakati sisi tuna lugha yetu ya Kiswahili kama lugha ya Taifa, tunashindwaje kujinasua hapo?

Huamini tuu kuwa hatuna akili timilifu?

Tazama nchi zote zilizoendelea duniani, Elimu hufunzwa kwa Lugha zao za Kienyeji na si kwa lugha za kigeni, ndo maana tunaendelea kubaki nyuma.
Mf. Iran wanasoma kwa Kifursi
Uturuki kwa Kituriki
China kwa kichina
Germany kwa kijerumani,
Sweeden kwa ki Swedish
Holand kwa Kidachi

Tuliobaki ni sisi waafrika.
Tunasoma kwa Lugha za Kifaransa, Kireno, Kiarabu au Kizungu.
Huko ndio kuonesha uwezo wetu kuwa ni Muflis wa akili

nishia hapo kwa sasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom