Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,270
- 105,469
Suala zima la race si ndilo hilo hilo la weusi na weupe?Kwa maana hiyo basi hatuna universally accepted definition ya "mtu mweusi" na badala yake kila mtu ana definition yake kulingana na muono binafsi.
Lakini mkanganyiko huu wa kutokuwepo kwa tafsiri sahihi ya mtu mweusi uko kwa watu waliochanganya race pekee(biracial people) na wala sio kwa mtu asiyechanganya race kama mimi hivi au wewe.
Kwa hiyo kumbe mimi au wewe ni mfano sahihi wa mtu mweusi.
Tukisema twende ndani zaidi kwa minajili ya kibailojia basi tutarudi kule kule kwenye mkanganyiko mfano ni hapo kwa huyo mwana mama Sigrid Johnson.
Sent using Jamii Forums mobile app
Na lenyewe ni la utunzi wa watu.
Kuna watu wengi sana wa pwani, wanajiita weusi, tunawaona weusi, lakini ukiwapima ki DNA wana viasili vingi tu vinavyohusishwa na waarabu.
Watu wamechanganyikana, wamechanganyikana sana, wamechanganyikana sana kwa maelfu na maelfu ya miaka kiasi kwamba kwa sasa tunajiwekea hadithi tu za "mtu mweusi".
Katika hao wanaoitwa weusi wenyewe kuna jamii kibao tofauti, Hottentonts, Nilotic, Bantu etc.
Haya mambo ukiyafuatilia kwa undani, utaona dhana nzima ya "watu weusi" inakuwa simplified kuliko facts zilivyo. Ni dhana ya kisiasa na kisosholojia zaidi ya kibaiolojia.