Je ni kweli watu weusi ni wajinga,wabinafsi na wachoyo??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni kweli watu weusi ni wajinga,wabinafsi na wachoyo???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Future., Jan 8, 2011.

 1. T

  The Future. Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu great thinkers, nimesoma makala ya dee lee mmarekani inayoitwa BLACKS DONT READ,humo kasema kua utafiti unaonyesha watu weusi hapendi kusoma vitabu na ukitaka kuficha siri za mafanikio kwa weusi we ziweke kwenye vitabu kwa sababu hawasomi, pia tuna asili ya ubinafsi,uchoyo na ujinga hivyo basi wazungu wanatumia kama silaha kumiliki mali zetu na kutu tawala bila nguvu nyingi kama walivyotumia kuingiza ukoloni, watawatumia viongozi wetu kutuibia na kwavile sisi ni wajinga na wao ni wabinafsi na wachoyo mambo yataenda vizuri tu, je kuna ukweli ktk kauli hiyo?na kama kweli tufanyeje ili tujikomboe? Nawasilisha.
   
 2. C

  CITYBOY Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee hii nikweli ndo maana ufisadi unamiziz mirefu na kuing'oa kwa kuichimba yote.Ufisadi ni ubinafsi na uroho.Tunaingia mikataba ya hovyo baada ya kuhongwa na hili wenzetu hili wanalijua ndo maana wanachota mali afrika kiulaini.Mfano kwa ujinga tunapewa silaha tuuwane wao wafaidike kwa mali zetu kwa kubadilisha na vilivyo duni kama silaha kwa kuahidiwa misaada.Mfano Sudan kusini kuna mafuta pale wapo wafaransa,wamarekani na waislael ndio wanao wahonga waafrika silaha.Mfano Congo wabelgiji na wafarasa wapo kuwapa waasi silaha ili wao wachote madini kilaini tu.Tanzania nawaachia wadau waseme kwani yapo mengi. Siri nyingi zipo vitabuni na vitabu hatusomi badala yake 2napenda udaku, ngono, pombe na muziki.Hao ndo waafrika bwana.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,566
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Concisely, Kweli ndivyo tulivyo mkuu! kama unavyoiona rangi Nyeusi huwezi kubadilisha ndivyo waafrika Tulivyo, Hope Nyani Ngabu can preach in wider view

  I once was thinking deeply about the behaviour of so called leaders, I turned my eyes widely to see how Citizens behave.

  Go to mlimani city, beaches, pubs, weddings, and any occasions, you will notice we are faking life! for some is real but for majority is fake! fake life, fake products, fake contracts, fake driving, everything is corrupt and not in order. The bottom line is that we dont think globally we think locally and locally here to be precise is our heart! our affairs.

  We need to change individually though, but truly, leaders reflect society, the society is criminal, we are living in a criminalised society where, messengers and minister both think to steal public money and to seize every opportunity that they may turn their lives positively!

  We need amazing leaders who know our inner behaviours! the leader who are wise to tune us to better side inspite of our natural lame!

  The issues of ujinga, ubinafsi na uchoyo is worse in Tanzania simply because we have had no and generation that they sacrificed for future generations. We are living in fake peace and preaching fake doctrines, we re not ready for fighting against ufisadi that alone manifesting our selfishness behaviour. Believe me history will condemn all of us not just JK and Rostam!! thats why what happened in Arusha have greater impact towards revolutions, Tukipigana tabia zetu za asili zitaondoka, we have seen this in Rwanda and Burundi, everyone now thinks of his nation..

  Some say they are done with Tanzanians, some say lets keep on pressing. However, have you ever imagined that Rostam, Lowassa, Chenge etc they have been selected legally by our fellow Tanzanians in their respective majimbos! that also explains more about our habit!

  You want me to go on!!!

  What do you think, seeing someone having 1 Tsh.Million cellular phone handset while his/her own young brother do not have Tsh 20, 000 for school?? or having mobile phone such expensive while your parents in village suffering by sleeping in mud house roofed with glasses and they need only 200,000 to buy iron sheets!

  How do you feel when you buy artificial South African Orange worth of Tsh 1000 while we have natural yet sweet oranges worth Tsh. 300!!!!

  If you think deeply my dear, we have a problem in our homes, in our communities in churches and mosques, in... name it!!!!

  Change should start Individually!

  If a nation swims in those three harmful behaviour then NATIONALISM is just a day dream, pretended or preached deceptively!
   
 4. T

  The Future. Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu zangu asanteni sana kwa michango yenye maana sana hasa ktk kipindi hiki, hata mimi binafsi naamini ni bora kuyajua mapungufu yetu tulio nayo ili tukabiliane nayo. Kwa mfano wajapani wana utamaduni wa kuheshim sana upanga na kioo, upanga ni kama kitambulisho cha ulinzi wa nchi yao,na kioo hutumika kama njia pekee ya kujitazama na kuona mapungufu ulio nayo then ukabiliane nayo. Ndugu zangu wazungu wametusoma sana na kutujua sana hata zaidi ya tunavyo jijua wenyewe, naamini kuna kila sababu ya kupambana na ujinga,ubinafsi na uchoyo wa asili tulionao, na kama tukishindwa basi waafrika wachache wataendele kushirikiana na wazungu kutunyonya na kutumia rasili mali zetu.
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  The future,

  Baada ya kusoma hayo makala, wewe mwenyewe ulijifanyia tathmini? Kama ndio uligundua kuwa makala imekuelezea wewe kama ulivyo? Yaani uligundua kuwa wewe husomi vitabu? pia ni mbinafsi , ni mchoyo na mjinga?

  Au kipi ulikubaliana nacho na kipi unaona makala hiyo imeongeza chumvi? Na kwa nini?

  Naomba utujulishe mawazo yako binafsi, halafu nitakuwa na aina ya kajimchango kadogo juu ya mada yako.
   
 6. T

  The Future. Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu nonda,nashkuru kwa swali lako, ni kweli nimejichunguza na kuwachunguza weusi wenzangu wa nchi na mabara tofauti. Mi binafsi nasoma vitabu lakini wengi hawasomi, kuhusu ubinafsi hua najiuliza mara kadhaa natamani kufanya starehe na vitu vya anasa lakini nimekua najishauri kuachana na mambo hayo kwa sababu asili yetu, ndugu yangu nonda we tazama p did mwaka jana katumia milion 2 usd kwenye shereh ya kuzaliwa kwake. Mi nimejipima na nime gundua hayo matatizo tunayo, na ni wajibu wetu kukubali ukweli na kujirekebisha. Au bado unajisoma bwana nonda.
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Umejibu kidogo sana. Rudia post yangu ya mwanzo. na jaribu tena kujibu. Hii mada yako ni nzuri sana. na tutapata wachangiaji wengi. Lakini toa tathmini ya ukweli juu yako.
  halafu jee katika hayo uliyoyataja kama mapungufu ya weusi katika hayo mabara yenye watu weupe mambo hayo hayako?

  Soma historia ya miaka ya nyuma pia. Afrika kama nchi huru ni historia mpya ina kama miaka 50-60. Jee hali ilikuwa tofauti kwa hao wengine miaka hiyo ?
   
 8. czar

  czar JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani si kweli kuwa weusi ndo wako hivyo tu hapana. Hata wazungu wapo hivyo hivyo sema wenzetu wamepiga hatua katika kuelimisha jamii zao. Ukiwa na jamii iliyoelimika itadai serikali inayowajibika ambayo italeta ufanisi. Sasa kwetu jamii kubwa haikuelimika na viongozi wetu wanatumia ubovu huo kutumaliza, pili kwa kuwa jamii haijaelimika inakuwa ngumu kudai serikali inayowajibika. Unadhani hata Ulaya na Marekani wangekuwa na katiba legelege kama zetu wangeendelea hivyo?
   
 9. T

  The Future. Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante mr nonda, lengo langu kutoa mada hii nikutaka kupata mawazo tofauti kutoka kwa great thinkers mbalimbali sidhani kama kuna haja ya ku comfece mmoja mmoja, ila la muhim tuizame jamii ya watu weusi wote duniani then tulinganishe na maneno ya wazungu hao kama yana ukweli. Kuhusu historia ya nyuma labda tuanzie karne ya 15.dr water rodney in his book of how europe under developed africa said,b4 the 15th century we were almost the same bt after the early contacts btn them and us the widen gape began,tujiulize kwanini baada ya kuanza biashara na sisi wao waliendelea?wengi watasema trans antlantic slave trade ndio sababu,tujiulize kipindi hicho kulikua na tawala zenye nguvu kama ghana,mali,songhai any kanen born empire na kwani viongozi kama akina tunka manen na alhaj mansa kankan mussa walishirikiana na wazungu kuwakamata watu na kuwafanya slaves?hapo hatuoni kama kulikua na ujinga pamoja na ubinafsi wa hali ya juu?kwanini hatuwezi kuungana kama EU, USA badala tunatengana, tanganyika na zbr,sudan(north and south) na nigeria?(muslims and christians).uchoyo ujinga na ubinafsi. Mi nafikiri upo kwenye dam yetu au nyie mnaonaje?
   
 10. N

  Nonda JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  haya mambo yako katika kila race na kila bara.
  kama nilivyoeleza mwanzo Afrika ina historia ya karibuni katika kujitawala ,wala si kujitawala hasa. wazungu walishajenga vitu viwili. systems za kuendelea kuwatumikia wao hata kama wameshaondoka. na walishatujenga kisaikolojia kujioni sisi ni inferior. kazi hiyo ilichukua miaka mingi.

  Pia wale wachache waliowapa hatamu ndio ma-agent wao. wa kuendeleza hiyo mifumo.
  ubinafsi uko marekani-unajuwa bail outs walizozifanya karibuni. huko ulaya pia, ubinafsi wa wachache umepelekea nchi ya Iceland chupuchupu ku-collapse. Ugiriki na Ireland umesikia zilivyoyumba.

  Ni world bank na IMF inaziamrisha nchi zetu zilipishe watu wake katika kupata elimu,iondoe subsidies kwa wakulima wetu,wakati wao wanawapa watu wao.

  kwa hiyo mkuu, hapa tunazungumzia viwango tofauti vya ulinganisho, kama afrika vimezidi,au kwa weusi hayo mambo yako kwenye damu ni kwa sababu zimetiwa kwenye damu.

  mada hii ni pana sana mkuu, nawewe unaonekana unaandika kutoka mobile, kwa hiyo ladha ya mjadala inapungua kidogo.

  kuna watu Afrika walikuwa na vision ya kuiendeleza afrika, Nkurumah, lumumba, nyerere...mambo ya ubepari na ukommunisti ulitibua sana mipango yao.

  sikatai kuwa wapo wajinga,waroho, wabinafsi lakini sio kwa weusi tu.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,270
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  Yes
   
 12. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  The future,

  thanks for bringing this subject.

  Its beyond reasonable doubt that we africans are that way. NI kweli kabisa kwamba sisi ni Wachoyo, Wavivu, Waongo, hatujuamini, tunaependa kusifiwa na daima huwa tunapenda short cuts. Hili halina ubishi na ukitaka kujua jaribu kuchunguza kwa waafrika wenzako haswa wa kutoka africa utagundua hilo.

  Nilipata bahati ya kukaa na wazungu kwa kipindi kirefu sana kama 10 years. Baadae nilipokuja kuishi na waafrica wenzagu niligundua tofauti kubwa sana. Daima lazima muafrika aseme uongo, hata kama kitu ni cha ukweli, but ataweka maneno mawili matatu ya kudanganya.

  Pia huwa tunapenda sana shortcut na uvivu, hatutaki kufanya kazi tukifikiri kwamba maendeleo yatakuja kutoka mbinguni. Ukitaka kuamini angalia vijana wanaotoka nje ya nchi ambao walikimbilia huko Ulaya kuishi halafu maisha ya kawa magumu, wanaporudi huwa wanakua na ujasiri na uwezo wa kufanya kazi sana haswa ukizingatia kwamba ule uvivu huwa unapungua au unaisha.

  Pia tuna element ya uchoyo, ubinafsi na kupenda kutukuzwa na kusifiwa. Hii inatokea sana haswa kwa viongozi wetu ambao daima wanapenda kusifiwa na kutukuzwa, haikosi ndio maana wengine kama Rais wa kenya anaitwa Mtukufu Rais (huo utukufu aemutoa wapi sijui)

  Kama alivyosema Waberoya hapo juu, suala hili kulibadilisha ni vigumu sana, inabidi kiongozi mmoja mmoja waone tatizo lilipo na kuanza kubadilika...! Jamii inabadilika kadiri viongozi wanavyobadlika. Kikwete akibadilika na kutembelea gari la bei nafuu, itakua ni vigumu kwa waziri wake kutembelea gari la gharama, itakua ni aibu, lakini swali ni nani anaweza kuanza kumrekebisha mwenzie? Mwananchi au kiongozi?
   
 13. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo kweli. Ingawa wana tabia ya kutokukubali matokeo wakishindwa kwenye uchaguzi
   
 14. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  :behindsofa: hilo halina ubishi
   
 15. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Si kweli tabia inatengenezwa na malezi, utamaduni, mazingira na survival skills end results ndio tabia. Kuna sababu nyingi sana ukitaka kuelewa zaidi google "G.H Mead, and his theory of The social behaviourism of role play". According to him we are all actors and the roles are dictated by the social, one reason for us not to elect another Kikwete ukiweka hali ngumu kimaisha inazua tabia za ajabu kwenye jamii.
   
 16. n

  niweze JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli Tuna Matatizo na Mifano Ndio Hii Wakina JK Wanaendeleza Kujenga Historia ya Watu Weusi. Angalia Huko Zimbabwe, Ivory Coast na Sehemu Nyingi Africa na Duniani Kote Tulipo. It's Real Sad. Maajabu ya Watu Weusi ni Kwamba Mungu Anatupenda Sana na Tunaweza Kupitia Haya Matatizo Yote na Tuka Toka Wazima. Tukiangalia Mahali Tulipo na Maisha Hasa Tanzani Bado Tuna Nafasi ya Kubadilisha Hali ya Inchi. Kitu Kimoja Kinatupa Shida ni Uongozi na Matatizo Mengi Tunaona Yanaanzia Ofisi ya Raisi. Kama Tanzania Tukibarikiwa Kiongozi Anaependa Taifa Lake na Kujua Nini Anataka Kufanya kwa Wananchi Wake, Tutanza Safari ya Mafanikio. Matatizo ya Ubinafsi na Uroho Yote Haya Lazima Tuendelee Kuelimishana Hasa Huku Kwenye Jamii Forum na Kama Wengine Wanakuwa Offended Thats Ok but We are Doing Our Job. Nchi Zetu Bado Zipo Kwenye Hatua ya Nation Building Kwani Hakuna Steps Zozote Tumefanya Kusimamisha Nguzo za Nchi. Tukichunguza Miaka Yote 49 Tangu Tuseme Tuna Uhuru, Hakuna Uhuru Wowote Tulikuwa Nao Wakati "Nchi Ilikuwa Haina Constitution ya Watanzania" Binafsi Naona Hatua za Kurekebisha Mabaya Yote Yaliotokea Kupitia Hiki Chama cha CCM It's Coming to the End. "Tuendelee Kushirikiana Kujenga Taifa Letu"
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Magazeti yamejaa mitaani watu wananunua kwa ajili ya kufungia maandazi kwenye migahawa badala ya kusoma. Mitandao kibao tunayo ambamo tunapata maarifa mengi bila gharama, lakini mswahili hana habari ila habari za pwagu na pwaguzi za kijiweni.
  Sherehe wabongo mtingo mmoja na ufahari wake huwezi amini ukilinganisha na kipato chake. Biashara kubwa mijini ni nyumba za kulala wageni ambazo zinaashiria zaidi nini kinaendelea ndani ya nyumba hizo.
  Baa za pombe kila kona badala ya kushindana uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vya kusindika vyakuna na utengenezaji wa zana mbalimbali.
  Viongozi kila kukicha safari mataifa ya nje kupanga kwenye mahoteli ya bei mbaya hata matajiri wa ulaya wanayakwepa.
  Magari ya serikali kubadilisha mapya kila baada ya miaka miwili wakati mataifa makubwa limit ya matumizi ya magari ni mfumo wa matumizi ya km/mls.
  bado kuna mengi tu.
  Wengi wetu wanafikiria maisha binafsi si kwa kizazi kijacho au taifa nini linahitaji kwa maisha ya wananchi wake.
   
 18. T

  The Future. Member

  #18
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante sana ndugu mhafidhina umeniongezea mambo mengi ktk fikra zangu hasa la uongo wa asili tulionao, pia ndugu candid scope umenikumbusha mbali niliwahi soma kitabu cha mtanzania wa jina hilo kinaitwa honest to my country ali reveal mapungufu mengi ya CCM let me get back to the topic kwa ujumla wengi wamekubali tunahayo matatizo na tusipo angalia tutaendelea kupotea zaidi, je tufanyeje? Nadhani vita kuu tulionayo ni kupambana na hizi tambia mbaya za asili ambazo zinazaa viongozi mafisadi.
   
 19. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  yes, miafirika ndivyo ilivyo! ni michoyo, haitaki kushirikiana kila katika kila kitu kazi imekalia tu umbea, ni mivivu ( we angalia mtu anaingia saa tutu ofisini ,saa nn4 anatoka kupata breakfast, saa 6 au saa saba anakwenda lunch wakati huo huo saa 9 tu ana maliza kazi na kurudi nyumbani, je hapo amefanya kazi kwa masaa mangapi? na je unategemea hapo kutakuwa na maendeleo? ), ni mizembe na imejaa husuda sana tu...haya yapo sana tu wala sio siri ,kinachohitajika ni mabadiriko ..
   
 20. N

  Nonda JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Kama wengi humu tunakubali haya ya kuwa "miafrika ndivyo ilivyo" na hayo mambo ,tabia" zimo ndani ya damu yetu" basi tunalalamika nini?
  Mmoja ameshasema huezi kuzibadilisha.Sote tunaochangia hii mada ni "miafrika" au vipi? sasa itabidi tufanye blood transfusion, tuweke damu ya kizungu au kijapani,kichina ili haya matatizo yatuondokee.
  kuna msemo wa kuwa kiongozi ni kioo cha waliomchagua au anawaowangoza.
  nionavyo mimi ni kuwa dhana hewa ya amani na utulivu na heshima ya woga ndio vitu vinavyoturudisha nyuma.

  Hatujaribu kuwawajibisha viongozi wetu.

  kila mmoja anataka kulaumu tu.
  Rumania walimnyonga kiongozi wao. South Afrika, Mbeki alilazimishwa ajiuzulu kwa madudu aliyoyafanya na mahakama.
  Sisi tunakubali kuwa sisi ni wavivu,wajinga, wasema uongo, wafitini, wabinafsi, wachoyo, nk hatuna zuri hata moja, tena tunamtupia nani lawama? tuende tu hivyo hivyo kama tumeyakubali haya.
   
Loading...