Je, Ni kweli Watanzania wanahitaji Katiba mpya?

game over

JF-Expert Member
Jan 1, 2016
6,908
2,000
Zaidi ya 90% ya Watanzania ni Watu wa Kipato cha kati na Chini, ambao tunahitaji mambo yafuatayo,

1.Umeme na Maji Safi kwa Gharama nafuu

2. Elimu bora na kwa Gharama nafuu

3.Masoko ya Mazao kwa Wakulima na wafugaji ambao ndio majority ya Watanzania

4.Huduma Bora za Afya na kwa gharama nafuu

5. Miundombinu ya uhakika hasa ya Usafirishaji kana vile Reli na Barabara

Hizi hoja za Katiba ni kwa Manufaa ya Nani ikiwa Watanzania walio wengi hata Katiba ya iliyopo hawana nakala na hawajawahi isoma?
Ni kitu gani kinatakiwa kitangulie kwa maslahi mapana ya wananchi walio wengi?

Pasi ya shaka yoyote, hizi ni agenda za wanasiasa hasa inapofikia hatua wakaona uwezekano wa wao kutawala unakuwa mgumu, wanatumani kuwa Katiba ikibadilishwa au pengine kukawa na tume nyingine basi itakuwa ni rahisi kwao kutimiza kiu zao za kutawala.
It is a human nature to struggle for power.

Tusio wanasiasa na tusio na ushabiki na vyama vya siasa tuendelee kuzisaka pesa maadam zinapatikana, nchi hii imejaa fursa na rasilimali kede zinahitaji kuvunwa, Tusikubali kuingia kwenye mipango ya wanasiasa tena kama tulivyozungushwa mikono kwa Lowasa 2015.
Natumaini kama imetokea mwanasiasa anaitisha maandamano kwa sababu zisizo na maslahi kwetu basi ajikute yuko peke yake barabarani,
Tusikubali tena kupotezeana muda. Pengine ningetamani kuona maandamano ya wafanya kazi wakidai haki zao, au wananchi wanaopinga mwenendo fulani wa serikali, na wala isiwe kwa kuhamasishwa na wanasiasa.

Katiba mpya sio kipaumbele cha Watanzania kwa sasa.

Nawatakia Pasaka njema na Mungu awabariki,

#ChukuaTahadhariCOVID-19isReal#

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,960

Katiba nk muongozo bila muongozo Bora yote uliyoyataja hayawezi fikiwa,katiba mpya inaondoa Kinga ya kutoshtakiwa,Kinga ya kutoshtakiwa ndio chanzo cha umasikini wetu
 
superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
6,522
2,000
Mada muhimu Kama hii inakosa wachangiaji inamaana watanzania wamechagua udikteta kunyamazishwa mdomo utekaji kea wakosoaji nk ?
 
aliali72

Member
Mar 13, 2020
46
95
Ndio tunahitaji, viongozi wa Sasa wakojuu ya sheria ambapo hupelekea kufanya maamuzi mabaya yanayowagusa wananchi wakijua hawatawajibishwa. Ndo Mana awamu hi ataingia kada anafanya vitu vya ajabu alafu awamu inayofata anaingia kada mwengine wa chama kile kile kurekebisha kidogo na kuendelea kufanya madudu mengine kisha anaona amefanya kazi kubwa, athari haiwapati wao Bali ni wananchi, wao wakimaliza huenda kupumzika na marupurupu yao sis wananchi tunateseka!!!
#katiba mpya
#maslahi ya mwananchi na taifa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom