Je, ni kweli Wasafi Media washakubali kuwa kivuli cha EFM?

Benjyhud

New Member
Nov 17, 2017
1
1
Ulimwengu wa entertainment (burudani) unaenda kasi sana, vitu vinabadilika kila leo, level ya ushindani imekuwa kubwa pia, mbali na kushuhudia hamahama ya watangazaji kutoka Media House Moja kwenda Nyingine, na tulipofikia ilishakuwa jambo la kawaida sana.

Kwa wiki sasa nimekuwa nikifatilia WASAFI MEDIA hasa baada ya upepo wa kisulisuli kuwapa faida ya kuweza kumnyofoa mtangazaji nguli wa muda mrefu bwana Maulid Kitenge (CHUMVI) kutoka EFM, na wengine wawili.

Nimekuwa mfuatiliaji nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua, hawa mabwana, watawezaje kutupindulia meza za EFM na Clouds ambao soko hili la tasnia ya habari wamelitawala kwa sasa.

Nimeshtushwa na u-kasuku walioamua kuja nao baada ya kuamua kuanzisha vipindi rasmi, (kivipi?).

Ujio wa Maulid kitenge na wengine, lengo ni kuanzisha kipindi cha michezo ambacho niliamini kitakuja kuwa changamoto kwa vipindi vingine vya michezo hasa SPORTS HQ ya EFM.

Ukasuku unaanzia hapa kwenye Jina la kipindi kutoka SPORTS HQ ya EFM, Wasafi Media wamekuja na SPORTS ARENA jambo ambalo kuna wakati watangazaji wake hasa Maulid wamekuwa wakichanganya majina haya Hewani.

Mbali na Majina, mpangilio wa vipengere katika kipindi cha SPORTS ARENA (Vipengere) kinafanana na kile cha SPORTS HQ, wakati SPORTS HQ kuna neno la kwanza namba 1 mpaka namba 4. SPORTS ARENA wana kivumbi cha kwanza cha kabumbu au soka la nyumbani namba 1 mpaka 4.

Vipengere hivi vyote vinafanana maudhui yake wakizungumzia soka la ndani. Ni imani yangu walikuwa na uwezo wa kufanya jambo kuepusha jambo hapa kuepusha huu mfanano, au wanatuaminisha kuwa ubunifu wao ndipo ulipoishia, na wameukubali ukasuku.?

Mbali na hili, wasafi media wamekua wakiendesha matukio (matamasha) ya WASAFI FESTIVAL na wamezunguka mikoa kadha wa kadha Tanzania, na wametangaza tarehe ya Tamasha hilo Dar es salaam, ambayo ni tarehe (9th November 2019) nawapongeza kwa hatua hii, ila kinachonishangaza katika mabadiliko ya uendeshaji kwa Dar es salaam kwa mujibu wa ratiba yao.

Tumezoea wasafi media kuwa na tamasha la usiku ambalo limeegemea kwenye matumbuizo ya wasanii tu, lakini safari hii wamenyumbulisha na kuongeza matukio kuanzia asubuhi (hapo sasa🤔)

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa, Shughuli zitaanza na jogging asubuhi, itafuatiwa na utafutaji wa vipaji kuanzia saa 4 halafu kutakuwa na mpira wa miguu na kisha tumbuizo litafunga shughuli, shangazo hapa ni mfanano wa ratiba hii na ratiba ya tamasha maarufu la MZIKI MNENE linaloendelea hivi sasa katika viunga vya Dar es salaam, kwa maana hivi ndivo wanavofanya EFM na tumeshawazoea na ratiba yao tangu mwanzo walivyoanza na tamasha lao.

Swali kwa ndugu zetu wa wasafi, inamaana hawakuuona kabisa huu mfanano? au ndio wamekubali kuwa kivuli cha EFM. nasubiri kuona watakuja na jambo lipi tena la kutushangaza japo naamini safari ijayo watakuja tofauti kuhuisha ushindani kwenye huu ushindani kwenye ulimwengu huu wa burudani.

- ni mimi mlimwengi.
 
Kosa walilofanya EFM ni hawakusajili miliki ya hivyi vipindi kuanzia maneno na maudhui. Clouds utahama ila maudhui yatabaki kwao
 
ACHENI MBWEMBWE NYIE, KUNA KITU KIPYA CHINI YA JUA??! KAMA UNACHO AU UNA IDEA MPYA PELEKA MEDIA UDAKE AJIRA.
 
Wasafi ndio wanakataza wanamuziki wao kujenga makanisani?
 
Anzisha lako mkuu kama watu watakuja
Kutoka CLOUDS Wamekopi:

- Tamasha ( Mpaka Mpangilio Wa Kutembelea Wakuu Wa Mikoa, Mapolisi na Shule )

- Jingles ( Nyimbo Za Uhamasishaji Redioni )

Tofauti Majina Tu
 
Kwani msanii gani Tz hii tangu mziki wa DDC mlimani mpk hawa wasanii wa kizazi kipya aliyewahi kujenga kanisa?
Wasafi ndio wanakataza wanamuziki wao kujenga makanisani?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom