Mambo vipi wadau?
nimesikiliza hotuba ya mgombea wa c.c.m kiti cha uraisi huko kirumba mwanza leo.................katika hotuba yake amesema amejitahidi kutoa nafasi mbalimbali za maamuzi kwa wanawake wengi kuliko kiongozi yeyote aliyepita...akatoa mifano kama vile mahakimu,mawaziri,manaibu waziri,majaji,wakuu wa wilaya na mikoa.....................
akaongeza kwamba hawa wanafanya vizuri kuliko wanaume....kwani ni waaminifu na baadhi ya wanaume ni wadokozi...............akaongeza kwamba wanawake hawa ni kidogo na wanastahili kupewa nafasi zaidi kuongezwa idadi........................
wadau tuondoe ushabiki wa kisiasa...tijadili ili kujenga nchi yetu...je ni kweli wanawake waliopo kwenye uongozi kwa sasa wanaweza???
kwa zile wilaya ambazo viongozi wa ngazi za juu ni wanawake kwa asilimia kubwa vipi kuna mafanikio?
kwa zile wizara ambazo waziri,naibu waziri au katibu mkuu ni mwanamke je ni kweli wanatosha?
Faithful,
Unaweza kuweka hiyo heading vizuri please; tujue, 'kupewa' nini; favor, vyeo, madaraka, au?