Je ni kweli wanawake wa tanzania wapo tayari kupewa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni kweli wanawake wa tanzania wapo tayari kupewa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by faithful, Aug 22, 2010.

 1. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mambo vipi wadau?

  nimesikiliza hotuba ya mgombea wa c.c.m kiti cha uraisi huko kirumba mwanza leo.................katika hotuba yake amesema amejitahidi kutoa nafasi mbalimbali za maamuzi kwa wanawake wengi kuliko kiongozi yeyote aliyepita...akatoa mifano kama vile mahakimu,mawaziri,manaibu waziri,majaji,wakuu wa wilaya na mikoa.....................
  akaongeza kwamba hawa wanafanya vizuri kuliko wanaume....kwani ni waaminifu na baadhi ya wanaume ni wadokozi...............akaongeza kwamba wanawake hawa ni kidogo na wanastahili kupewa nafasi zaidi kuongezwa idadi........................

  wadau tuondoe ushabiki wa kisiasa...tijadili ili kujenga nchi yetu...je ni kweli wanawake waliopo kwenye uongozi kwa sasa wanaweza???

  kwa zile wilaya ambazo viongozi wa ngazi za juu ni wanawake kwa asilimia kubwa vipi kuna mafanikio?
  kwa zile wizara ambazo waziri,naibu waziri au katibu mkuu ni mwanamke je ni kweli wanatosha?
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Baadhi yao wanaweza ila kisiasa..... labda viti maalum!
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Aug 22, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Unaposema "wanaweza" kwa takwimu zipi?
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kama rais anawachagua wafanyakazi wanaotokea kuwa wanawake "on the merit" na wanaenda kufanya kazi vizuri, kuwa identify kama "wanawake" ni discrimination.

  Wafanyakazi wazuri ni wazuri tu, na wabaya ni wabaya tu, wawe wanawake au wanaume. Sasa atataka kuangalia nini zaidi, kati ya waislamu na wakristo nani wanafanya kazi vizuri zaidi? Kati ya Wakwere na Waha nani wanafanya kazi vizuri zaidi?

  Hivi ingekuwaje kama rais angesema "Nimeongeza idadi ya wamasai serikalini, wanafanya kazi vizuri tu, tena kushinda makabila mengine" ? Si watu wangemsema mkabila.

  Cheap populism and divisive politics.
   
 5. M

  Msharika JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hivi jamani mliopo nyumbani silaa ameanza kampeni?????? Huyo mzee wa data dhaifu alipokuwa anaongea hayo mambo mwanza akuanguka tena?
   
 6. D

  Dopas JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  :focus:Hiyo hoja ya JK ni dhaifu sana, na anaitoa bila kuitafakari, kwaajili ya kupata ushabiki zaidii wa kisiasa. Nadhani ni kwa mtindo huo anapata mvuto sana wa kina mama. Hoja ya mgombea mwenye uwezo wa kupima mambo ingekuwa watendaji wangapi aliwateua kwenye nafasi mbalimbali ili kuongeza tija kwa watanzania. Na akichaguliwa tena atakazia maeneo yapi ili kuondokana na hali duni ya mtanzania, bila kujali watendaji hao ni wa-ke, wa-me. Muhimu kwa maendeleo ya mtanzania sio m/ke au m/me.
   
 7. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Sofia Simba anachechemea, Meghji kashindwa mapema, Dc wa kasulu dada machangu kakamatwa kwa utoaji wa rushwa, mama Sitta kakamatwa akiwa katika mazingira ya kutoa rushwa, Mwantumu mahiza alitochosha sisi walimu kwa kuongea kitaarabu, Hawa Gasia anakiburi kama nini,

  Kuwasifia wanawake ni kutaka cheap popularity.

  In general hotuba yake ilikuwa ni hovyo vovyo
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Aug 22, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Natamani bongo tungekuwa na kitu kama factcheck.org maana hawa wanasiasa wanaweza wakaropoka tu bila kauli zao kuwa checked na mijitu ikaamini.

  Kuna sehemu humu nimeona kuna mtu kaandika kuwa Kikwete katengeneza ajira milioni moja na ushee. Really? Kwenye sekta gani? Unemplyoment rate wakati anaingia madarakani ukilinganisha na sasa ni kiasi gani? Au hata ku track unemployment rate hatufanyi?
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Ku track employment si mpaka uwe na a functioning Bureau of Statistics, hata western world mostly wanatoa data zao katika unemployment benefit claims, sasa sisi hatuna hii wala a functioning Bureau of Statistics, kwa hiyo ni open season.

  Hata wakijenga "machinga complex" yenye uwezo wa ku accommodate watu 3,000 watakwambia "wametengeneza ajira 3,000".

  Uchumi wetu mostly una revolve katika informal sector, sasa kupata tangible data kutoka informal sector ni kudanganyana tu.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kama anawapenda sana wanawake KWA NINI YEYE 'DR.MKWERE' asiwaachie magogoni basi ?? si wanaweza ? au? au anadhania umma wa watz ni akina Malaria Sugu tu?
   
 11. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kiranga naomba nitofautiane na wewe kwenye hili. Kwenye jamii nyingi duniani, wanawake wamekuwa/walikuwa wakinyimwa nafasi katika maamuzi na masomo. Mf jumuia ya SADC na nyinginezo kama hizo zilijiwekea nafasi ya wanawake katika maamuzi angalau zifikie asilimia 50% baada ya miaka kadhaa. Hii ni kiashiria kwamba kuna tatizo na lazima tulikubali ili tuweze kulitafutie ufumbuzi. Sasa km tatizo lipo na linatafutiwa ufumbuzi ni lazima baada ya muda fulani liweze kupimwa na kuzungumziwa utekelezaji wake. Kwahiyo suala la kuzungumzia nafasi za uwakilishi/uongozi kwa wanawake katu haiwezi kuwa ni gender discrimination. Km unakumbukumbu sawia, hivi karibuni vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa vinazungumzia pia idadi ya wanawake ambao ni ma CEO kwenye FTSE 100 na indices nyingine. Kwahiyo sidhani mtazamo wa descrimination ni sahihi katika hili.
   
 12. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio list yoote?
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Aug 22, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Ila hii ya kumwita "Dr" Kikwete ndio inanimaliza kabisa....ni "Dr" kwa misingi ipi? Hata kama huo u "Dr" ni wa kupewa, kafanya lipi (japo kwa kiduchu) linalostahili hiyo title?
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Tukifikiri tena kwenye suala la ajira, serikali - katika enzi hizi za mfumo huria, kuuza mashirika ya umma na kupunguza ukubwa wa serikali - haitengenezi ajira per se, inatengeneza mazingira ya makampuni ya sekta binafsi kutengeneza ajira kwa kuweka misingi mizuri itakayofanya uchumi utabirike (na zaidi ya hapo utabirike kwa mazuri) na siasa kuwa madhubuti, chini ya utawala wa sheria usiotetereka. Mazingira kama haya yatasababisha sekta binafsi kushamiri.

  Sasa na hii rushwa yote iliyopo, political machinations, sheria fyongo na zile nzuri zilizopo kuwa hazitekelezeki, kulindana etc, Kikwete hawezi kusema hata kwamba kaweka mazingira ya kuongeza\ajira, achilia mbali actually kuongeza\ajira.
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu inawezekana MS kakubwaga kwenye kura za maoni kila post hata iwe haihusiani unamtaja..anyway, mi nadhani JK kasema "wanaweza" nyinyi mnataka takwimu za "kwanini" ama "kwa vipi"wanaweza wakati nyinyi hamna hata hizo za kwanini hawawezi?
  Mnajuwa nyie wasomi wa vitabuni msioweza kuvumbua hata sindano mnatabu kidogo, ndiyo mliotufikisha hapa tulipo, nchi masikini mnatuletea takwimu za kwenye makaratasi tu wakati ukitazama kwa macho tu unakuta njaa kali bado.

  Mkuu anasema "wanaweza" mimi nakubalinana naye kuwa baadhi ya sekta wanawake wameweza sana tu, kama mahakama, nimewaona kwa macho yangu akina mama Mjasiri, Kimaro, Munuo etc wakifanya vizuri tu kuliko hata wanaume, wakuu wa mikoa na wilaya kama Hajjat Amina Said Mrisho, Christine Ishengoma, Betty Mkwasa wanaongoza vizuri tu kwa kadiri ya uwezo wao...kweli wanaweza wala haihitaji takwimu hiiiiizo kujuwa kuwa wanaweza, wakuu give the devil his due...tuweni wapinzani lakini penye ukweli tusemeni.
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wewe bana ustake ncheke..hivi una akili timamu kweli wewe?

  Rais wako kipenzi chako Dr.Mkwere anasema wanawake wanaweza na wanaume ati ni wadokozi, sasa huoni hiyo statement ni self-defeating?? yeye yupo kundi gani? Kwanini basi asianze yeye kuachia ngazi pale magogoni?

  Pili nimemtolea mfano Malaria Sugu, maana yeye ni kama buu , anakula chochote chenye lebo ya CCM bila kutafuna, pengine yupo kama wewe, ndio maana hamchekani.

  BTW, sijaongelea hata takwimu, vita yangu mimi ni ya kimantiki zaidi sio matukio wala kauli fyongo za Dr.Mkwere which u find faultless..I bet hujui wala huelewi post unayoijibu. Typical STUPIDITY by choice.

  Siezi hata kujadili hayo majina uliyoaweka, maana principally sikubaliani na kupeana vyeo kwene ofisi za umma kwa njia ya kuteuana. Mnateuana mpaka nafasi za ubunge, typical wabongo halafu mnaketi kitako kujadili kwanini hamuendelei.

  Pheeew
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kwani hao wanawake aliwapa cheo kwa kuwa ni wamezaliwa wanawake tu au kwa kuwa wanaweza?

  au anataka kutuambia aliwachagua lakini hakuwa na uhakika wa utendaji wao na wamem SUPRISE kuwa wanaweza!

  ingelikuwa mimi ni mmoja wa majaji waliochaguliwa kisha mkuu wa nchi akawa suprised kuwa naweza ningelijiskia ovyo sana.

  asirudie hii kitu!
   
 18. G

  GEOMO Senior Member

  #18
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Huyu anatafuta kuungwa mkono na jopo kubwa la wanawake kwa kuwaadaa tu alafu baada ya hapo utamsikia mkutano mwingine kawaponda wanaume, mkutano mwingine kawasifia vijana na wakati yeye ndo mbovu na ghala la uozo wote wa nchi hii. Ni jambo la bahati mbaya sana tukimwacha huyu bwana arudi madarakani maana hana jipya tena. Kama hao wanaume ni wadokozi ni kwa baraka zake kama sio kwa baraka zake amechukua hatua zipi kali za kisheria na kimamlaka dhidi yao? Zaidi zaidi ni kuwafuta jasho kwa lugha zinazotukebehi sisi watanzania. Mfano-"kapata ajali ya kisiasa" n.k yaani jitu limebainika ktk mpango wake wa wizi ww unasema ni ajali kama huo wizi haukuwa mpango wenu wote ww na yeye tusemeje?
   
 19. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika uchaguzi wa 2005 (sina takwimu) lakini inasemekana kwamba JK alipata kura nyingi kutoka kwa za akina mama na akina dada kwa sababu ya sura yake nzuri! Katika mikutano yake ya kampeni Dar na Mwanza ukichunguza utagundua kwamba idadi kubwa ya waliovalishwa "jezi" za CCM ni akina mama. Kwa hiyo si jambo baya kwa JK kulipa fadhila!
   
 20. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kimsingi hawana tofauti na wanaume! Kama ni mapungufu ni yaleyale tu ambayo mtanzania anaweza kuwa nayo bila kujali jinsia yake. Ni perception tu ndio tatizo kubwa la mfumo dume.
   
Loading...