Hawapendani pale mmoja anapokuwa na kitu na akaonyesha uwezo wake wakipesa basi tambua hapo anakuwa ametengeneza maadui wengi utakuta wanachukiana pasipo kuwepo na sababu.
Mwanaume alilala nje usiku kucha na alipoulizwa na mke wake akamwambia nililala kwa rafiki yangu, mama wa watu alipopiga simu kwa marafiki wa mumewe anaowajua wote wakakubali tena wa kumi akajibu akisema bado yuko hapa anajiandaa kuja nyumbani. Ukawa ugomvi na ukaisha.
Sasa ilipotokea mke akalala nje na akajitetea kwamba alilala kwa rafiki yake, mume naye akapiga simu kwa rafiki wa mkewe hakuna hata mmoja aliyekubali kati ya wote kumi aliojaribu kuwapigia.
Nakumbuka nilipokuwa form five, kulikuwa na wasichana wawili marafiki sana wakati tunaanza A-level, urafiki wao uliendelea mpaka muhula wa kwanza ulipoisha, muhula wa pili nakumbuka upepo wa urafiki wao ulibadilika sana tena sana, no mawasiliano wala nini ni kuchuniana tu, sasa kuna mmoja hadi tunamaliza six alikuwa tayari alibadilisha marafiki wanne tofauti kwa vipindi tofauti na mwingine alibadilisha marafiki watatu kama sikosei. Hapo ndo niligundua kuhusu tabia za hawa viumbe juu ya urafiki!! Mweee!!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.