Je ni kweli wanasiasa duniani wanataka kutatua shida?

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Mara Nyingi Kuna dhana fulani kuwa Viongozi wa Siasa wa sehemu mbalimbali jukumu lao la kuwa Viongozi ni Kutatua Matatizo ya watu wao na Kuwarahisishia Maisha. Lakini Kwa Falsafa Yangu Nimegundua Kuwa Dhana hii sio kweli, Dhana hii Tuanaifikiria sisi Watu.

Wale hasa wale Wanaonufaika Katika Dunia hii, au hata Wakuu wa Uchumi hawawazi hivyo. Nitatoa Mifano Michache.
1) Hivi Leo Akitokea Dactari Bingwa akasema, salaale Nimegundua kwa Kibahati tu Vaccine ambayo, Ukimdunga Mtu hatakaa aumwe ugojwa wowote mpaka kufa kwake, labda tu afe kwa ajali.
Huyu Dactari Kesho yake tu hawatamwacha alione Jua, Hata "Pope" (Nimetoa tu mfano kwa Kizingatia Hospitali bora asilimia kubwa Duniani Ni za Roman Catholic, Lakini siseme Pope ni mbaya) mwenyewe akiulizwa tumfanyeje atasema mfuniengieni katika box la shaba na mulitumbukize Mariana trench! Kwanini wafikie Uamuzi huo?

Je Unajua Kuna hospitali Ngapi Duniani zitafugwa kwa sababu ya "Wazimu wa doctor huyo" Je Unajua Ni Viwanda Vingapi vya madawa Vitafugwa, Je Unajua ni Madactori wangapi na Manesi watakosa kazi? Je unajua ni Mashirika mangapi ya Bima za Afya yatakufa?

Mfano Mwingine, Akitokea Mwanafalsafa Mmoja akasema Nimepata Protocol moja Nzuri ambayo tukiiweka inplace, dunia yote itakuwa amani, hakutakuja kuwepo tena Vita. Unafikiri atapigiwa Makofi? No, Atapelekwa Mbele ya ufukwe wa Bahari na Kupigwa Risasi kwa hukumu ya Kijeshi kwa "Wazimu" Huo, Je Unafahamu Mzinga Mmoja wa Cruiser in Dolar Milioni 20 Na makampuni mengine wanalipa watu ili waende wakashawishi serikali zao zianzishe Tafrani mahali ili wauze "bidhaa" Unafikiri Kampuni itatengeneza Mizinga ya Dolar milioni 20, Ndege za Milioni 200 Vifaru na kadhalika ili wavikalie miaka hamsini bila hakijanuka mahali, una wazimu!

Ningetoa Mifano Mingi Lakini Nisiwachoshe, Mimi Ndiyo Ninavyoiona Dunia Ukionacho na Kukisikia sicho!
 
hoja zako dhaifu subiri UKAWA wakamate nchi.ndio utajua wapinzani ni mwiba.


swissme
 
Hoja yangu Inahusianaje na Ukawa au CCM, Ni Dhana ya Jumla ya Siasa Popote Duniani, Vipi my friend where are you coming up with this crap!
 
Back
Top Bottom