Je ni kweli wakenya walikuwa sahihi kuhusu Bunge letu?

mzaawa

Member
Dec 16, 2013
7
0
Kwa siku za karibuni mtakumbuka kuwa vyombo vya habari vya Kenya viliwahi kudhihaki mwenendo wa bunge letu la jamhuri ya muungano wa Tanzania.Baadhi ya watu walilaumu kitendo hicho na wengine kuunga mkono.Kwa hali inayoendelea sasa bungeni mpaka mijadala nani anatembea na nani.Je majirani zetu walikuwa sahihi kutudhihaki? na kama spika ataruhusu mijadala ya namna hiyo,ni nani atakaye baki salama ikiwemo spika ambaye inasemekana hana mume na pia naibu spika ambae hajui idadi ya watoto alionao.Je haya ndio tuliyo watuma sisi wananchi kujadili bungeni?
 
...ni nani atakaye baki salama ikiwemo spika ambaye inasemekana hana mume na pia naibu spika ambae hajui idadi ya watoto alionao.Je haya ndio tuliyo watuma sisi wananchi kujadili bungeni?
Mkuu, mbona na wewe unawajadili pia?
 
Kwa siku za karibuni mtakumbuka kuwa vyombo vya habari vya Kenya viliwahi kudhihaki mwenendo wa bunge letu la jamhuri ya muungano wa Tanzania.Baadhi ya watu walilaumu kitendo hicho na wengine kuunga mkono.Kwa hali inayoendelea sasa bungeni mpaka mijadala nani anatembea na nani.Je majirani zetu walikuwa sahihi kutudhihaki? na kama spika ataruhusu mijadala ya namna hiyo,ni nani atakaye baki salama ikiwemo spika ambaye inasemekana hana mume na pia naibu spika ambae hajui idadi ya watoto alionao.Je haya ndio tuliyo watuma sisi wananchi kujadili bungeni?

Ni mwanahabari mmoja tu Gado ambaye ni mtanzania aliyechora cartoons depicting the Tanzanian parliament... just wanted to correct that
 
walikwa sahihi pasiposhaka mkuu si unaona maneno na vituko vinavyofanyika Bungeni tena vinafanywa na watu wanaotakiwa kukemea wenzao wanapopotoka.
 
Bunge letu limepungua heshima sana kutokana na udhaifu wa maspika wetu--ndugai na bi kiroboto wameshindwa kuliongoza bunge. mbona enzi za mkwawa, msekwa na sitta walikuwa hawafanyi ujinga kama huu?
 
Shida ni nyingi sn ndani ya bunge! Na kubwa Zaidi ni Hawa wawakilishi na viongozi Wa serikali kutokujua wajibu! Usipoelewa wajibu wako kila kitu kitakwenda ndivyo sivyo!
 
Bunge limekua sehemu ya kuchafuana kisiasa na uitikadi Wa vyama!
 
Nyie ndugu zangu mkuu, lazima nifuatilie mambo kwa karibu.

Kuna mambo mengi nakusapoti, machache nakupinga.. So nikiwa nakupinga uwe mpole, dnt be up sometimes.. Kwa hili la kutetea bunge la Tanzania nakuunga mkono.. Ni kweli kuna mwandishi mmoja tu ndio alichafua taswira ya bunge la Tnz..
Big up bro!!
 
Back
Top Bottom