Je, ni kweli uwepo wa Tume Huru ya uchaguzi ndiyo suluhisho/ mwarobaini wa migogoro ya kisiasa?

KITAULO

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
1,926
2,777
Wana JF,

Kwa miaka mingi vyama vya siasa vimekuwa vikilalamika juu ya kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi. Kwa maoni yangu nadhani sasa ndio muda muafaka wa wananchi kukaa chini na kuelimishana ni kwa namna gani tuta pata tume huru na tutajiridhisha kuwa Tume inayosimamia uchaguzi hakika ni huru pasipo kutia shaka.Na kunamsawali kadha wa kadha ya kujiuliza tunapokuwa tunajiridhisha kama ifuatavyo;
  • Tume huru huwa inaundwa vipi?
  • Viongozi wa Tume wanatakiwa kupatikana vipi?
  • Ni mamlaka gani kisheria inanguvu ya kuregulate mchakato mzima wa tume?
  • Je katiba yetu tuliyonayo inatupa mwanya wa kuunda tume huru?
  • Je na kama ikiundwa kutakuwa hamna mgongano wa kimaslayi/conflict of interest?
  • Je itakuwa huru kweli katika Nyanja zote?
Hayo ni maoni yangu wana jamvi najua humu kunawabozi wa sharia na mambo ya kisiasa …tujuzane ili hata kama tutakosa tume huru walau tupate picha tumekosa kitu gani na nani wa kumlaumu kwa hilo!!
 
Tume huru ya uchaguzi
Ili iwe huru lazima iundwe na vyama vyote vya upinzani kwa pamoja mwenyekiti wa tumekosa huru achaguliwe kutoka kwenye umoja huo wa vyama wanapendekeza jina linapigiwa kura au apigiwe kura na wananchi wote kama alivyo Rais yaani a naomba kura

mwanabhonga
 
Tume huru ya uchaguzi
Ili iwe huru lazima iundwe na vyama vyote vya upinzani kwa pamoja mwenyekiti wa tumekosa huru achaguliwe kutoka kwenye umoja huo wa vyama wanapendekeza jina linapigiwa kura au apigiwe kura na wananchi wote kama alivyo Rais yaani a naomba kura

mwanabhonga

kwa Tanzania mbona kama hiyo ni ndoto za mchana..huo mchakato utakuwa mgumu mnooo
 
Kupata Tume huru na ikawa huru kwenye mazingira ya sasa ni kazi ngumu.
Uchaguzi uliopita Zanzibar walikuwa na Tume huru iliyoundwa na vyama vyote vya siasa, lakini mwisho wa yote matokeo ya uchaguzi huo yalichezewa.
 
Back
Top Bottom