Je ni kweli ukiajiriwa uwezekano wa kuwa tajiri ni mdogo sana au haiwezekani kabisa?

Saveya

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
2,309
2,246
Habari za asubuhi wanabodi,
Kumekuwa na mitazamo/ dhana maeneo mengi sana duniani kwamba ili uwe tajiri ni lazima uwe nje ya mfumo huu wa kuajiriwa bali unatakiwa ujiajiri, na wanasema kwamba
'hautakuwa tajiri ' kabisa. Je, kuna mfano wa waajiriwa ni matajiri? Kama wapo tuwataje

Karibuni kwenye mjadala.
 
hapa Tanzania kuna ajira zinawapa watu mshahara milion 10 , 20 hata 30 kwa mwezi nyingi tu..
 
Kwanza inabidi ufafanue unaposema utajiri unamaanisha nini mkuu.

Kuna watu akiweza kumiliki 1 M ni tajiri.
Mwingine akiweza kuwa na usafiri, ni tajiri. Mwingine akiweza kuwa na kwake ni utajiri. Hali kadhalika anaepeleka watoto shule za school bus ni tajiri. Lakini mwingine anavyo vyote hivyo na bado haoni ni tajiri.

Kwa ufupi, utajiri una tafsiri nyingi lakini kwa kiwango cha chini kabisa ni ile hali ya kutokusumbuliwa na mambo madogomadogo na kuwa na uhakika wa vyanzo vya mapato vibavyokuingizia pesa.
Hapa namaanisha mambo ya matibabu (afya), elimu, malazi, usafiri, chakula, kusaidia wale wa karibu sio vitu vinakuumiza kichwa tena. Hapo wewe unasimamia na kuanzisha njia nyingine za kuendelea kukuingizia pesa bila kukumaliza sana wewe kiafya.

Hapo litafuata kuwa na umiliki wa ukwasi kiasi gani ndio itaamua uwe kwenye kundi lipi la matajiri, hawalingani viwango.

Unapokua umeajiriwa, unabanwa muda wako mwingi kuutumia kwa mwajiri na unaridhika na kile kipato unachopewa mwisho wa mwezi.

Akili ya kukiwekeza au kukitumia hicho mnacholipwa ndio inaleta tofauti kati ya mwajiriwa mmoja na mwingine. Kuna watu wanalipwa 1M, 5M, 10 M hadi 30M sasa ukisema kuajiriwa hauwezi kuwa tajiri, inakua ni sentensi ya ujumla sana.

Ugumu unakuja hapa, ili jambo lolote lifanikiwe vizuri na lilete ufanisi, lazima ulipe muda wako wa kutosha kwenye usimamizi, hauwezi kuwa na huo muda ukiwa kwenye ajira. Lazima uchague moja. Vinginevyo hautapata manufaa chanya ya shuguli yako nje ya ajira.
 
Back
Top Bottom