Je, ni kweli udhamini GSM ni wa kimkakati?

Acha kukalili mambo, kwa taarifa yako ni kuwa hakuna kanuni inayozungumzia juu ya mdhamini mwenza nembo yake itakaa/haitakaa kwenye jezi ya timu, bali ni hao tff wanapomfuata huyo mdhamini kumuomba udhamini , na yeye ndiye anatoa masharti yake, mkiyakubali sawa anatoa pesa!!na tff ndio walimfuata GSM, na yeye akatoa masharti hayo.sasa kama hao wadhamini wenza wa nyuma hawakutoa sharti hilo ni wao!!kanuni zipi hizo ambazo zimekuwepo kwa miaka mingi?mbona hadi sasa timu hazifahamu hyo mdhamini mkuu washindi watapata kiasi gani?TFF, ndiye mwenye ligi na mikataba yote ya wadhamini ni yeye ndiye anaiingia, hata CAF, ni hivyo hivyo, nyie timu mtapewa tu utaratibu wa kuufuata basi, kuna timu hapa hapa ina udhamini wa ttcl na logo yake iko bega la kushoto , sasa watakapokuja kuambiwa waitoe/kuihamisha utasikia kelele tena!!wakati kanuni ziko wazi kuwa hata ukipata mdhamini wako huko lazima uijurishe tff kwanza!!Tatizo la kwetu u yanga na simba ndio kikwazo.
Ila ki kanuni ktk hili simba hoja zake hazina mashiko.mfano eti yanga hajatwaa kombe miaka 4, hivyo kuna kitu kinaandaliwa!!!si upuuzi huo, GSM, ndio atacheza?
Sawa mkuu nimeacha kukalili, me ngoja niwapishe muendelee na hii topic nimechangia vya kutosha acha nikabidhi kijiti nitarudi badae kusoma michango yenu
 
Screenshot_20211208-105432.png
 
Ndio maana mpaka sasa refa wa namungo na yanga hawajamjadili hii yote ni rushwa wanayopewa na gsm huku akijificha kwa kivuli cha udhamini
Hivi Morrison alupompiga kiwiko mchezaji wa GG alipewa adhabu gani mikunbushe wenye kumbukumbu zenu.
 
Hili la udhamini wa GSM sio tu litavuruga ligi lakini pia linatachafua amani ya nchi na kupelekea kumwagika kwa damu.

✍🏽
 
Azam Tv sio wadhamini wa ligi, isipokuwa wana haki za matangazo ya television ya ligi.

Kingine Azam haipo kwenye jezi ya timu, tofauti na timu anazozizamini.

Mkataba wa Gsm na TFF una makandokando mengi ya kikanuni. Kwanza kanuni hakuna sehemu zinaposema mdhamini mwenza anakaa kwenye jezi, isipokuwa mdhamini mkuu. Sasa kwa nini TFF walazimishe gsm akae kwenye jezi wakati ni mdhamini mwenza?

gsm ni kit supplier wa Yanga lakini baadhi ya timu zina kit supplier wengine ambao kiuhalisia ni washindani wa kibiashara wa gsm. Mfano Simba na polisi Tanzania wana vunjabei. Kuwaweka gsm na vunjabei kwenye jezi moja ambao ni washindani kibiashara hauoni ni mgongano wa kimaslahi?

Sikuwahi kudhania kama TFF na gsm ni mbumbumbu kiasi hiki.
Umeongea jambo la maana sana na Mimi naomba nikukumbushe kitu. Umeongelea suala la nembo ya Azam kwenye timu anazodhamini, ni sahihi. GSM walipoweka nembo kwenye jezi za Namungo likaibuka zengwe toka timu moja ikiongelea "fair competition ". Sasa GSM wameona waweke nembo kwenye timu zote ili kubalance fair competition napo mnalalamika. Halafu huu mpira wenu ambao kila siku walalamikaji ni Simba au Yanga unawasaidia nini? Mbona hatumsikii Azam au Mtibwa au wao hawana haki? Karia amerudi kwenye uongozi kwa mgongo wa Simba tena mkiwa mnakomaa kweli kweli kwamba Karia ameleta maendeleo ya Soka kwa kuisaidia Simba kufika robo fainali CAF. Miongoni mwa ahadi zake wakati wa uchaguzi ambao alifanikiwa kuwaengua wagombea wengine kwa kutokuwa na sifa (CCM style) ilikuwa ni kuoata wadhamini ili ligi iwe na fedha za kutosha vilabu kujiendesha msimu mzima bila taabu. Kapata mdhamini katoa bil.2 timu moja inakuja kupinga. Leo Karia mliyepigania ashinde uchaguzi siyo msaada kwenu tena ni adui. Hivi nini role ya mdhamini wa ligi labda? Kuna mahali mdhamini ana influence mshindi wa mechi yoyote? Yaani tuseme NBC anaweza kuamuru mshindi kati ya Mtibwa na Biashara awe Mtibwa na ikawa?? Tunapopinga kitu tuweke na vielelezo basi.! Tunapenda tujue athari ya udhamini wa GSM kwa timu zote si kwa timu moja tu. Hata hivyo niwashauri TFF hili halina haja ya kulipa uzito mkubwa wakati jambo lenyewe ni dogo tu. Hakuna haja ya kumlazimisha mtu kuweka nembo ya mdhamini wasiyemtambua, ila na wao hawapaswi kufaidika na chochote toka kwa mtu wasiyemtambua.
 
Uyo gharib mwenyewe elimu yake inatatanisha kapata pesa kiunyonyaji na uhujumu uchumi,amezungukwa na machawa na vishoia unafikili kuna kitu hapo
Ujinga ni kudhani kuwa umasikini wako unatokana na utajiri wa mtu mwingine. Elimu mbovu ya mtu yeyote kama si mwalimu wako au wa mtoto wako haiwezi kukuathiri labda awe daktari atakayekutibu. Mfanyabiashara akiwa na Elimu ya kuungaunga inakuathiri nini wewe mteja ambaye una option ya kwenda kununua kwingine?
 
Mbona Azam hamkulalamika, kama mnalalamika hapa inabidi malalamike na Azam sababu tofauti na hapo ni double standards za ajabu.

Iliyodhamini Ligi ni AZAM MEDIA.

AZAM MEDIA inamilikiwa na Mzee Said Salim Bakhressa

AZAM FC inamilikiwa na Mtoto wa Bakhressa

Hivyo Azam Media haina uhusiano wowote na Azam FC

Wala mmiliki wa AZAM MEDIA Mzee Said Salim Bakhressa hana uhusiano wowote na Azam FC

Mtoto kumiliki Timu haimaanishi kuwa Timu hiyo lazina na Baba itakuwa ya kwake.

NOTE: AZAM FC sio Timu ya Kampuni kama ilivyo Mancity au NewCastle kule Uengereza bali ni Timu ya Mtu Binafsi kama iliyo Chelsea au Hull City pale Uengereza.

Hivyo usitolee mifano isiyohusiana.
 
Upupu mtupu umeandika hapa,so Yanga timu ya GSM!?
 
Sawa mkuu nimeacha kukalili, me ngoja niwapishe muendelee na hii topic nimechangia vya kutosha acha nikabidhi kijiti nitarudi badae kusoma michango yenu
Hapana!!mkuu twende tu na sarakasi zetu, mpira wa nchi hii simba na yanga ndio sumu ya mpira.
 
Sawa mkuu nimeacha kukalili, me ngoja niwapishe muendelee na hii topic nimechangia vya kutosha acha nikabidhi kijiti nitarudi badae kusoma michango yenu
Mkuu nimeumia sana ulivyokua unatumia nguvu nyingi kumjibu mjingamimi

Huyo jamaa ni zaidi ya mpumbavu sio tu mjinga.
 
Unaweza kunipa sababu ya Simba kukataa kuvaa nembo ya GSM?

Tambua pia kuwa GSM ni mpinzani wa VUNJABEI katika suala zima la Uuzaji wa jezi na mavazi. Sasa itakuwaje kwa Simba na Polisi Tanzania kuvaa mpinzani wa VunjaBei hauoni kuwa wanakiuka masuala ya kimkataba?

Turudi kwenye uhalisia na sio mihemko. Ujue kuwa kutokana na sheria na kanuni za kimkataba Yanga washawahi kuhoji uhalali wa wachezaji wao kuvaa Tshirt za kampuni ya Kubeti bila kushirikishwa kipindi fulani. Kampuni hiyo ni moja ya wapinzani kibiashara na Sportpesa? Unafahamu?

Unaelewa kuwa hakuna club inaweza vaa nembo ya Bank mshindani wa NBC pale kifuani kwenye ligi yetu? Unafahamu.

Sasa kwa nini TFF wanataka kuwanyong'onyeza SIMBA SC & POLISI TANZANIA kibiashara na kwa nini hawakushirikishwa juu ya hili. Hata FIFA wanaelewa hili babu.
 
Huyo GSM kama ana hela nyingi akalishe hata wasiojiweza kuliko kutaka kuhonga kila mahali ili achukue kombe.
 
Tambua pia kuwa GSM ni mpinzani wa VUNJABEI katika suala zima la Uuzaji wa jezi na mavazi. Sasa itakuwaje kwa Simba na Polisi Tanzania kuvaa mpinzani wa VunjaBei hauoni kuwa wanakiuka masuala ya kimkataba?

Turudi kwenye uhalisia na sio mihemko. Ujue kuwa kutokana na sheria na kanuni za kimkataba Yanga washawahi kuhoji uhalali wa wachezaji wao kuvaa Tshirt za kampuni ya Kubeti bila kushirikishwa kipindi fulani. Kampuni hiyo ni moja ya wapinzani kibiashara na Sportpesa? Unafahamu?

Unaelewa kuwa hakuna club inaweza vaa nembo ya Bank mshindani wa NBC pale kifuani kwenye ligi yetu? Unafahamu.

Sasa kwa nini TFF wanataka kuwanyong'onyeza SIMBA SC & POLISI TANZANIA kibiashara na kwa nini hawakushirikishwa juu ya hili. Hata FIFA wanaelewa hili babu.
Labda tunashindwa kuelewa.
GSM amedhamini LIGI.
Sio JEZI.
sisi tunaoleta ushabiki ndio tunaona GSM ni chapa ya YANGA.
ILA GSM ni kampuni inayojitegemea.
Sijui mnaelewa hapo?
 
acha kunitisha.
sikulazimishi uamini maoni yangu.
Na wewe usinilazimishe kuamini maoni yako.
club zinafata muongozo wa TFF.
Sio Ushabiki maandazi wenu wa Simba na yanga.

Bodi ya Ligi na TFF nani anafaa kuongoza na kusimamia Ligi? Ni nani Mlezi na ni nani ni overall mlezi wa vilabu kati ya TPLB na TFF?
 
Utarudi hapa kwa aibu ,Simba havai nembo ya gsm na hakuna kitu atafanywa ,Ni Mambo mawil tu ama kalia apewe burn ya milele na FIFA au ligi yote ivurugike Sasa tuone mtapata wapi nguvu ya kubwata hapa jamvin ,maana hakuna yanga bila Simba au Simba bila yanga Hawa watu ili wawe walivyo lazima uwepo wao uwepo .

Tff Ni Malaya na Wana tamaa na Pesa lakin zinaenda kuwatokea puani ,Zama hizi sio za bla bla wasomi wamejaa kila Kona plus mitandao ndio Basi Tena kila kitu kipo wazi ,tuliendeshwa kindez Karne ya analogy Ila sio kwasasa ,uhuni mwisho kila kitu kitafuata kanuni na Sheria .

Kama ambavyo mligomea kuvaa nembo ya twiga mweupe na mkapenya bac mnaamin na hili mtapita.

Na lengo la gsm kuleta udhamin wa kihuni safar hii tunajua Ni kuzima aibu walizopata huko cas baina ya Morrison na kuwasahaurisha mandez wote wa uto Hilo Jambo ,na mlivyo vichwa panzi kweli mmejaa kwenye mbinu yao .
Hili povu kama si la MIMBA CHANGA sijui...
 
Back
Top Bottom