Je, ni kweli Uchaguzi wa Malawi umewatia woga viongozi wengine wa Afrika?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,793
71,206
Wapinzani hadi wananchi kwa jumla wa Malawi waliamua na wameweza kufanya kile ambacho kilikuwa kinaonekana hakiwezekani kwa nchi za kiafrika. Yaani kuiondoka kwa kura serikali na kiongozi aliyeko madarakani.

Kulitokea kitendo cha ajabu Malawi, Rais Mutharika alimuagiza Mkuu wa majeshi asaidie jeshi kuzuia watu maandamano lakini aligoma kushambulia RAIA alio apa kuwalinda akafukuzwa kazi. Maana yake mkuu huyo wa majeshi kwa sasa atakuwa na Heshima kubwa zaidi kwa Raia na Rais wa sasa.

Mkusanyiko huo wa matukio umesababisha viongozi wa nchi za kiafrika hususani za kusini mwa Sahara kutopokea habari za Rais mpya kwa bashasha kama kawaida yao.

Je, response ya Jeshi na RAIA imewatia woga watawala kuwa wananchi wakiamua kusimama kidete unaondoka madarakani? Au kitendo cha siku moja tuu madarakani kwa rais mpya na kumuondolea kinga Mutharika ndicho kimetia chumvi kidonda cha hofu?

IMG_20200703_111128.jpg
 
Malawi ni miongoni mwa nchi za Africa zilizopiga hatua ya kidemokrasia ukilinganisha na nchi nyingi za Africa, nchi ya malawi imewahi kufanya chaguzi zilizoviangusha vyama tawala vya nchi hizo tukianzia na anguko la Dr Kamuzu banda ambae aliangushwa katika uchaguzi wa mwaka 1994 na Bakili Muluzi.

Vile vile anguko jengine lilitokea kwa Rais Dr Joyce banda alishindwa uchaguzi akiwa madarakani na Rais alieshindwa kipindi hiki, kwa hiyo nchi ya malawi ina uzoefu mkubwa wa kubadilisha uongozi kwa njia ya kidemokrasia kulinganisha na nchi nyingi za Africa.

Jambo jengine nchi ya malawi ina katiba nzuri pamoja na taasisi imara za utoaji wa haki vitu ambavyo ni mihimili ya ukuaji wa demokrasia, hivyo kutokuwa na katiba nzuri, kutokuwa na mahkama huru na tume huru ya uchaguzi kamwe hakutaakisi ukuaji wa demokrasi. Matokeo ya malawi kamwe hayatawanyima usingizi nchi nyengine ambazo hazijaweka mihimili ya ukuaji wa demokrasia.
 
Sasa waogope nini wakati kama hapa Tanzania tume na polisi wote wanalamba viatu vya rais aliyeko madarakani.

Yaani hapa rais hata akiamua asifanye kampeni kabisa lkn bado anaweza akatangazwa ameshinda kwa asilimia 100 na ikawa imetoka tu hivyo.

Ktk nchi kama Tanzania hakuna haja ya uchaguzi ni kuharibu tu pesa na kupoteza muda kwani tayari rais ana matokeo yote nchi nzima na hata amekuwa na kiburi cha kuwaambia wapinzani kuwa hawawezi kurejea tena bungeni... sasa hii maana yake nini si ni kufanya watu wajinga kujifanya eti wanasubiri uchaguzi kumbe ni usanii mtupu.
 
Mwenge huo mwenge mbio mbio!!!! Km bado unawaka kileleni na mitaani. Ccm itabaki madarakani milele. nimeonaengi kwenye mwenge jamni heee!
 
Back
Top Bottom