Je ni kweli tunayataka mabadiliko yanayotokea tunisia, misri nk? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni kweli tunayataka mabadiliko yanayotokea tunisia, misri nk?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Derimto, Feb 1, 2011.

 1. D

  Derimto JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mgaya wa TUCTA ameandaa ya kwake na hataki wanasiasa waingilie anadai wasije kuingiza mambo ya siasa kupitia wao na maandamano yake yanashonewa sare kabisa wakati wanaoteseka ni wananchi wengi tuseme karibu wote swali kwani nchi inaongozwa na nani kama siyo wanasiasa ambao watu hujiunga nao kutokana na hoja na sera zao na siyo kundi fulani kama wengine wanavyotumia fimbo ya udini.

  Wanavyuo nao hawataki wanasiasa waingile mambo yao na wao wanataka kuandamana kivyuovyuo na kupigwa na kuuawa kama kule dodoma na mambo yanaishia chinichini' nini kwani chuo si cha kwao ccm mtawafanya nini mnasoma kwa msaada (nashindwa kuamini) nini maana ya utawala bora

  CUF nayo wanaandaa ya kwao kuanzia buguruni kama kawaida na nimemsikia Mtatiro amesema na yeye ana intelijensia yake na ana uhakika maandamano yatakuwa ya Amani na polisi wasilete intl.zao za kizushi maana ya kwake ni ya uhakika zaidi hivyo watafanya maandamano ya amani na kupinga mambo mengi yanayoendelea hapa nchini kama vile Dowans, katiba nk.
  Hii ni kama nimeitamani na imenivutia lakini hawa jamaa hawaaminiki kabisa inajulikana kama ccm b. Na wanatafuta kazi zaidi kama aliyopatiwa maalim Seif (samahani hivi Zanzibar kuna rais?) hana mvuto wa kisiasa amewekwa tu kama mkuu wa mkoa fulani.

  Viongozi wa dini na wao wameganyika kidini ambao viongozi wa dini ndiyo waliohakikishaga kuwa Yesu Kristo anasulubiwa hawa wengi ni wanafiki wakubwa sana na wavurugaji wa kwa kutumia nafasi zao maana watu wengi wanawaamini sana kuwa wanaweza kuwapatia maisha bora ya umilele lakini wanaingiza siasa kulingana na ushabiki wao na kutumiwa vibaya na wanasiasa huku maisha magumu yakiwaadhibu kila mtu bila kujali aina ya dini yake na chama chake maana hata hao VILAZA WANAOJIITA WANA CCM. Wamechakaa na maisha na huku wamevaa kofia na vilemba vya uchaguzi wa 2005 akidai hicho chama kinamfaa. Hapohapo waisilamu wameshaingia mtegoni wakiamini kwamba mabadiliko yanayotakiwa na CDM.ni ya kikristo zaidi na wanachukulia kuwa wakristo wanampinga kikwete waisilamu wao wanaamini maisha yao yako sawa na hawahitaji mabadiliko kulingana kauli8 zao nyingi wao wakishapewa mahakama ya kadhi ambayo ni kama wameshaipata tayari hawana jingine wanalotaka.

  Na kuna mwanaharakati mwenzetu humu jamvini yeye amerusha thread yake akiomba vijana, wanafunzi na watu wote wenye kutaka mabadiliko wakutane mnazi mmoja tarehe 2 walianzishe na wengi tumemuunga mkono na siyo vibaya.

  Nimesikia tena CDM. Wao wameandaa ya kwao Tarehe 28 na kila karibu watu wote hawa kilio chao ni kimoja lakini tatizo hatujajipanga kwa mtindo ambao utabadilisha sura ya kisiasa kama tunayoyaona Tunisia Misri na kwingineko ninachokiaona hapa zaidi ni ubinafsi zaidi na wachache wanaojitafutia umaarufu wa kisiasa.

  Kwa haya ya CDM. Nitakwenda hayajaonyesha kuwa ni ya kwao wenyewe bali ni ya watanzania wote hayana sare na hayajasema ni ya watu wa dini gani wala wao hawatafuti kazi kama maalim Seif na kundi lake maana Lipumba ameshatoswa ila pamoja na kuwa Prof. Hajastuka tu nina mashaka gorofani kwake hazimo au huenda na yeye anataka apewe ka uwaziri.

  Tuache mambo ya ushabiki hapa hebu tuangalie ukweli halisi kuwa ni chama gani cha upinzani Tanzania kwa wakati huu kina nguvu ya kuweza kuwakusanya wananchi kona zote za Tanzania na kinasikilizwa na aina nyingi ya jamii na kuungwa mkono then kwa pamoja twendeni kwenye maandamano kwa HOJA ZA KITAIFA NA SIYO KICHAMA NA KIDINI KI TUCTA NK.

  Na Polisi ambao wao ni kama maroboti wakae mbali maana hata wao wamechoka mbaya kama hawatasikia kuna Jeshi ambalo linajua mipaka ya kazi yake na yatawakuta yale ya Misri.

  Nitahudhuria maandamano yaliyoandaliwa na Chadema maana ndiyo sauti ya wengi na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu na ndiyo waliokurupua mambo mengi ya mabadiliko ya kisiasa hapa nchini.

  Tahadhari kwa wavivu wa kufikiri na kuniona kama mwanachama wa chadema watakuwa wamekosea hapa maana kila Mtanzania anayeishi kwenye dhahama hili anahitaji mabadiliko ya kweli na siyo malumbano akili zanggu zinanitosha kuchambua mambo ya msingi na kujua wapi pa kwenda kuwaunga mkono ili tulete mabadiliko ya kweli

  Shime!!! shime!!! Hima!!! Hima!!! Watanzania tuuungane kona zote za nchi kuleta mabadiliko ya kweli na kuacha ubinafsi wa kimatabaka na tusitumiwe vibaya na watu wasiopenda maendeleo na mabadiliko ya kweli tushikaname kama tulivyozoea zamani kuita maanadamano ni matembezi ya mshikamano.:sad::sad::sad::sad::embarrassed::embarrassed::embarrassed::embarrassed::embarrassed:

  MUNGU IBARIKI TANZANIA NA MUNGU WALAANI WOTE WENYE NIA MBAYA NA NCHI HII KWA UFISADI NA M
  ATAKWA YAO BINAFSI. Amen
  :sad::embarrassed:
   
 2. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni kwamba watanzania hatujui mambo gani yanayotuunganisha.

  Ni kweli tuna tofauti za kiimani/dini lakini - polisi kuua raia hakuna dini na hatukupaswa kutofautiana.
  CDM na CUF wanaweza kupishana juu ya mambo ya kambi ya upinzani lakini - katiba inawahusu wote maana CCM itaendelea kuwanyuka come 2015 kwa katiba hii.
  TUCTA wanapigania haki za wafanyakazi, asasi za kiraia zinapigania haki za wananchi (wafanyakazi wakiwemo) lakini - bado hawaoni issue kama kupanda kwa gharama za umeme inawaunganisha wote.
  UVccm wanakabana koo na Bodi ya mikopo na wamepanga maandamano ilihali - CDM walishalisemea kwenye mkutano wao na wanachuo, kwani kuna shida gani hawa vijana wakiungana kuwa na sauti moja yenye nguvu. Adha ya mikopo kwa wanafunzi inapaswa kuwaunganisha kama kweli nia ni kumpigania mwananfunzi.

  Tumeparaganyika kila mtu kivyake na watawala wanafurahia tunapogawanyika.
  Hivi unafikiri kwa nini Mubarak alifungia mawasiliano ya simu, internet, facebook, twitter n.k kama si hofu ya a unified force kama ilivyotokea Tunisia??

  Wapinzani Misri wamemchagua El-Baradei kuwa msemaji wao ili kusiwe na sauti nyingi zaitakazowachanganya wananchi.
  Sauti ya wamisri huwezi kuiita kelele za mlango

  Kwa hapa kwetu hilo tunaona halipo tutaandamana kila wiki kwa vikundi vidogo vidogo tukiwaacha watawala wanalala usingizi maana wanaona ni kelele za mlango.

  Mungu na atujalie watanzania hekima ya kutambua kwamba anayesababisha madhira yetu ni mmoja, tushikamane kama mtu mmoja na ushindi ni hakika.
  Waisrael enzi hizo walizungumza lugha moja nao wakaazimia kujenga mnara ili wamfate Mungu huko huko aliko nao wakafanikiwa kuwa mtu mmoja isipokuwa walivurugikiwa baada ya kutofautiana lugha.
   
 3. D

  Derimto JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  RealMan umegusa kunako angalia mfano walimu Arusha wameandamana peke yao wakati tatizo lipo kila mahali nadhani jaman kama tunataka mabadiliko ya kweli tuwe na sauti moja.

  Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu hatuwezi kuishinda hii serikali dhalimu bila kuwa na umoja wa dhati
   
 4. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  HATA TUTAMBIKIE TULIE TUFE TUFUFUKE YANAYOTOKEA MISRI NA TUNISIA HAPA HAYAWEZI KUTOKEA KAMWE

  -WATANZANIA NI WAOGA KULIKO KIUMBE YOYOTE DUNIANI
  -POLISI NA WANAJESHI WAKO TAYARI KUUA KWA AJILI YA CCM
  -NJAA NA TABU HAZITUPI MUDA KUANDAMANA
  -UBINAFSI NA UNAFKI UMETUJAA WATANZANIA HATUKO TAYARI KUTETEA MASLAHI YA WOTE
  -URAFIKI NA UNDUGU TULIONAO SIO RAHISI KUUVUNJA KWA SABABU YA ITIKADI ZA VYAMA ,DINI NA KABILA
  -KWETU KIONGOZI NI MKUU HIVYO TUTAMUHESHIMU KWA KILA NENO
  -CCM INA MBINU ZA KIITELIJINSIA KUJUA NI NANI ANATAKA KULETA MAANDAMANO BATILI

  NA SABABU NYINGINE TELE HAPA MAANDAMANO YA NCHI NZIMA HAYAWEZEKANI NA TUSAHAU,TUNA SHIDA NYINGI LAKINI BADO TUNASEMA NDIO MZEE

  WANANCHI WA IGUNGA WALIMPA KURA ZA KUTOSHA ROSTAM AZIZ BILA HATA AIBU,WA MONDULI JE WALIPEWA NINI WAKAMCHAGUA LOWASA KWA KISHINDO NA WATANZANIA KWA UJUMLA WAO WALIKUWA WAMELALA WALIPOMCHAGUA JK TENA?

  HAPA KUNA TATIZO ZAIDI YA MISRI NA TUNISIA NA SIO SAWA KUTUFANANISHA NAO

  kazi ni ngumu sana kupata watu kwenye hayo maandamano
   
 5. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  UMOJA HAPA MWIKO KUTENGANA NDIO STAiLI
   
 6. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Mwana Nchi (SoS) tusikate tamaa, kila safari ina mwanzo wake.
  Wa-Tunisia kuna mahali walainzia kama ilivyo kwa wa-Misri, nasi tunaweza hata kama sio leo.

  Arusha na Mwanza wametuonyesha kwamba inawezekana kama tukidhamiria.

  Sijawahi kuandamana ktk maisha yangu lakini niko tayari mwezi huu kuungana na CUF au CDM, nitachuja hoja zao. Ambako naona kuna maslahi ya nchi zaidi kuliko siasa ndio nitaenda.

  Ila pointi yako ni ya msingi: kwamba TUAACHE ubinafsi kama tunataka mabadiliko ya kweli.
   
 7. D

  Derimto JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Naamini kabisa hiki kinawezekana ila kikubwa hapa lazima watu kwanza tuondoe akili mgando kama kweli tunataka mabadiliko ya kweli na haya ya kuishia kwenye keybord za computer na blackberry tuanze sasa kwa matendo na tutumie vitu hivi vizuri kama Misri Nadhani Misri wametumia vyombo vya mawasiliano vizuri sana pamoja na serikali kutumia nguvu kubwa kutaka kuwazimisha na kufunga mitandao yao yote.

  TUKIAMUA INAWEZEKANA KWANI WAO WAMEWEZA WANA NINI NA SISI TUSHINDWE TUNA NINI?
   
Loading...