Elections 2015 Je, ni kweli Tanzania tuna "majanga?", Hassy Kitine anatia shaka Urais 2015

NYAMALINGO

Member
Jun 14, 2015
32
38
Kuna majanga ya aina nyingi ambayo kimsingi binadamu anakutana nayo.Kuna majanga ya asili na majanga yanayotokana na kazi za binadamu.Lakini majanga ya asili ni rahisi sana kuepukika,kwani ni majanga ambayo hutokea kwa kuzingatia kipindi fulani periodic au hutokea kwa dalili fulani kuonekana au hutokea baada ya ashirio fulani.Ni majanga machache sana katika kundi hili ambayo hutokea ghafla bila ya kutarajia.

Majanga yatokanayo na kazi za binadamu na viumbe wengine ni majanga ya kujitakia.Majanga haya hutokea aidha kwa makusudi au kwa tamaa,Na kwmba,matokeo yake mara nyingi yanamwacha binadamu na majuto badala ya furaha.Watanzania tunatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwezi october tarehe 25.

Ni uchaguzi wa tano tangu nchi yetu iingie katika mfumo wa siasa ya vyama vingi.Ni uchaguzi wa kumtafuta Rais mpya wa nchi yetu,wabunge wapya,wawakilishi wapya na madiwani wapya.

Tayari kuna watiania wa vyama mbalimbali ambao wameonyesha nia ya kugombea urais,ubunge na udiwani.

Lakini kivutio kikubwa kipo ndani ya chama cha mapinduzi CCM.Mpaka sasa Chama cha Mapinduzi kina watia nia takriban 40,ni idadi kubwa sana kuwahi kutokea.

Aidha,Kati ya watia nia hao,kuna baadhi wanafaa kuteuliwa na chama hicho lakini kuna baadhi wasiyostahili hata kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa mtaa.

Hebu tuchukulie mfano wa Dr. Hassy Kitine au Dr. HASSAN KITINE,Mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa wa zamani.

Huyu bwana wakati anajinadi kwa kutangaza kuwa na yeye ni mtia nia,Alisema"Nikichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania ,nitapambana na rushwa kwa nguvu zangu zote".Dr. HASSAN KITINE ni miongoni mwa mawaziri wa Mkapa ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya matibabu feki ya mkewe.

Katika sakata hilo,Mbunge wa jimbo la Mtama mhe. Benard Membe alilithibitishia bunge pasipo shaka kwamba matibabu hayo yalikuwa feki na yaliligharimu taifa doller za marekani 63,000,Ambapo bunge lilimwadhibu Dr. Hassan Kitine kurudisha fedha hizo huku mwenyekiti wa kamati ya bunge ya huduma za jamii ambaye kwa kuhongwa/kupewa rushwa na dr. Kitine na taarifa ya kupotosha bungeni Mhe.Ndassa alifungiwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge.

Leo hii dr. Kitine na wapambe wake wanaeneze maneno ya uongo kwa watanzania kuwa Benard Membe,prf. Mwandosya,Samwel Sitta,Makongoro Nyerere,Mizengo Pinda na Magufuri ni mafisadi na hawafai kuchaguliwa kuwa rais wa Tanzania!.Ni ajabu ajabu na ajabu mara mia!.

Ni lazima akina Kitine na vibaraka wao watambue kuwa wao ndio mafisadi wakubwa ambao kwa kiwango kikubwa wametufikisha hapa tulipo.

Bado anatakiwa atujibu.Je, fedha alizotupora kupitia matibabu feki ya mkewe alirudisha?

Je, baada ya kurudisha fedha hizo alifikishwa mahakamani kama mtuhumiwa mwenye ushahidi?.

Kitine na Apson Mmwang'onda wakiwa kama waajiriwa wa idara ya Usalama wa Taifa, wanaweza kutuambia ni nini kilichotokea katika vifo vya kutatanisha vya Meja Gen. Imran Kombe,Gibson Mwaikambo na Horace Kolimba?.

Ni wakati mwafaka kwa watanzania kuwahoji baadhi ya maswali yenye utata ambayo kimsingi yalitendwa na baadhi ya watia nia!.

Ni wakati sasa kwa watanzania kutambua kuwa tuna majanga na majanga hayo yanaweza kuwa ya kujitakia,na kama ni ya kujitakia basi tutajuta baada ya uchaguzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom