Je, ni kweli Tanzania ajira hakuna au vijana ndio hawaajiriki?

Tufanyeje ss??tukae kuingoja serikali au ndio tuanze kufikiri nje ya box?
Kwa kweli tupo pagumu kwa kujua nini cha kufanya kwa sababu sio biashara wala kilimo kinachokubali... zaidi ni kwamba wenye uwezo na njia wanakimbilia zao kwenye siasa za maslahi binafsi
Sisi tunaoitwa wanyonge tupambane tuu kwa namna yoyote ili mradi mkono uende kinywani.
 
Kabla hujafikiria hizo degree za chupi kama ni moja ya tatizo, ulianza kwanza kujiuliza kwa mwaka labor market inakuwa supplied na labor force kwa kiasi gani na demand ya labor force ipo kiasi gani?!

Uliwahi kujiuliza labor market ina aggregate labor supply ya kiasi gani na aggregate labor demand ni kiasi gani at any time "t"?

Hivi ulitakiwa kuhoji ni nani basi wanafanya kazi huko sekta binafsi au ulitakiwa kuhoji uwezo wa sekta binafsi ku-absorb available labor fource?

Hivi Tanzania hii kuna taasisi yoyote iliyo chini ya sekta binafsi yenye wafanyakazi wanaofikia 10K? Kuna kampuni ngapi zenye angalau wafanyakazi 5K?

Hivi kama watu wasingekuwa wanafanya hicho mnachoita kufikiria nje ya box, ulishawahi kujiuliza ni watu wangapi kila leo wangekuwa wanaokotwa barabarani kwa ajili ya njaa?!! Ulishawahi kujiuliza ni kwa kiasi gani ujambazi, wizi na uovu wa kila aina ambavyo ungekuwa umetamalaki?!

The problem kuna watu mkipata kashughuli ka kuwaingizia vilaki vinne au vitano kwa mwezi ndo basi tena mnaona wengine wote ni mapoyoyo tu lakini nyie ndo ma-gwiji wa kufikiria nje ya box!!
You nailed it! Msumari wa mwisho juu ya jeneza marehemu ashushwe kaburini
 
Hivi hakuna hata mfano mmoja duniani wa nchi iliyofanikiwa kupunguza tatizo la ajira?

Kila siku tuna lalamika humu kuwa hakuna ajira lakini hatupendekezi hatua za kuchukuliwa na serikali au sisi wenyewe mmojammoja au kwa umoja wetu na kupunguza au kumaliza shida hii.
 
Hivi hakuna hata mfano mmoja duniani wa nchi iliyofanikiwa kupunguza tatizo la ajira?

Kila siku tuna lalamika humu kuwa hakuna ajira lakini hatupendekezi hatua za kuchukuliwa na serikali au sisi wenyewe mmojammoja au kwa umoja wetu na kupunguza au kumaliza shida hii.
Hatua & njia kila siku zinapendekezwa mkuu tatizo kuna mtu alishasema hashauriki
 
Back
Top Bottom