Je, ni kweli Tanzania ajira hakuna au vijana ndio hawaajiriki?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau!

Ebu leo tuongee ukweli hivi kweli Tanzania ajira ni tatizo au tatizo ni wahitimu wetu na vyuo vyetu vinavyozalisha hao wahitimu.?

Si kwamba kuna vyuo vinatoa wahitimu wepesi wenye degree na GPA za chupi na zenye uzito wa kinyoya na weupe kichwani kabisa kiasi ambacho hata wawekezaji wanaogopa kuwaajiri sababu wanakosa zile sifa anazotaka muajiri?
Au tatizo lipo kwenye mifumo yetu ya elimu?

Tunasema serikalini hakuna ajira, je na sekta binafsi nako hakuna mbona mashirika binafsi ni mengi je nani anafanya kazi huko?

Je, tuendelee kungoja ajira za serikali au tukubaliane na Kigwa kuhusu kufikiri nje ya box?

Wengi wanaogoma kukubali ukweli wa Kigwa wa kufikiri nje ya box hawana hata watoto wa kusingiziwa au hawatumi na yakutolea.

Ukweli siku zote lazima huwe mchungu ili hiwe ngumu kumeza,kuna mda inabdi tusemwe vibaya ili tupate gazabu na kuongeza juhudi.
 
Wewe either utakua uko kitengo flani unavuta ukwasi kiulaini ,au ni mtoto wakishua au una connections mingi sana mjini hapa .

Watu namna ndio hudhani majobless ni wazembe au hawajiongezi. Maana hata watoto wa ulaya ukiwaambia kuna watu wanakufa kwanjaa yemeni wao watashangaa tu inakuaje mtu anakosa appetite mpaka anakufa kwa njaa ni vigumu kwao kudhani kama mtu anaweza kukosa chakula kabisa.

Kwakifupi ni kwamba who feels knows it.
 
Habari wadau...!
Ebu leo tuongee ukweli hivi kweli Tanzania ajira ni tatizo au tatizo ni wahitimu wetu na vyuo vyetu vinavyozalisha hao wahitimu.

Si kwamba kuna vyuo vinatoa wahitimu wepesi wenye degree na GPA za chupi zenye uzito wa kinyoya na weupe kichwani kabisa kiasi ambacho hata wawekezaji wanaogopa kuwaajiri sababu wanakosa zile sifa anazotaka muajiri????
Kabla hujafikiria hizo degree za chupi kama ni moja ya tatizo, ulianza kwanza kujiuliza kwa mwaka labor market inakuwa supplied na labor force kwa kiasi gani na demand ya labor force ipo kiasi gani?!

Uliwahi kujiuliza labor market ina aggregate labor supply ya kiasi gani na aggregate labor demand ni kiasi gani at any time "t"?
Tunasema serikalini hakuna ajira ,je na sekta binafsi nako hakuna mbona mashirika binafsi ni mengi je nani anafanya kazi huko.??
Hivi ulitakiwa kuhoji ni nani basi wanafanya kazi huko sekta binafsi au ulitakiwa kuhoji uwezo wa sekta binafsi ku-absorb available labor fource?

Hivi Tanzania hii kuna taasisi yoyote iliyo chini ya sekta binafsi yenye wafanyakazi wanaofikia 10K? Kuna kampuni ngapi zenye angalau wafanyakazi 5K?
Je tuendelee kungoja ajira za serikali au tukubaliane na Kigwa kuhusu kufikiri nje ya box????

Wengi wanaogoma kukubali ukweli wa Kigwa wa kufikiri nje ya box hawana hata watoto wa kusingiziwa au hawatumi na yakutolea .

Ukweli huwe mchungu ili hiwe ngumu kumeza,kuna mda inabdi tusemwe vibaya ili tupate gazabu na kuongeza juhudi.
Hivi kama watu wasingekuwa wanafanya hicho mnachoita kufikiria nje ya box, ulishawahi kujiuliza ni watu wangapi kila leo wangekuwa wanaokotwa barabarani kwa ajili ya njaa?!! Ulishawahi kujiuliza ni kwa kiasi gani ujambazi, wizi na uovu wa kila aina ambavyo ungekuwa umetamalaki?!

The problem kuna watu mkipata kashughuli ka kuwaingizia vilaki vinne au vitano kwa mwezi ndo basi tena mnaona wengine wote ni mapoyoyo tu lakini nyie ndo ma-gwiji wa kufikiria nje ya box!!
 
Mm cjasoma maelezo yako ila title yako nimeielewa💯
Jibu NI KWELI KABISA✍ VIJANA WANAZO SIFA ZOTE ZA KUAJIRIKA. we huoni waliosoma walivyowengi mtaani.
NB. Maelezo yako ni maoni yk kama yalivyo yangu. Mkishiba mnatutesa kweli tusio na hizo ajira😬😬😬
 
Habari wadau...!
Ebu leo tuongee ukweli hivi kweli Tanzania ajira ni tatizo au tatizo ni wahitimu wetu na vyuo vyetu vinavyozalisha hao wahitimu.

Si kwamba kuna vyuo vinatoa wahitimu wepesi wenye degree na GPA za chupi na zenye uzito wa kinyoya na weupe kichwani kabisa kiasi ambacho hata wawekezaji wanaogopa kuwaajiri sababu wanakosa zile sifa anazotaka muajiri????
Au tatizo lipo kwenye mifumo yetu ya elimu???

Tunasema serikalini hakuna ajira ,je na sekta binafsi nako hakuna mbona mashirika binafsi ni mengi je nani anafanya kazi huko.??

Je tuendelee kungoja ajira za serikali au tukubaliane na Kigwa kuhusu kufikiri nje ya box????

Wengi wanaogoma kukubali ukweli wa Kigwa wa kufikiri nje ya box hawana hata watoto wa kusingiziwa au hawatumi na yakutolea .

Ukweli huwe mchungu ili hiwe ngumu kumeza,kuna mda inabdi tusemwe vibaya ili tupate gazabu na kuongeza juhudi.
Alieshiba hamjui mwenye njaa. Anaevaa kiatu kinachobana ndio pekee anayajua maumivu yake. Wewe umeshiba hauna shida kabisa
 
Mimi nina ndugu yangu na ujanja wote imembidi aomba ajira ya kufundisha shule ya msingi na kapata na degree anayo.....

Shida unawezaje kufikiria nje ya box, wakati anayezungumza hayo yupo kwenye ndumba ya hali na mali apate ajira ya ubunge?

Hatuna mitaala inayomfanya mtu akitoka au akimaliza ajiajiri ila inategemea na sector mtu kama Dr. au Pharmacist unamtengenezea mazingira akaibe dawa siyo au awauzie karanga wagonjwa? Yuko ofisini 24hours/7

Kuna siku niliwaza hivi wale akina kinjikitile tunajifunzaga na hatukuwahi kuapply? Sikebehi hapana.....

Ipo namna tuwaandae watoto kuwa innovator since chekechea ikiwezekana.....

Saizi mentality za wazazi wanawaza kuwapeleka watoto boarding na English medium akifika chuo na marks zake zote unakuta anaangukia mule mule

We need to change
 
Back
Top Bottom