Michael Chairman
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 922
- 583
Mtaani kuna hali ya sitofahamu juu ya kupanda kwa bei ya mahitaji ya lazima kwenye kaya na jamii na hili limekuwa likitokea kila siku iendayo kwa Mungu , Sukari kwa sasa bei yake ipaa hadi kufikia Tsh 2700/= kwa kilo moja hapa jijini kwetu Mwanza , hali hii inaleta maumivu kwa wanyonge ambao kila kukicha mahitaji haya yanapanda bei posho za vibarua nazo hazipandi kufidia pengo la upandaji wa bei ya bidhaa hizi,.
Bunge kupitia wabunge wake hakuna hata mmoja aliyepeleka hoja binafsi juu ya hili bali wanachohangaikia wabunge wetu ni kwa maslahi mapana yao na si vinginevyo,
Ombi kwa serikali sasa ni wakati muafaka wa kutoa tamko juu ya uapandaji wa bidhaa muhimu hizi na msisubili wabunge wanyanyuke na hoja ya kuahirisha shughuli za bunge kwa kitu kidogo kama hiki.