Je ni kweli sisi tumeuza zaidi katika soko la E.A kama jeykey asemavyo?

Augustine N

Member
Nov 24, 2010
11
1
wakuu wana jamii hongereni kwa elimu bora.

napenda kufahamu uhalisia wa hili swala la watz kuuza zaidi katika soko la jumuiya ya afrika mashariki.
Je imeleta tija kwa kiasi gani kwa mtz?

a.n aka comlee
 
:embarrassed: nafuga kuku na mayai yameshuka bei mfano hakuna. Mayai yameingizwa TZ toka Kenya kwa bei rahisi, na TZ chakula cha kuku na madawa vimepanda bei maradufu. Sijui cha kufanya wala sioni mwelekeo. Labda nihamie hizo nchi zingine ili niwe nakuja kuuza TZ. Kizunguzungu.
 
Thamani ya pesa yetu kwa ujumla imeshuka na hiyo unaiona katika ununuzi wa vifaa/mahitaji ya utengenezaji wa chakula cha kuku -ni ghali sana kwa hiyo hata mayai yetu sokoni ghali wenzetu ni tofauti kabisa bidhaa zao ni chini kwani ndiyo maana wanauza zaidi kwao na hata hapa kwetu.
Lingine pia tangu zamani sisi watanzania si wauzaji wazuri yaani hatujiuzi/hatujitangazi vizuri na hiyo inatucost kila mahali duniani. Vile vile bidhaa hazina kiwango mayai kwa mfano unaona kiini ni cheupe badala ya kuwa yellow hiyo tu inaonesha hakuna kiwango. Wengine watasaidia pia.
 
Huyu jamaa mwache tu mara zote huongea kama hadithi maana hana vigezo wala takwimu sasa tutaamini vipi. Na hiyo si sawa kwani hata kama yeye JK ni mchumi kama tungekuwa tumeuza nje zaidi uchumi ungepanda na sh yetu ingepata nguvu maana pesa ya kigeni imefurika na sokoni mambo yangekuwa rahisi- ni elimu ya uchumi rahisi sana tu haihitaji mtu aende chuo kikuu
 
Back
Top Bottom