Je, ni kweli Serikali haifanyi lolote au tunajipumbaza kisiasa?

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Tumekaa kimya lakini wapuuzi Aina hii wanapaswa kujibiwa.

📄 Katika andiko la Zitto Kabwe Ruyagwaa analalamika kwamba Rais haonekani, Makamu wa Rais haonekani, na badala yake Waziri Mkuu ndio anaonekana akiwa na Waziri wa Afya wakizungumza zaidi juu ya Corona, Covid-19

👀 Katika Macho ya kawaida kwa Mujibu wa katiba yetu nami najibu Kama ifuatavyo

✍ Waziri Mkuu ndiye mwenyekiti wa mfuko wa maafa
✍ Waziri Mkuu ndio mwenye mamlaka ya kutangaza mambo yote yanayohusiana na Maaafa.
✍ Waziri Mkuu Yupo na anawajibika Kama katiba ya Tanzania inavyomtaka na kumwelekeza.
👀Katika macho ya kawaida Zitto hapaswi kulalamika kwamba Rais haonekani.

👣Unapotembea ndani ya Tanzania inamaana upo Tanzania Hivyo Kama Rais yupo Chato, Ni lazima ieleweke kwamba Chato Ni sehemu ya Tanzania na katiba haimzuii mtu kufanya kazi popote ndani ya Tanzania.

✍ Zitto anasema Rais hajahutubia Taifa na hakuna Budget Hivyo anataka Michango iwekwe wazi kila mtu ajue kwamba Budget ya Serikali Ni kiasi gani na Michango ya wadau Ni kiasi gani?

👀 Katika andiko Hilo lililojaaa chuki la Zitto dhidi ya Rais Bila shaka Zitto hajajua kwamba Rais au Waziri Mkuu ni Taasisi ambazo zinamamlaka kisheria kufanya na kusimamia uhai wa wa Tanzania.

🤝Uzalendo huu wa Zitto ambao si wa kitaalamu ni mhemko tu wa kisiasa hauna faida kwa Taifa kwa Sasa ,

🦍Tusiwaogopeshe wa Tanzania Kama Zitto afanyavyo huu Ni upuuzi anaoufanya .

👀Ukiangalia Lockdown zilizofanyika Nchi nyingine bado wamerudi kuziondoa kwakua watu wanakufa si kwa Corona Bali kwa Njaa.

🙏Ni Jambo jema kuacha tuliowapa dhamana tuone Nini wanafanya.
Rais hata huyu Trump anashughulika kwa jinsi anavyoona inafaa na bado maambukizi Ni makubwa na vifo Ni vingi.

👀Sioni haja ya kuanza kupiga kelele ya mapato na matumizi Sasa wakati mambo hayajawa ya kutisha kwa kiasi anachosema Zitto.

🙏Tuombe Mungu huku tukichukua Hatua na si kutaka kwa kua umeandika Barua yako kwa Rais watu wakae ndani Alafu wapewe laki 3 je! Laki tatu itatosha?
 
Zitto ndio unamjua leo kama ni mpuuzi?

Cha ajabu rais anhekuwa ndio yeye anaongea ungesikia wakisema anapenda kuonekana kwenye media,!

Walivyo wajinga hawajui kuwa yale yanayosemwa na mawaziri yana baraka ya Rais.

Kingine wanajitoa ufahamu kwamba Rais ni tasisi siyo mtu mmoja. Wao wamezoea kwenye mivyama yao kwamba anachosema mwenyekiti hakuna wa kupinga na mwenyekiti ndio alfa na umega. Sasa wanataka mambo hayo yawepo hadi selikalini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi gani wameweka lockdown halafu wameiondoa pasipo uhakika wa kuudhibiti ugonjwa?

Nchi zinaongeza muda wa lockdown wewe unasema zinaondoa.

Huko nchi zingine walikokufa hawasali? Tanzania ina kitu gani special mpaka Mungu asikie maombi yenu nchi zingine akae kimya.

Acheni ujinga.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom