Uchaguzi 2020 Je, ni kweli Rais Magufuli ni Rais wa wanyonge?

adriel

Member
Jul 31, 2015
50
32
Katika kile ambacho Rais Magufuli huwa anakisema mara nyingi kuwa yeye ni Rais wa wanyonge na masikini ndicho kimenipa kipaumbele cha kuandika uzi huu.

Ni kweli yeye ni Rais wa wanyonge na masikini, lakini hayuko kuwasaidia hao wanyonge na masikini anaowaongoza kwanini??

Kwasababu ameshindwa kutegua kitendawili cha kuwasaidia na kuwafuta machozi hao wanyonge na masikini. Hawa wanyonge na masikini wamesomesha watoto wao kwa kuuza nyanya na pombe, na serikali ikawashika mkono kwa kuwakopesha vijana kwa ajili ya masomo ya elimu ya juuu.

Na vijana hawa hawa, walipomaliza elimu zao za juu ambazo zinawafundisha kutegemea ajira, wanasubiri ajira na Mheshimiwa Rais wa wanyonge na masikini amefunga kabisa zoezi la kuajiri.

Hapa ndipo ninaposema Mheshimiwa Magufuli amefeli pakubwa kwa 100%, na kibaya zaidi anawaongezea deni lao la mikopo kila mwaka kama fee ya kuchelewa kulipa mkopo wao na bodi ya mikopo Tanzania.

Na hilo halitoshi, anapokuja na kauli ya "MAENDELEO HAYANA CHAMA" Na hapa anafeli tena, anatoka kusema hapa Maendeleo hayana chama, hapo hapo anakuambia nichagulieni Diwani na Mbunge wa CCM, anaenda mbali zaidi na kutoa vitisho kwamba MSIPONICHAGULIA HAWA MTAPATA TABU KWELI KWELI, HAMTAPATA MAENDELEO HAPA.

Hapa ndipo ninasema anafeli pakubwa, analeta siasa za ubinafsi na ubabe, ilihali anatuaminisha kuwa MAENDELEO HAYANA CHAMA.

Naomba kuwasilisha

Kutoka Jangwani
Adriel Joseph
 
TAFAKURI BAADA YA HABARI.

Mkemia na Upinzanium!

Mkemia mmoja nguli, PHD (Permanent Head Damage), alijimwambafy kwa wakemia wenzie mpaka wakampa ukuu wa kitengo!

Mara baada ya kushika ofisi alifanya mambo mengi makubwa ikiwa ni pamoja na kununua vinu vingi vya kuchakata madini. ... lakini kubwa zaidi ni pale alipoutangazia umma kuwa lile tatizo la muda mrefu la madini ya 'Mwambium' kuwa na kiasi kikubwa sana cha 'Upinzanium' yeye atalimaliza na si muda mrefu atapata pure 'MWAMBIUM', yaani 99.999% pure. Wakemia wenzie walipomuambia 'MWAMBIUM' safi kiasi hicho ni hatari na kwamba kiasi fulani cha 'Upinzanium' kinatakiwa kibakie kubalance shobo akawaambia waache kuwashwa ... huku akiwauliza wao walifanya lipi la maana kipindi chao?
Hakuishia hapo, akawatimua mateknishani wawili waliomsaidia sana wakati akiusaka ukuu na kisha kumuajiri mwanasheria, bingwa wa kumsifia, ili awanyamazishe wakemia wenzie...!
Waskia sana ... kumbe mkemia alikuwa haijui vizuri 'MWAMBIUM', kwamba ikiwa safi sana na ukaitunza sehemu moja kuzidi uzito unaokubalika huwa inajilipua yenyewe bila shinikizo la nje (SPONTANEOUS REACTION)! Sasa maabara imelipuka na CHAIN REACTION inatishia kuangamiza kiwanda chote! 🤔🤔🤔 ... ama kweli Kemia bila Fizikia ni Maumivu! ... na nshomile waliishasemaga:" "...yakwatilwa mgogo niwe mshuma! (aliyekutwa na mkungu wa ndizi ndiye mwizi!) CASE CLOSED!

KIBURI SI MAUNGWANA!

😅
👊 ✌✌✌💥
 
Mnamlaumu tu hata yeye nadhani hajajua tatizo lipo wapi? Bila katiba mpya ya kupunguza gharama za serikali kuu hizo ajira mtaendelea kuzisikia kwa walionazo, mfano wakuu wa mikoa na wilaya kila muda wanaajiliwa na kuondolewa alafu wachukue mafao yao na hivyo hivyo nafasi nyingi zipo kisiasa hizo ndo zinakomba hela.
 
Katika kile ambacho Rais Magufuli huwa anakisema mara nyingi kuwa yeye ni Rais wa wanyonge na masikini ndicho kimenipa kipaumbele cha kuandika uzi huu.

Ni kweli yeye ni Rais wa wanyonge na masikini, lakini hayuko kuwasaidia hao wanyonge na masikini anaowaongoza kwanini??

Kwasababu ameshindwa kutegua kitendawili cha kuwasaidia na kuwafuta machozi hao wanyonge na masikini. Hawa wanyonge na masikini wamesomesha watoto wao kwa kuuza nyanya na pombe, na serikali ikawashika mkono kwa kuwakopesha vijana kwa ajili ya masomo ya elimu ya juuu.

Na vijana hawa hawa, walipomaliza elimu zao za juu ambazo zinawafundisha kutegemea ajira, wanasubiri ajira na Mheshimiwa Rais wa wanyonge na masikini amefunga kabisa zoezi la kuajiri.

Hapa ndipo ninaposema Mheshimiwa jiwe amefeli pakubwa kwa 100%, na kibaya zaidi anawaongezea deni lao la mikopo kila mwaka kama fee ya kuchelewa kulipa mkopo wao na bodi ya mikopo Tanzania.

Na hilo halitoshi, anapokuja na kauli ya "MAENDELEO HAYANA CHAMA" Na hapa anafeli tena, anatoka kusema hapa Maendeleo hayana chama, hapo hapo anakuambia nichagulieni Diwani na Mbunge wa CCM, anaenda mbali zaidi na kutoa vitisho kwamba MSIPONICHAGULIA HAWA MTAPATA TABU KWELI KWELI, HAMTAPATA MAENDELEO HAPA.

Hapa ndipo ninasema anafeli pakubwa, analeta siasa za ubinafsi na ubabe, ilihali anatuaminisha kuwa MAENDELEO HAYANA CHAMA.

Naomba kuwasilisha.

Kutoka Jangwani
Adriel Joseph
Hapa ndipo ninasema anafeli pakubwa, analeta siasa za ubinafsi na ubabe, ilihali anatuaminisha kuwa MAENDELEO HAYANA CHAMA.
 
Huyu size yake ilikuwa ni unyapara wa barabara tu hii ya urais ni kosa kubwa sana, sasa kweli hayo ni maneno ya kutamkwa na kiongozi wa nchi anayetegemea kuchaguliwa na watu. Very saddening.
 
Ni Raisi aliyejifelisha na kukiuwa Chama
Hili neno hawawezi kulisema wasiojitosheleza kifikra. "Amejifelisha". Alikuwa na nafasi kubwa ya kuwa Rais bora kipindi anaanza lakini akashindwa kuendeleza fikra bora za kuunganisha Taifa alizoanza nazo. Akawa kama Rais anayeongoza nchi mbili tofauti. Rais wa Chama tawala na Rais wa Wapinzani. Ameshindwa kabisa kutambua kwamba Watangulizi wake wote akiwemo baba wa Taifa waluongoza Taifa lenye Chama tawala na Wapinzani.

Hata tulipokuwa na Chama kimoja humo ndani kulikuwa na Wapinzani wasiokubaliana na kila kitu kinavyoendeshwa na Chama, ushahidi upo. Sasa kama yeye anadhani watu wamgeogopa kukosoa kwa sababu Rais anamiliki Majeshi yote, na amefanikiwa kuzitiisha Mahakama na Bunge chini ya miguu yake alikuwa anajidanganya. Ipo siku hata hawa anaoona wanamshangilia majukwaani watajitokeza hadharani na kutaja madhaifu yake kwa ufasaha na hataamini.
 
Kwa wanaojua..! Naomba kuelimishwa kuhusu yafuatayo:-
Mikopo ya elimu ya juu inalipwa kwa kupitia mishahara au ..?
Kama ni mishahara, mtu asipoajiriwa maisha yake yote anakuwa amejipatia elimu ya juu bila jasho?
Mikopo inakuwa hai kwa muda gani kabla haaijafutwa?
 
Salamu wakuu?

Nimejalibu kuliwazia hili jambo nikitafakari kwa kina. Rais Magufuli anaitwa hasa na wanachama wa CCM Rais wa wanyonge, lakini kivitendo hakuna alichofanya kwenye hii miaka mitano kuendana msemo wake . Badala yake yalofanyike ni kinyume kabisaa.

- Watu wamebomolewa nyumba zao bila kulipwa hata senti huko mbezi na kimala.

- Watu wametumikia serikali kwa miaka mingi lakini wamefukuzwa kwa kukosa cheti cha form four bila kupewa hata nauli

- Hajawahi kutoa kauli yoyote kuonyesha kuguswa na matukio ya wananchi kutekwa na kupotezwa.

- Pale bukoba kulitokea tetemeko, maafa na uharibifu wa makazi vilitokea.hatukuona raisi akionyesha kwa vitendo kwamba kweli yeye ni Rais wa wanyonge . sanasana tuliona akiwakejeli na kuzuia Rambirambi

Na mifano mingine mingi.

Mwenye kujua wadau. Huyu mkuu wetu anaposema yeye ni Rais wa wanyonge ana maanisha nini, ni wepi hao wanyonge. Je, ni sisi Watanzania?
 
Back
Top Bottom