Je ni Kweli Pogba ana Thamani ya Paundi Milioni 100?

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
1,387
3,453
Mjadala mkubwa kwa sasa Duniani kwa wapenzi wa mpira ni Man Utd kutaka kumsajili Pogba kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao Msimu ujao. Lakini klabu inayommiliki Paul Pogba, Juventus ya Nchini Italy inahitaji Paundi Milioni 100 kama ada ya uhamisho ili kuweza kumuachia mchezaji huyo.

Je ni kweli Pogba ana thamani ya Paundi Milioni 100? Ada ambayo itavunja rekodi ya Dunia katika Uhamisho? Tuweke unazi pembeni, Pogba ana nini cha ziada kufikia hela hiyo? Je Pogba anakuzwa kuliko uwezo wake? Kama Pogba anauzwa kwa bei hiyo, Zidane angeuzwaje leo hii kama angekuwa anacheza?

Karibuni tujadili.
paul-pogba-juventus-midfielder_3302303.jpg
 
#Time value of money#zidane kipindi chake pesa hazikuwa hivi, usitake kufananisha pesa ya kipindi cha zidane vs now, utakuwa una fail.
 
Mjadala mkubwa kwa sasa Duniani kwa wapenzi wa mpira ni Man Utd kutaka kumsajili Pogba kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao Msimu ujao. Lakini klabu inayommiliki Paul Pogba, Juventus ya Nchini Italy inahitaji Paundi Milioni 100 kama ada ya uhamisho ili kuweza kumuachia mchezaji huyo.

Je ni kweli Pogba ana thamani ya Paundi Milioni 100? Ada ambayo itavunja rekodi ya Dunia katika Uhamisho? Tuweke unazi pembeni, Pogba ana nini cha ziada kufikia hela hiyo? Je Pogba anakuzwa kuliko uwezo wake? Kama Pogba anauzwa kwa bei hiyo, Zidane angeuzwaje leo hii kama angekuwa anacheza?

Karibuni tujadili.
paul-pogba-juventus-midfielder_3302303.jpg
Pogba ni mchezaji mzuri, lakini si kwa kiwango cha kuvunja rekodi ya usajili. Siamini katika hilo
 
Du apo tumepaniki tu bora tu mrudishe christan na chenji juu aje kumalizia mpira wake hom
 
Juventus Bado wanamuhitaji Ndo maana wakataja kiwango hicho,na wakiona demand inaongezeka wataongeza pia bei
 
homa za vipindi huyo anapanda na kushuka hana thamani ya millioni 100. timu itakayolipa hiyo pesa imekula kwake. bora mara 100 kumnunua yule dogo wa ureno sijui anaitwa sanchez kwa hiyo pesa kuliko kumnunua huyo pogba. dogo kaonyesha anaweza mwanzo mwisho toka apewe nafasi. pogba akicheza leo vizuri mechi mbili zijazo anaharibu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom