tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,851
Ndugu wana JF,
Kama una Passipoti (Passport), basi fungua ukurasa wa Mwanzo kabisa, utaona ngao ya Taifa na chini yake kuna maneno ambayo ukiyatafakari kwa kina utaona kuwa yanakinzana kwa kiasi Fulani na katazo la kusafiri nje ya nchi kwa mtu, hasa mtumishi wa umma ambaye tayari amekabidhiwa pasipoti kihalali.
Maneno hayo yanasomeka hivi:
"HII NI KUWAOMBA NA KUWASIHI, KWA JINA LA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WALE WOTE WANAOHUSIKA, KWA KUSUDI LA KUMRUHUSU MWENYE PASIPOTI HII KUPITA BILA KIZUIZI AMA KIPINGAMIZI CHOCHOTE NA VILE VILE KUMPA MSAADA NA ULINZI WOWOTE AMBAO UTAKAOONEKANA WA LAZIMA"
Kwa maana hiyo, kitendo cha kumkabidhi mtumishi wa Umma, pasipoti halali ya Tanzania yenye maneno hayo hapo juu, umempa na kumuombea ruhusa, tena kwa jina la Rais.
Kwa hiyo basi, ili katazo la kusafiri nje kwa watumishi wa umma liwe na nguvu zaidi, inabidi maneno haya yabadilishwe na kiongezwe kipengere chenye kuonesha "ruhusa" kwa mtumishi wa umma anayesafiri. Vinginevyo akitokea mtumishi wa umma mjanja akaenda mahakamani na tafsiri ya maneno haya kwenye pasipoti, nadhani ataleta heka heka za kutosha.
Nawasilisha, kwa maoni, kukosoa, maelekezo na mapendekezo.

Last edited: