Je, ni kweli ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ina hela kuliko ofisi ya Mkuu wa Wilaya ?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,252
2,000
Bongo mambo mengi sana.

Mkuu wa Wilaya anapeperusha bendera ya taifa na ana power kwenye Wilaya kuliko Mkurugenzi wa Halmashauri yake.

Inasemekana ofisi za maDC hazina hela kabisa kama zilivyo za maDED.

Kwa nini maDC wasipewe hela za kutosha maana ndiyo wawakilishi wa Mh. Rais na hata kimajukumu DC anamzidi DED.

Hi set up ikoje wadau?


Sent using Jamii Forums mobile app
 

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,568
2,000
Tengeneza swali lieleweke vizuri zaidi, ana hela za ofisi ama za kwake Kama mshahara na marupurupu mengine?
 

Mzee Wa Kale Kabisa

JF-Expert Member
Mar 25, 2018
1,437
2,000
Wote wale wale tu, kinachombena DED ni kuwa na makusanyo yani vyanzo vya mapato vya halmashaur husika viko chini yake. Ila kwa suala la OC wote sawa tu japo hii inategemea na halmashauri au wilaya husika kiutendaji na kimkakati
 

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,166
2,000
Ni vyema ukajielimisha kujua muundo wa serikali na majukumu ya kila chombo / ngazi ya serikali.

Fedha za miradi na matumizi na mapato yote ya haashauri yanasimamiwa na DED. Ofisi ya Wilaya ni ofisi ya usimamizi tu haitekelezi kitu chochote. Haijengi barabara wala hainunui panadol za zahati zilizoko chini ya halmashauri/wilaya.

Hivyo DED ana bajeti kubwa na majukumu makubwa vile vile. Fedha siyo zake ila ni za serikali. Yeye ni msimamizi tu. Mshahara wa mkuu wa wilaya na malupulupu mengine ni mkubwa kuliko wa DED. Unless DED awe fisadi kipato chako hakizidi cha mkuu wa wilaya.
 

ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
1,670
2,000
Nimekuja mbio nilidhani unaongelea
net worth zao maana kuna DED namdai hela mbuzi miaka nenda rudi ananitia sounds ndio nimejikuta nataman kujua vipato vyao
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,962
2,000
Wote wale wale tu, kinachombena DED ni kuwa na makusanyo yani vyanzo vya mapato vya halmashaur husika viko chini yake. Ila kwa suala la OC wote sawa tu japo hii inategemea na halmashauri au wilaya husika kiutendaji na kimkakati
Una uelewa lakini kuhusu hizi ofisi mbili?!

Hivi unafahamu over 90% ya waajiriwa wilayani wapo chini ya DED?

Hivi unafahamu miradi karibu yote ya serikali wilayani ipo chini ya DED?

Hivi unafahamu mashule, hospitali, vituo vya afya na zahanati karibu zote zipo chini ya DED?

Hivi unafahamu barabara zote za wilaya husika mfuko wa ujenzi wake (Road Fund) ipo chini ya DED?!

Itoshe tu kusema kwamba, kwa DC hakuna kitu... ni yeye na DAS wake, basi! Bora miaka ya nyuma shule za sekondari zilikuwa chini ya serikali kuu!!
 

Bombabomba

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
998
1,000
Ninavyofahamu DC ni mwanasiasa, na Mkurungenzi awe wa Mjini, Wilaya, Manispaa na Jiji ni Mtendaji Kimuundo. Zamani DED Alikuwa ni lazima awe Afisa Mwandamizi Serikali kwa maana ya Kafanya Kazi kwenye nafadi za juu kwa miaka osiyopungua 12.

Hivyo aliijua Halmashauri vilivyopo, ndiye msimamizi wa shughli zote zamaendeleo na watumishi KTK Halmashauri. Lkn kwa Sasa Dc na baadhi ya maded wote waweza kuta ni wanasiasa tunkwa sababu wote huteuliwa.

Ni kweli DED kimjukumu ni mkubwa sana na Matumizi ni makubwa. Dc anaweza omba gari, MAFUTA na posho kwa DED, lkn DED hawezi pewa hayo na Dc. Hawa wawili wakiwa PAMOJA shughuli zinaenda vizuri, wakikosana noma sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

All TRUTH

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
4,332
2,000
Ila jua DED ANAPATA MAPAATO MENGI KUMZIDI DC BILA HATA KUWA FISADI SEMINA NA WASHA ANAZOPATA DED ZINAMZIDI DC NA PESA ZA UFUATILIAJI NI NYINGI MNO ZAIDI YA DED.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kabulala

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
269
500
Watanzania tusiwe mbumbumbu kiasi hiki na kufanya akili zetu kuganda, si DC wala DED mwenye ata senti moja, pesa zote ni za wananchi,DED na DC ni watumishi tuu wa wananchi.
 

Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
6,094
2,000
Hivi punde,
Dc na RC hawana kazi ndo maana watanzania walipendekeza nafasi hizo zifutwe maana Jamaa wanazitumia kuwahonga michepuko yao na kuwasaidia makada uchwara Kama akina muru angalau watoto wao waende chuoni,ila hazina tija yoyote kwa taifa hili
 

Chrismoris

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
13,205
2,000
Dc na RC hawana kazi ndo maana watanzania walipendekeza nafasi hizo zifutwe maana Jamaa wanazitumia kuwahonga michepuko yao na kuwasaidia makada uchwara Kama akina muru angalau watoto wao waende chuoni,ila hazina tija yoyote kwa taifa hili
Rc ni mtu mzito sana ambaye alitakiwa awe anapatikana kwa kupigiwa kura.

Kwa Marekani RC ni sawa na Governor. Ambapo Governor ni kiongozi wa State.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom