Je ni kweli ndoa inaongeza urefu wa maisha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni kweli ndoa inaongeza urefu wa maisha?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SMU, Jun 2, 2009.

 1. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  LIVING IN their own home with a loving husband and children is the ambition of almost all women though not all achieve this ambition.


  A new survey from America shows why women want this. The results of the survey show that:
  • 10.7 of each 1,000 unmarried women die each year, compared to 5.7 married women.
  • Across all causes and all age groups, unmarried women have a 42-114% higher premature mortality rate than married women.
  • Of every 1,000 women who divorce before the age of 30, at least 378 will die before they reach 65 compared to only 266 married women.
  Kwa uzoefu wako (casual observation!), je kuna uwezekano, matokeo ya utafiti huu yakawa valid hata kwa wanawake wa hapa africa/tanzania? Kama ni tofauti, unadhani ni nini kinachangia?
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kutuwekea matokeo ya utafiti huu.
  Kabla ya kujibu swali lako naomba unijuze sababu ya vifo maana hiki ni kigezo muhimu cha kulinganisha nakuona kama kuna huo uwezekano.
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Katika utafiti huo ni kufa kwa sababu zozote zile. Angalia vizuri hiyo bullet ya pili.
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  hayo matokeo hayatoshelezi... hivyo nasita kusema kuwa kuna uwezekano kwa Tanzania
   
 5. i

  isdory Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maisha ya ndoa yanafupisha sana maisha
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Jaribu kutizama wanawake(wabibi) ambao unadhani wameishi muda mrefu. Were they married or not?
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwa nini?
   
 8. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Inawezekana ikawa kweli katika aspect hii hapa chini.


  FAIDA SEX KWA AFYA YA MWILI
  Huimarisha immune system kwenye mwili.
  Wanandoa ambao hushiriki angalau mara mbili kwa wiki walionesha kiwango kikubwa cha antibody zinazosaidia kupigana na magonjwa.

  Huongeza umri wa kuishi.
  Wanaume ambao walikuwa wanafika kileleni (orgasm) zaidi ya miaka 10 wali- boost uwezo wa kuishi miaka zaidi kuliko wale ambao walikuwa na hawafiki kileleni.

  Hupunguza uwezekano wa kupata prostate cancer.
  Wanaume ambao wali ejaculate zaidi ya miaka 35 walikuwa na asilimia 33 pungufu kupata prostate cancer.

  Hupunguza cholesterol (mafuta)
  Kutokana na zoezi la kufanya mapenzi (sex) ni zoezi tosha kuweza kupunguza cholesterol na kuondokana na kupata magonjwa ya moyo.

  Huimarisha mzunguko wa damu mwilini
  Tunapofanya mapenzi mapigo ya moyo huongezeka na mzunguko wa damu huwa na speed zaidi na damu huongezekana maradufu kwenye ubongo na sehemu zingine za mwili na matokeo ni mzunguko wa damu kuwa mzuri mwili mzima.

  Huongeza uwezo wa kukua (growth)
  Watafiti wengi wanakiri kwamba sex huongeza uwezekano wa mifupa kukua na kuimarisha repair ya tishu kwenye mwili.

  Hupunguza maumivu (pain relief
  Unapokaribia kufika kileleni kiwango cha homoni za oxytocin huongezeka mara tano zaidi kuliko kiwango cha kawaida, matokeo ni kutolewa kwa endorphins ambayo hupunguza maumivu ya kila kitu kuanzia kichwa, arthritis nk.


  Hupunguza uwezekano wa kupata cancer ya matiti.
  Wanawake ambao hawajawahi kuzaa walionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata cancer ya matiti, hii ina maana kwamba kujihusisha na sex hupunguza kupata cancer ya matiti.

  FAIDA YA SEX KWA AFYA YA AKILI
  Hupunguza stress
  Sex huweza kupunguza stress kwa kupunguza kiwango cha masumbuko (anxiety) na kuongeza relaxation na kusaidia kuwa na usingizi mzuri.

  Hupambana na depression
  Wanawake ambao walijihusisha na sex kwa kuwa contact na semen walikuwa less depressed kuliko wale wambao hawakufanya.

  Hupambana na kuthibiti alama za kuzeeka
  Sex hufanya mtu kuonekana kijana zaidi.
  Katika utafiti mmoja watu ambao walishiriki sex zaidi ya mara 3 kwa wiki walionekana ni vijana zaidi ya miaka 10 pungufu ukilinganisha na wale ambao walikwepa sex.​

  Huimairsha kujisikia upo fit
  Dakika 30 za kufanya mapenzi huweza kuchoma kiasi cha 150 calories.
  Na mtu anayeshiriki sex kila mara 3 kwa wiki huweza kupunguza kilo 2.5 za uzito kwa mwaka. Pia sex huweza kunyumbua misuli na kupelekea mtu kuwa fit, pia hekaheka za milalo mbalimbali huweza kufanya contractions ya mapaja, mikono, mabega, shingo, tumbo, kifua, mgongo, ******, miguu, kiuno na pia sex huzalisha testosterone ambayo huimarisha mifupa na misuli.​
  FAIDA YA SEX KWA AFYA YA UZAZI
  Husaidia kuwa na mzunguko mzuri za siku za mwanamke.
  Wanawake ambao hujihusisha na sex angalau siku moja kwa wiki huwa na
  mzunguko wa siku uliosawa tofauti na wale ambao hutoa visingizio.​

  Huimarisha fertility
  Kwa kuwa kushiriki sex hufanya mzunguko kuwa regular inakuwa rahisi mwanamke kushika mimba na kuzaa tofauti na mwanamke akiwa na mzunguko wa siku ambao ni irregular.

  FAIDA KATIKA KIROHO
  Watafiti wengi wanakiri kwamba kuna sexual energy kama energy zingine ambayo wakati wa sex ikiunganishwa kati ya mwanaume na mwanamke hasa wakati wa kufika kileleni huweza kuwaunganisha wawili in deepest part of of selves. ​

  Na hii energy (non physical) huweza kuimarisha maeneo mengine ya maisha yetu, hutufanya kujisikia ni kitu kimoja na kuwa stronger zaidi katika nafsi na mahusiano kwa ujumla.
  Hivyo matokeo ni kujisikia vizuri wewe mwenyewe, mwenzi wako na maisha kwa ujumla.

  TAHADHARI:
  Hii mada ni kwa ajili ya kupeana habari tu (ndiyo maana hakuna reference links, ingawa unaweza mwenyewe ku- Google),
  Jambo la msingi ni kwamba kuna umuhimu wa hali ya juu sana kuzingatia kwamba hapa tunazungumzia sex katika ndoa tu na si zaidi ya hapo.
  Pia ni muhimu kuzingatia kwamba ili kushiriki sex ni muhimu kuangalia afya ya mwenzi wako, maadili na kutii sheria na amri za Mungu otherwise badala ya sex kukupa afya inaweza kukuua kimwili na kiroho.​

  Upendo daima!​
  source: The Hill Of Wealth


  mapenzi sex afya kimwili kiroho kiakili
   
 9. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  sex inafanyika kwa wliokatika ndoa na wale ambao hawapo katika ndoa.
  hivyo sidhani kama sex ni kigezo cha uhakika katika kujadili kama ndoa inaongeza urefu wa kuishi kwa wanandoa
   
 10. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  labda sababu ya kuwa sex ndani ya ndoa ni rasmi and you don't feel guilty psychologically.

  lakini kwa wanaume ndoa inafupisha maisha sababu ya responsiblities unazokuwa nazo hasa kama income in utata.Unafanya kazi nyingi na za hatari ili kufanikisha maisha yako na vitegemezi vyote ulivyonavyo nyumbani kwako.
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kuna factors nyingi zinazoweza kuunga mkono maoni haya, lakini nyingine pia zinaweza kuleta shaka.

  Kwa mfano, inawezekana kuwa rahisi zaidi, under constant conditions, kwa watu wasiokuwa katika ndoa kupata magonjwa yanayohusiana na kujamiiana kama UKIMWI na mengineyo, kuliko watu waliooana.Nakubali kwamba hili linahitaji kuelezewa kwamba ndoa haibadilishi tabia ya mtu ila kuna uwezekano mkubwa wa mtu asiye katika ndoa kuwa na uhuru mkubwa kijamii na kisheria kujamiiana na watu wengi kuliko mtu aliye katuika ndoa.

  Kwa upande mwingine mtu anaweza kusema kuwa ndoa zenye matatizo zinaweza kuwapa wanandoa msongo wa moyo kwa kiasi kikubwa kuliko wale wasio katika ndoa.

  Tafiti zaidi inabidi zifanywe kuweza kujua wiano zinavyofumuka.
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Stanfford si tunaambiwa mapenzi hupunguza stress za maisha?
   
Loading...