Je, ni kweli NCCR Mageuzi ilitoka wabunge sita mpaka mmoja kwa sababu ya Ukawa?

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
3,590
8,475
Ningependa watu wajadili hoja hio ya Mh Mbatia kuwa NCCR Mageuzi, haikunufaika na Ukawa bali ilizamishwa na Ukawa? Je, kuna ukweli hapo? Maana sikufahamu Kama NCCR Mageuzi ilikuwa na wabunge 6 kabla ya 2015, na kabaki mmoja tu.

Kwamba aliitoa taasisi ya NCCR Mageuzi kisa Ukawa lkn hakulalamika.

Je, mfano CUF&CHADEMA&ACT Kuna chama kimojawapo kinaweza ruhusu kipungukiwe na wabunge kisa ushirika?

Je, inawezakana mwaka huu CHADEMA wakaachia mgombea uraisi atoke chama kingine, Kisha wao kwa nguvu yao wamsapoti ili kuonesha ushirika wa kweli?

Je, inawezekana maalimu akubali kuaacha kugombea uraisi Zanzibar, awapishe CHADEMA Kisha yeye awasapoti?

Kama upinzani watashirikiana basi wawe makini na kushirikiana kwao, bila tume huru ya uchaguzi hakuna uchaguzi huru.

Mageuzi ya kweli yalisalitiwa 2015 kwa kumpa tiketi fisadi kugombea uraisi.
 
UKAWA walikuwa na makubaliano kila chama kinachounda umoja wao wamsimamishe mgombea mmoja pale ambapo chama husika kinaamini kina nguvu za kutosha.

Sasa kwa NCCR ya Mbatia nayo ilipewa hiyo nafasi, lakini matokeo yake pamoja na Mbatia kuongezewa nguvu na vyama vilivyounda UKAWA bado akashindwa.

Hii maana yake ni kwamba Mbatia na wagombea wake hawakuwa na ushawishi kwa wapiga kura kwenye majimbo husika, hivyo kuwalaumu UKAWA kwenye hili Mbatia amekosea sana.

Kwa muktadha huo, inawezekana kabisa Mbatia na NCCR yake ndio waliovihujumu vyama vingine vya UKAWA, kwasababu inawezekana vilikuwa na wagombea wanaouzika zaidi kwa wapiga kura, but ikawalazimu wamuachie Mbatia kulingana na makubaliano yao, hii ikasababisha wagombea wa CCM kushinda kwa urahisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kuelewa hilo angalia dhana nzima ya kupata viti maalumu.

Kwanza unatakiwa uelewe kuwa viti maalumu wanapatikana kutoka na asilimia kila chama ilizopata kwa kura za urais kwenye uchaguzi mkuu na 2015 ni CHADEMA tu ilipata kura chini ya ukawa. Unadhani vyama vingine ,wabunge wa viti maalumu wangewapataje?

Tanzania hakina sheria ya vyama kuungana ila kulikuwa na makubaliano tu hivyo kwa vyovyote vile sheria ina nguvu kuliko makubaliano. Sheria inatambua kwamba ,wabunge wa viti maalumu wanatakiwa wawe 30% ya wale wa kuchaguliwa na mgawanyo wa hiyo 30% utatokana na idadi ya asilimia kila chama kilizopata uchaguzi mkuu kwa kura za urais. Je vyamà vingine chini ya ukawa wangepataje wabunge?
 
Acha uongo wewe mbona CUF wana wabunge wa viti maalum, je walikuwa na mgombea urais? Wabunge viti maalum wanatokana na asilimia ya wabunge wa kuchaguliwa.
 
Mbatia alikuwa ni kirusi ndani ya ukawa
UKAWA walikuwa na makubaliano kila chama kinachounda umoja wao wamsimamishe mgombea mmoja pale ambapo chama husika kinaamini kina nguvu za kutosha.

Sasa kwa NCCR ya Mbatia nayo ilipewa hiyo nafasi, lakini matokeo yake pamoja na Mbatia kuongezewa nguvu na vyama vilivyounda UKAWA bado akashindwa.

Hii maana yake ni kwamba Mbatia na wagombea wake hawakuwa na ushawishi kwa wapiga kura kwenye majimbo husika, hivyo kuwalaumu UKAWA kwenye hili Mbatia amekosea sana.

Kwa muktadha huo, inawezekana kabisa Mbatia na NCCR yake ndio waliovihujumu vyama vingine vya UKAWA, kwasababu inawezekana vilikuwa na wagombea wanaouzika zaidi kwa wapiga kura, but ikawalazimu wamuachie Mbatia kulingana na makubaliano yao, hii ikasababisha wagombea wa CCM kushinda kwa urahisi.

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Wewe kila post yako ni sifuri kabisa
Ukitaka kuelewa hilo angalia dhana nzima ya kupata viti maalumu.

Kwanza unatakiwa uelewe kuwa viti maalumu wanapatikana kutoka na asilimia kila chama ilizopata kwa kura za urais kwenye uchaguzi mkuu na 2015 ni CHADEMA tu ilipata kura chini ya ukawa. Unadhani vyama vingine ,wabunge wa viti maalumu wangewapataje?

Tanzania hakina sheria ya vyama kuungana ila kulikuwa na makubaliano tu hivyo kwa vyovyote vile sheria ina nguvu kuliko makubaliano. Sheria inatambua kwamba ,wabunge wa viti maalumu wanatakiwa wawe 30% ya wale wa kuchaguliwa na mgawanyo wa hiyo 30% utatokana na idadi ya asilimia kila chama kilizopata uchaguzi mkuu kwa kura za urais. Je vyamà vingine chini ya ukawa wangepataje wabunge?

In God we Trust
 
NCCR mageuzi na CCM ni mtu na mjomba wake ndio maana Mbatia alivyotoka hapo Magogoni akaelekea Mbeya kwa Mkuu wa Mkoa na kunywa nae chai baadae igizo la kuzuiwa na kisha kupokea wanachama wa chadema.
 
Hivi yuko wapi Felix Nkosamali? , alikuwa Mbunge kupitia NCCR Mageuzi awamu iliyoita.
 
Ningependa watu wajadili hoja hio ya Mh Mbatia kuwa NCCR Mageuzi, haikunufaika na Ukawa bali ilizamishwa na Ukawa? Je, kuna ukweli hapo? Maana sikufahamu Kama NCCR Mageuzi ilikuwa na wabunge 6 kabla ya 2015, na kabaki mmoja tu.

Kwamba aliitoa taasisi ya NCCR Mageuzi kisa Ukawa lkn hakulalamika.

Je, mfano CUF&CHADEMA&ACT Kuna chama kimojawapo kinaweza ruhusu kipungukiwe na wabunge kisa ushirika?

Je, inawezakana mwaka huu CHADEMA wakaachia mgombea uraisi atoke chama kingine, Kisha wao kwa nguvu yao wamsapoti ili kuonesha ushirika wa kweli?

Je, inawezekana maalimu akubali kuaacha kugombea uraisi Zanzibar, awapishe CHADEMA Kisha yeye awasapoti?

Kama upinzani watashirikiana basi wawe makini na kushirikiana kwao, bila tume huru ya uchaguzi hakuna uchaguzi huru.

Mageuzi ya kweli yalisalitiwa 2015 kwa kumpa tiketi fisadi kugombea uraisi.
Mbatia kalipwa mkuu , usijihangaishe naye , lakini aliyemlipa ameliwa
 
Kafulila aliyegombea kupitia NCCR alidai kuwa alishinda na kupokwa ushindi na tume ya CCM, sijui UKAWA walihusikaje hapo, Machali naye aliibwaga NCCR na kuhamia ACT wazalendo sijui na hapo UKAWA napo ilihusika vipi, labda kama angemulaumu Zitto hapo kwa mbali angekuwa na ukweli fulani.
 
Mbatia ni wakupuuzwa,vyama vingine vya upinzani msimjibu chochote huyo mgonjwa, anatafuta pesa za matibabu.
 
Muulize huyo msaliti Mbatia kama UKAWA ndo ilimkosesha Ubunge mwaka 2010 mpaka akapewa Ubunge wa viti maalumu na Kikwete.
Wajinga kama huyu afanye tu kazi yake ya usaliti bila kusumbua watu na aache kuropoka kuonyesha uanamke wake.
 
Ukitaka kuelewa hilo angalia dhana nzima ya kupata viti maalumu.

Kwanza unatakiwa uelewe kuwa viti maalumu wanapatikana kutoka na asilimia kila chama ilizopata kwa kura za urais kwenye uchaguzi mkuu na 2015 ni CHADEMA tu ilipata kura chini ya ukawa. Unadhani vyama vingine ,wabunge wa viti maalumu wangewapataje?

Tanzania hakina sheria ya vyama kuungana ila kulikuwa na makubaliano tu hivyo kwa vyovyote vile sheria ina nguvu kuliko makubaliano. Sheria inatambua kwamba ,wabunge wa viti maalumu wanatakiwa wawe 30% ya wale wa kuchaguliwa na mgawanyo wa hiyo 30% utatokana na idadi ya asilimia kila chama kilizopata uchaguzi mkuu kwa kura za urais. Je vyamà vingine chini ya ukawa wangepataje wabunge?
ACT ina Wabunge wangapi wa viti maalum au nayo haikuwa na mgombea Urais? Au ukisimamisha tu mgombea urais hata ukipata kura 10 unapewa viti maalum?
Chama gani kilikuwa juu kati ya ACT na NCCR?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom