Je, ni kweli NASA ilidanganya kuhusu safari ya mtu wa kwanza kutua mwezini(Apollo Moon Mission)?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,743
25,535
Apollo Moon Mission sio jina geni kwa wafuatiliaji wa mambo ya anga, kwani mnamo mwaka 1969-1972 shirika la anga la Marekani (NASA) lilifanikiwa kupeleka binadamu wa kwanza mwezini na kuushangaza ulimwengu, lakini kuna baadhi ya madai kuwa mission hiyo ilikuwa fake na haikuwahi kutokea.
4dbd146cbc35ffb319ed3ffe72535506.jpg

Neil Armstrong kama inavyofahamika ndiye binadamu wa kwanza kutua katika mwezi, katika safari iliyofanywa na wanaanga watatu wa kimarekani iliyofahamika kama Apollo Moon Mission katika miaka ya 1969-1972.
1a376c233fff4410cb70b85c0bc33f35.jpg

Hatuna sababu ya kujua wa pili alikuwa nani au watatu alikuwa nani ila kikubwa kinachoitia dosari safari (mission) hii ni kuibuka kwa madai kuwa Marekani walidanganya ulimwengu na hakuna safari kama hii iliyowahi kufanyika katika kipindi hicho.
ecaf6e700e94a11e88d0bb77a7ec2b88.jpg

Madai hayo yamegawanyika katika makundi mbalimbali na kila kundi likijaribu kutoa sababu za kwanini hii safari ilikuwa ni ya uongo. Lakini kabla ya kuendelea kuna swali moja la muhimu la kujiuliza, kwanini NASA waliamua kongopea umma kuhusu safari hiyo?


Sababu kubwa inaonekana ni mbio za sayansi ya anga kati ya Marekani na Urusi (USSR) ambazo kwa kipindi hicho zilikuwa zipo katika kilele na zilikuwa zikihusishwa na nguvu ya kisiasa kati ya mataifa hayo mawili makubwa duniani. USSR walikuwa mbali kisayansi na kiteknolojia ya mambo ya anga hivyo ili kushinda mbio hizo Marekani wakaamua kuudanganya ulimwengu kuwa walikuwa wa kwanza kupeleka mtu mwezini.
Kwa mujibu wa kitabu cha “We Never Went to the Moon: America’s Thirty Billion Dollar Swindle”, kilichoandikwa na
Bill Kaysing mwaka 1976, uwezekano wa kutua mwezini ulikuwa ni asilimia 0.0017% kwa kipindi hicho. Hii ilipelekea Urusi kujiandaa na kufanikisha safari yao ya kwanza ya kupeleka mtu wao mwezini.

Shirika la kwanza kutoa maoni yake juu ya uwongo wa safari hii lilikuwa ni Flat Earth Society, likidai kuwa picha na video za mission nzima zilifanyika katika studio maarufu za movie za Walt Disney Studios, Hollywood na kuongozwa na Stanley Kubrick. Huku wakijaribu kufananisha picha za chombo kilichotumika katika mission na chombo kilichoonekana katika muvi ya Capricorn One (1978).

Sababu nyingine inayoonekana kwanini NASA waliamua kufake hii mission ni kujaribu kujipatia kiasi cha fedha ili kuweza kujiimarisha zaidi kwani kiasi cha Dolla bilioni $30bn zilitumika katika mission hiyo. Hii inahusishwa pia na kumridhisha Rais wa nchi hiyo bwana Kennedy aliyeahidi kupeleka mtu wa kwanza mwezini kabla hajaondoka madarakani.

Wengine wanadai NASA waliamua kufanya hivyo ili kukimbiza mawazo ya wengi ambao kwa kipindi walikuwa wakifikiria vita ya Marekani na Viettnam. Kwa kutumia nguvu ya vyombo vya habari ilijaribu kuhamisha mawazo ya wengi kwani vita hiyo na mission hiyo viliisha katika mwaka unaofanana.

Zifuatazo ni sababu mbalimbali zinazojaribu kueleza uongo wa NASA katika safari hiyo.


1. HAKUNA CARTER ILIYOTENGENEZA NA MLIPUKO WAKATI CHOMBO HICHO KINATUA.
1550a17c91f25a47fedf8d4cc7c1f3cc.jpg

Picha za chombo cha Apollo kikiwa kinatua mwezini hazionyeshi vumbi wala shimo la crater lililotengenezwa wakati chombo hicho kikitua mwezini.

2.VAN ALLEN RADIATION BELT:
ad8da0274562d01e09720589fe9c17c1.jpg

Wataalamu wa mambo ya anga wanauliza ni jinsi gani NASA waliweza kuvuka ukanda wa miale wa Van Allen radiation belt kwani miale kutoka katika ukanda huo ungewaunguza wanaanga wote waliokuwemo katika chombo hicho kabla hata ya kutua mwezini. Van Allen radiation belt ni ukanda wenye chembe chembe za hewa zenye chaji ambazo zinashikiliwa na nguvu ya usumaku ya dunia ambayo imegawanyika katika matabaka mawili, tabaka la nje na tabaka la ndani.

3.HAKUNA NYOTA KATIKA PICHA ZOTE ZILIZOPIGWA:
6201c46c40517bd75eaec71f5cc7db74.jpg

NASA walipiga picha nyingi sana wakiwa katika mission hiyo, ila hakuna picha hata moja inayoonyesha nyota za angani jambo ambalo linawafanya watu wengi waamini mission hiyo ilikuwa ni fake na ilifanyika katika studio. NASA walilijibu hilo kwa kudai kuwa picha hizo zilikuwa na ubora hafifu hivyo inawekana nyota zilipotea wakati wa kuziongeza ubora picha hizo.

4. KUPEPEA BENDERA YA MAREKANI MWEZINI:
95451fb128a302c4bbdfd405c69b58c4.jpg

Wataalamu wa mambo ya anga wanadai mwezini hakuna hewa hivyo ni vigumu kwa kitambaa kupepea, hivyo kuonekana kwa bendera ya Marekani ikiwa inapepea mwezini ni dalili tosha ya uongo wa mission hiyo. NASA wamejaribu kulitolea hili maelezo kwa kudai kuwa kupepea kule kuisababishwa na kinetic enertia iliyotakana na wanaanga hao wakati wakijaribu kusimika bendera hiyo.

5.BACKGROUND MOJA:
20ba5291371488e1335ff38495262140.jpg

Baadhi ya picha zilizopigwa na NASA zinaonyesha background moja kati ya zile zilizopigwa kutoka umbali mrefu na zile zilizopigwa karibu. Ushahidi huu unaonyesha kuwa NASA walitumia background moja katika picha nyingi. NASA wakajibu kw kudai kuwa mwezi ni mdogo sana ukilinganisha na dunia hivyo horizons zinaonekana karibu zaidi kwa macho ya binadamu ukilinganisha na duniani. Ni ngumu kuamini hili kuwa picha mbili zifanane hata kama zimepigwa umbali tofauti.

6. JIWE LA MWEZINI:
f45b85fb31709882d66328ee47530d52.jpg

Ilisemekana wanasayansi walirudi na zawadi ya mawe kutoka mwezini, lakini mawe hayo yanaonekana kufanana zaidi na yale yanayopatikana duniani.

7. KUONEKANA KWA MWANGA WA STUDIO.
64b5213b0961f8ef9b1dffa7f1ad4577.jpg

Katika baadhi ya picha: Roger Launius kutoka Smithsonian’s National Air and Space Museum alidai katika moja ya picha zilizoachiwa na NASA mwanga wa studio uliotakana na Lens Flares uikuwa ukionekana wazi wazi wakati akizungumza na National Geographic.
Ukweli wa NASA
Kuwashutumu NASA kwa sababu zilizokaa kinadharia ni moja ya makosa makubwa tunayoyafanya kila siku. Katika kujitetea NASA nao wanasababu zao wakijaribu kuuaminisha ulimwengu ukweli wa Apollo Moon Mission ilikuwa ni ya kweli na si ya kupikwa studio.

1. Ilionekana na vyombo vingine vya Anga:
b1374623c722ceb13e8b0c13aafcb4aa.jpg

Kutua kwa chombo hicho mwezini kulioekana pia na vyombo vingine vya anga kama China’s Chang’e 2 lunar probe.

2. Sura ya furaha ya Neil Armstrong:
188ed484ad8cda4c9ecd4961996dd19c.jpg

Sura ya furaha ya bwana Neil Armstrong baada ya kukamilisha ziara yake katika mwezi inaonyesha ukweli wa ziara hiyo kwani si rahisi mtu kufake tabasamu kwa kitu asichokifanya.
3. Picha za ubora wa hali ya juu zilizotolewa:
ee2ebd55d36c17b9375ec659d1f2e29d.jpg
9c24b786b43ac79eafd38edba59af2c9.jpg

Kipindi kile wakati safari ya Apollo mwezini watu walilalamiki NASA kutoka picha zenye ubora hafifu sana, lakini hivi karibuni katika sherehe za kuadhimisha miaka 40 ya safari hiyo NASA walitoa picha nzuri zaidi zilizofanyiwa marekebisho.


4. Eneo ambalo chombo kilitua bado linaonekana:
a987f0137885e3858ab05c1549680632.jpg

Kuonekana kwa eneo ambalo chombo cha Apollo kilipotua kunaonyesha ushahidi wa ukweli wa safari hiyo. Eneo hilo lilionekana katika picha zilizopigwa na chombo cha Lunar Reconnaissance Orbiter kilichotumwa mwezini June 18, 2009.

5. Uwiano wa picha zilizopigwa na chombo cha kijapan cha mambo ya anga cha Koguya zinaonyesha ukweli kuhusu safari hiyo.
786a6d51f94892d5d8730026118a31f7.jpg

Baada ya kukosolewa sana katika Mission ya Apollo NASA waliamua kutoa fact sheet yao iliyoonyeza mawe waliyokusanya kutoka mwezini, mawasiliano wakati wa safari pamoja na mengine mengi ili kuondoa mawazo ya watu waliokuwa wakipinga safari hiyo.
Mpaka sasa ukweli unajulikana na maafisa wa NASA peke yao pamoja na wananga walioshiriki safari hiyo hivyo ni ngumu kulipinga tukio hilo kubwa kuwahi kutokea katika historia ya maisha ya mwanadamu duniani.




*****The Man From Mars*****
 
Hii safari haijapata kuwepo!
Sababu moja kubwa ya ufeki wa safari hii ni uwepo wa upepo unaopeperusha bendera! Ukiitazama hiyo video clip inaonyesha uwepo wa upepo mkubwa ukipeperusha bendera na si mtikisiko wa bendera unaotokana na watu kuichimbia bendera!
 
Ukitaka kujua kuwa safari hii ilikuwa ina maigizo ndani yake

Hebu jiulize ikiwa mwaka 1972 enzi hizo teknolojia ya kawaida waliweza kutuma mtu mwezini

Je ni kitu gani kilichowashinda kutuma watu wengine katika kipindi hichi ambacho teknolojia ipo imara zaidi?
wamepeleka mara nyingi tu na hata India sasa hivi wanaenda .kiukweli NASA wako mbali wanao wapinga ni watu wanaotumia imani za kidini .
 
Hii safari haijapata kuwepo!
Sababu moja kubwa ya ufeki wa safari hii ni uwepo wa upepo unaopeperusha bendera! Ukiitazama hiyo video clip inaonyesha uwepo wa upepo mkubwa ukipeperusha bendera na si mtikisiko wa bendera unaotokana na watu kuichimbia bendera!
huo sio upepo kwenye mwezi hata mtu anapepea , mbona hizo bendera zinazowekwa na Warusi leo hii zinapepea. Wapinzani wa kubwa wa NASA sio wanasayansi ni watu wa Dini kama ile jamii inayosema Dunia ni flat . Unajua mwezi ulikuwa unaabudiwa Mwezi ulikuwa Mungu katika jamii za kiarabu ndiyo maana mpaka leo kuna dini ambazo zinatumia alama ya Mwezi .
 
nasubiri kwa hamu kubwa kusoma maoni ya wanasayansi feki wa jf wasioamini uwepo wa Mungu juu ya suala hili.
 
Hii inshu imeshakuwa discussed sana Humu mkuu nafikiri unge search tu uzi wa aina hii halafu ukamwaga nondo hizi kuliko kuanzisha uzi mpya, Mimi ninachokumbuka katika safari ya Armstrong ni kuwa huyo jamaa alisikia adhana huko mwezini ingawaje hakuna medium ya kusafirisha sauti (atmosphere) pia ali slim kabla hajafa, Loool faiza Foxy @mahtaan
 
Hii ni hatari sana kwamba ukikosoa jambo lenye kuhusu sayansi unaonekana mdini,kwa maana hiyo hutakiwi kupinga maana utaonekana mdini.

Hii ndiyo sayansi kweli ??
 
Inawezekana walidanganya kisayansi tunaaminishwa sio kitu kigumu lakini kiundani inaingia akilini kuamini walidanganya...

Kutorudi tu tena INATOSHA KUTILIA SHAKA,
 
Back
Top Bottom