Je ni kweli Mnyika ameponzwa na akina Ndugulille, Zungu na Mntenvu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni kweli Mnyika ameponzwa na akina Ndugulille, Zungu na Mntenvu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by shykwanza, Jan 4, 2012.

 1. s

  shykwanza Senior Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika sakata la Magufuli na nauli za kivuko cha kigamboni linaloendelea na huku Mh Magufuli akionesha kuungwa mkono na wakazi wengi wa Dar na Tanzania kwa ujumla juu ya upandishwaji wa nauli za kivuko. Wananchi na wakazi wa Dar na TZ wanaendelea kuwashutumu wabunge wa Dar kuwa ni wanafiki wakubwa na wanajipendekeza kwa wananchi kwa kutumia mbeleko ya nauli za kivuko.

  Ktokana na shutuma nzito zinazoelekezwa kwa wabunge wa Dar hasa kupitia CCM, wachambuzi wa masula ya kisiasa wanasema kukurupuka kwa J. Mnyika kuwaunga mkono kina ndugulille, Zungu na Mntenvu katika kumpinga Mh Magufuli kumempunguzia umaarufu wake wa kisiasa, jeni kweli Mnyika ameponzwa na anatakiwa kufanya nini sasa ilikuonesha yupo tofauti na wabunge wa dar kupitia CCM katika kusimamia hoja?
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,356
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye red umefanya utafiti gani kujua?mnyika angekaa kimya angekuwa ameside na fisadi magufuli so nampa big up pamoja na hao wabunge wa ccm,..magufuli kashakatiwa mlungula pale kivukoni..pesa ilimuuza yesu bwana...
   
 3. t

  taja2020 New Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sidhani kama umeshafanya utafiti ya kinacholalamikiwa kazi kubwata bwata kwancho lalamikia ni ushirikishwaji sio nauli shykwanza
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Thread haina mashiko kabisa hii, na muanzishaji hajajaribu kabisa kujiweka nafasi ya wapanda feri!!...
   
 5. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,710
  Trophy Points: 280
  nilimsikiliza mbunge wa kigamboni asubuhi radio Clouds
  swala sio kupanda kwa nauli
  wanachosisitiza wanataka kujua mapato na matumizi
  kuweza kubainisha kama kivuko kinajiendesha kwa hasara au faida
  na wametumia kigezo gani kupandisha kuwa 200 na sio zaidi au pungufu


   
 6. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Hivi kati ya mnyika na hao wabunge wako ni nani anaweza kuwaponza wengine
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  masaburi at work
   
 8. n

  namimih Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpaka sasa nikifuatilia suala la nauli ya kigamboni naona kila mtu ameshikilia nauli ya 200, wanasahau suala la guta ambalo lina uhusiano mkubwa sana na mahitaji yanayouzwa huko kigamboni kila siku, kumbuka asilimia kubwa ya wananchi wa huko ni wateja wa reja reja wa bidhaa za kila siku na wanategemea soko na magenge ili kupata mahitaji yao.

  Sasa ukijumlisha 200 ya kwenda na kurudi, ongeza na hizo huduma zingine zitakavyopandishwa kufidia gharama ya kuvusha hapo kwenye pantoni utakuwa mada haibaki kwenye ongezeko la 100 tu, bali ni zaidi ya hiyo, hesabu ya kawaida ya kukisia, kama mtu anavusha watoto 3 kwenda shule anahitaji 300 na yeye 200, kwa watembeaji wa miguu, ukijumlisha na ongezeko la bidhaa za chakula ambayo hiyo haina mjadala kuwa haitopanda, kwahiyo tuangalieni kwa upana zaidi hiyo gharama iliyoongezwa na Dr.Makufuli.
   
 9. n

  namimih Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 10. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  nchi ishauzwa hii ni kwamba wanamalizia kugawana mabaki tu. nyie wazaramo wa dar kalaghabaho. Kila uchao magufuli anahangaika na ntoke vp yake sijui mwishowe utakuwa nini.
   
 11. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
   
 12. shungurui

  shungurui JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 1, 2008
  Messages: 1,577
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  kuna jamaa yangu amejenga nyumba yake kwa hela za hicho kivuko.
  Tatizo sio mapato madogo.
   
 13. e

  emike JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mimi nadhani kama kuna kuponzwa kitu ambacho siamini, basi wabunge wa ccm ndiyo walioponzwa.kumbuka kuwa mnyika yuko kwenye upinzani,na maada yao ilikuwa kupinga maamuzi ya waziri wa serikali ya chama tawala ccm ambayo ndiyo kazi hasaa ya opposition akiwepo mnyika.kwanza siyo maadili ya kiongozi sehemu yoyote duniani kutoa lugha ya kejeli au matusi kwa wanainchi aliwopewa dhamana ya kuwaongoza kama hiyo issue ya kupiga mbizi.pili temese wanapaswa kupeleka maombi ya kuongeza nauli kwenye mamlaka husika yaani sumatra kama tanesco wanavyo pitisha maombi yao ewura wananchi kupitia wawakilishi wao wangeshirikishwa kwa maamuzi hayo, tatu ilani ya uchaguzi ya magamba ilikuwa kujenga daraja kigamboni mh magufuli angefanyia kazi hilo badala kuanzisha mzozo wa nauli, mwisho siyo siri kuna ubadhirifu kwenye ukusanyaji wa mapato.
   
 14. kajwa

  kajwa Member

  #14
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani jimbo la ubungo ni kisiwa kwamba hawaingiliani kabisa na kigamboni?? labda mbunge wake asiingilie??
  Kwani mbona mnaongea mambo as if kigamboni ni kisiwa cha dar es salaam... wengine wanatuletea hadithi zao za vijijini kwao eti wao wanalipa mia 3....
  serikali ni lazima iingie gharama ya uzezeta wake wa kutokuweka daraja pale sababu kama kungekuwa na daraja hata nauli hiyo ya mia isingelipwa coz watu wangetembea tu.
   
 15. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,710
  Trophy Points: 280
   
 16. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,710
  Trophy Points: 280
  kutokana na tetesi mbunge alizopata kuna jamaa anasema kwa siku anapata 300,000/= za mfukoni sasa huyo ni mmoja, na taarifa alizonazo mapato ya kivuko kwa siku ni 13,000,000 na sio 8,000,000 kana alivyosema waziri.
   
 17. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hakuna umaarufu uliopungua toa data za kisayasi
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Labda pengine mimi sikumsoma vizuri Mnyika lakini nilichosoma ni kwamba Mnyika alipinga kauli ya Maguifuli kuwaambia wananchi kama hawataki kulipa wapige mbizi kuvuka... Sidhani kama alionyesha kukereka na kupanda kwa nauli toka Tsh 100 hadi tsh 200..
   
 19. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ushabiki kama huu wa kijinga na cheap politics ndio zimeleta maafa bonde la Msimbazi.
  Tumewaangalia watu wanajenga vibanda, baadaye zikawa nyumba nyumba na sasa umekuwa mji. Uliona wapi Duniani watu wanajenga nyumba mabondeni? Wenye pesa zao, wamehonga na kuruhisiwa kujenga magarage, petrol station na kuziba njia za maji. Kama unataka ushahidi nenda njia ya kigogo upande wa kushoto, kama unaelekea Msimbazi,

  Leo hii tunalipa gharama za ujinga wetu kwa vifo vya watu wanaosombwa na maji. Mvua zikisha, watarudi mabondeni na kama kawaida ya watznania, tutasahau hayo yote hadi next mafuriko.

  Thank you God kwa kuwa tunaishi kwenye nchi ambayo maisha ya raia hayana thamani, isingekuwa hivyo, tungeona mabadilliko.
   
 20. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kuna umuhimu wa kufanya utafiti kabla ya kutoa data za uongo.
   
Loading...