Je, ni kweli mitandao ya kijamii haina faida kwa maendeleao ya taifa?

Mtu mdogo

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
525
826
Binafsi nimesikitika sana baada ya boss wa nchi kusema kwamba tupige kazi na tuache maneno ya udaku wa kwenye mitandao.

Tujaribu kurejea kilicho tokea Brazil na Korea ya kusini;
BRAZIL
Wananchi waliweza kutumia mitandao ya kijamii kushinikiza rais wao bi Dilma Rousseff kujiuzulu kutokana na matumizi mabaya ya ofisi ya urais na hatimaye bunge likapiga kura ya kumuondoa madarakani, je ule ni udaku?

KOREA KUSINI
Wananchi walipata taarifa ya ufisadi alio ufanya bi Park Geune-hye kupitia mitandao ya kijamii na hatimaye wakashupaa hadi bunge likaingilia kati na kuungana na wananchi hatimaye wakamvua madaraka.

Je isingekuwa mitandao ya kijamii wananchi wangewezaje kuelezea malalamiko yao. Kwahiyo tukiona mtu anapinga mitandao ya kijamii kwamba ni udaku tu hiyo ni defence mechanism anajiwekea na wananchi vilaza wata msapoti.
 
Back
Top Bottom