Je ni kweli mbegu za kisasa zinatumika kueneza magonjwa ya mazao?

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
4,333
2,000
1. Miaka ya 1995 baadhi ya watu walianza kusema kuwa hizi hybrid seeds zinashambuliwa sana na magonja kuliko mbegu za asili.
2. Miaka ya hivi karibuni wadudu wanaoshambulia mazao wamekuwa tishio, hata kwa mazao ambayo miaka ya nyuma hayakuwa yakishambuliwa na wadudu. Kwa mfano mahindi.
3. Wakukima wengi wanaamini hizi mbegu za kisasa zimechangia kueneza wadudu, au ni dhaifu sana dhidi ya wadudu.
4. Je wataalamu wa mbegu na kilimo kwa ujumla mna majibu gani?
 

CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,741
2,000
Hizo taarifa sio za kweli. Mbegu za hybrid zinazalishwa zikiwa na sifa za kuhimili baadhi ya magonjwa/wadudu, kuhimili ukame,kuzaa vizuri kwenye idongo wa rutuba hafifu,nk Na hufanyiwa majaribio katika maeneo tofauti tofauti na kwa misimu tofauti ili kujiridhisha kitaalam kuhusu sifa ilizo nazo kabla haijatangazwa rasmi kuwa ni mbegu bora.
Tatizo la wadudu waliojitokeza toka msimu uliopita ni suala tofauti na dhana potofu walio nayo baadhi ya wakulima. Kuna tatizo la viwavi jeshi toka bara la Amerika ambavyo vinaitwa Fall army worms. Ni wadudu wageni kabisa hapa Africa na waliathiri nchi mbali bali za Afrika zikiwemo Zimbabwe, Malawi, Zambia, Nigeria,nk.
Hawa wadudu ni wagumu kuua na ni dawa chache sans zinazoweza kuwaua. Dawa zenye kiambata (active ingredient) cha Cypermethrin+ mfano DUDU ALL, DUDUBA nk ndizo zenye uwezo wa kudhibiyi hawa wadudu. Dawa hizi ni ghali na sio nyingi. Jinsi ya kuwatambua fall army worms njia rahisi mi kitafuta huyo kiwavi na kumchinguza kichwa chake. Kina mistari 3 inayotengeneza umbo la Y iliyogeuzwa chini juu. Ukimtambua ni yeye dawa ndio hizo. Sio lazima wawe wengi kuna mashamba mengine unakuta no mimea michache tu iliyoshambuliwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom