Je, ni kweli mabaharia wenye seaman book wanasafiri bila Visa?

lodirofaa

Member
Jul 6, 2021
25
62
Ndugu zangu nilikuwa nahitaji kufahamu je ni kweli wale mabaharia wanaomiliki seaman book huwa wanaingia nchi yoyote bila visa?

Nia yangu nijue.
 
Hapana...huu utaratibu ulikuwa zamani kwa sasa hautumiki tena..
 
Mabaharia wenye seaman book wakiingia nchi ambayo wanalipishana Visa atatakiwa kulipa Visa, kama atakuwa anapita tu au anaingia kuona mji endapo meli yao imetia nanga kwa ajili ya kushusha mzigo au kupakia atatakiwa kulipa Transit Visa mara nyingi huwa ni dola au uero 30.

Vinginevyo akibaki ndani ya meli anaweza kuzunguka nchi zote zilizopakana na bahari bila ya kulipa, cha msingi abakie melini tu.
 
Back
Top Bottom