Je, ni kweli maambukizi ya COVID-19 yamepungua nchini au ni propaganda tu?

Tunaowajua mpaka hivi sasa walitambuliwa vp! Sio kwa kupimwa? Na unaposema serikali ipime watu wote una maana gani? Hivi inawezekana? Naweza kupata mfano wa nchi hasa ya ulimwengu wa kwanza iliyokwisha pima raia wote.

Waliosema kuwa vitendea kazi vya kupimia havifai ni nani? Sasa hao mnaosema mmewatambua mmewatambuaje kwa kutumia NYUNGU? Mbona hamsemi kuwa mnavitendea kazi vya uhakika sasa na ndio maana hata mtoto wa JPM akagundulika na corona!!

Tunaposema kuwapima wananchi wote ni figurative pengine hilo huelewi ; lakini ukiwapima wananchi wa kutosha hapo tunaweza kusema kuna jitihada za kuzuia kuenea kwa ugonjwa na hiyo ndio sababu ya kuwapima watu ili uweze kuwafuatilia wale ambao wanaweza kuwa na maambukizi.

Sasa sisi tunafukia kichwa chetu kama mbuni kwenye mchanga na kuwalisha wananchi matango pori a' la Makonda kuwa corona imekwisha na watu waache hata kuvaa barakoa!!! Kutokuwapima representative sample ya population yetu ndio kunaifanya serikali kutotoa takwimu sahii za ugonjwa huu na hasa kuhusu idadi ya wananchi waliokwisha kupimwa nchi nzima!!!!
 
Nakumbuka Jumapili Rais alisema maambukizi yamepungua nchini ya covid 19

Kuna maswali ya msingi ya kujiuliza.

Je, maabara baada ya kutuambiwa inatatizo isharekebishwa lini?
Je, ni lini ilianza kupima wagonjwa wapya wa covid 19?
Je, kama nzima mbona takwimu hazitolewi za wagonjwa wapya na waliopona?
Je, takwimu za Rais za wagonjwa alionao ni baada ya mashine kupona au la?
Je, mashine iliyotumika mtoto wake alipimwa kwa mashine zipi au hiyo hiyo aliyoishutumu?
Je, vituo alivyotaja rais ndivyo vilivyopo nchi nzima vya wagonjwa wa vovid19?
Je, kwanini madereva tuambiwe wanakorona ikiwa nchini maambukizi yamepunguwa?
Ni kweli wamepungua sijakutana na watu wanokohoa njiani. Ndiyo kipimo no 1.
 
Don’t listen to any fool who says COVID-19 cases are waning in Tanzania, Hali ni mbaya. Niishie hapo, wanaojitambua watanielewa
 
mwisho wa siku tupo huru na corona.
Japo kuna hawakupenda tunawapa pole itabidi wazoee
 
Kwangu Mimi binafsi mtaani kwetu KWA ujumla sijaona MTU aliyekufa KWA korona wala taarifa ya mgonjwa WA korona. Sasa nikiacha siasa korona hakuna. Lkn kama nikilitea siasa zangu korona imetapakaa jomba kila mahali wtu wanakufaa ati.
 
Kwangu Mimi binafsi mtaani kwetu KWA ujumla sijaona MTU aliyekufa KWA korona wala taarifa ya mgonjwa WA korona. Sasa nikiacha siasa korona hakuna. Lkn kama nikilitea siasa zangu korona imetapakaa jomba kila mahali wtu wanakufaa ati.
😀😆😀
 
Sio rahisi kujua kwa sababu Watanzania ni watu wasiopenda kufanya utafiti wanaropoka tuu hata vitu wasivyojua, wengine wanasema Hospital zimejaa, seriously ni lini Hospital za Tanzania zilikuwaga wazi, mmesahau issue za wagonjwa kushare vitanda, wagonjwa kulala kwenye floor nk nk.
Ili kujua ukweli nadhani tungeanzia ktk circle ya familia tujue kuna wagonjwa na waliokufa wangapi halafu tuangalie cycle ya jamaa na marafiki kuna wagonjwa na waliokufa wangapi kwa muono wangu hii itatupa rough picture ya huu ugonjwa maana wataalam wetu bado wako shuleni hawajafuzu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi ktk familia yetu na watu wa karibu tunashukuru mungu mpaka sasa hatuna aliyepoteza maisha kwa ugonjwa huu au unaosadikika kuwa corona, ila kuna watu kadhaa wamepata mshike mshike kidogo lkn wote walipona na wanaendelea vizuri na gurudumu la maendeleo.
Kinachonisikisha ni kila aliyeenda hospital alikutwa either na typhoid au UTI na wachache malaria, sasa sijui shida ni vipimo au ????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom