Je ni kweli Leviathan yupo hapa duniani? Sehemu ya 1

Habarini za ijumaa wakuu. Natumaini mpo salama sana poleni kwa mihangaiko. Naomba niletee kwenu Uzi huu kuhusu huyu kiumbe ambaye nimeanza kumsikia kwenye biblia mpaka baadhi ya mitandao ya habark tofauti tofauti duniani.
Kiumbe Huyu anaitwa Leviathan. Nimejaribu kufuatilia kidogo kuhusu huyu kiumbe nimeshtuka na kuamua nije tujadili ndani huku maana JF ndo jukwaa huru la kifikria.
Karibuni.
Leviathan ni mnyama wa baharini ambaye amezungumzwa sana katika vitabu mbalimbali vya dini mfano: kitabu cha Ayubu, kitabu cha Isaya, pamoja na Zaburi bila kusahau Kitabu cha Amos. Mnyama huyu kazungumwa sana katika imani mbili nazo ni Wahebrania pamoja na na Wayahudi.

Katika kitabu cha Ayubu 3:8, na Ayubu 40:15, Ayubu 41:25, Zaburi 74:13-23, Zaburi 104:26 pamoja na Isaya 27:1. Ndani ya vitabu hivi kiumbe huyu anaonyesha sana. Mfano tu Ayubu 41:1-8 inasema "1 Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana?Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?
2 Je! Waweza kutia kamba puani mwake?Au kutoboa taya yake kwa kulabu?
3 Je! Atakusihi sana?Au, atakuambia maneno ya upole?
4 Je! Atafanya agano pamoja nawe,Umtwae kuwa mtumishi wako milele?
5 Je! Utamchezea kama ndege?Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako?
6 Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara?Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?
7 Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha,Au kichwa chake kwa vyusa?
8 Mwekee mkono wako;Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena."
Lakini Ndani ya sura hii ya kitabu cha Ayubu imeeleza kiumbe ambaye kwa sifa hizo sio kiumbe cha kawaida.
Lakini pia Zaburi ya 104:25-26 inasema "25 Bahari iko kule, kubwa na upana,Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika,Viumbe hai vidogo kwa vikubwa.
26 Ndimo zipitamo merikebu,Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo." Lakini pia kwenye Isaya 27:1 inasema"Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini."
Kutajwa kwa Leviathan ndani ya Vitabu hivi hasa hasa Zaburi inaonyesha kuwa huyu kiumbe sio wenye madhara na ni kama viumbe wengine wa bahari na kujumuishwa kama viumbe vya Mungu tu.
Kwa upande wa Wayahudi kupitia kitabu cha Tanak wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu aliumba Leviathan wawili yaani Leviathan wa kiume na wakike. Lakini aliona kuwa kutokana na asili yao na namna ya uumbaji wao akamfanya jike kutokuonana na Dume yaani kutokuingiliana kwa hofu ya kuzaliana Leviathan wengine. Hivyo alimuulia mbali Leviathan jike na kumuacha Leviathan dume. Lakini baadaye tena wazee wa dini walikuja na tafsiri mpya kuhusu Leviathan. Kwamba Leviathan ni dragoni ambaye anaishi kwenye vyanzo vya chini kabsa vya bahari ambapo huishi huko pamoja na Mnyama mwingine dume anayeitwa Behemoth. Kitabu cha Enock kinaelezea vyema sana huyu Leviathan Jike kuwa huyu Leviathan jike anaishi eneo linaloitwa Tiamat huku dume akiwa kwenye jangwa la Dunaydin (mashariki kwa Eden)
Kwa upande wa Wayuda (Judaism):
Kupitia maandiko kutoka katika Talmud Baba Bathra kuanzia aya ya 75 inasema "Halo ndipo Leviathan atakapochinjwa na nyama yake kufanya kitoweo kwa wale mwenye haki mbele ya Mungu wakati wa Messiah atakaporudi. Ngozi yake itafanyishwa tent mahali ambapo tukio hili litafanyika. Ndani ya Talmud Baba Bathra imeeleza vitu vyenye usawa na Zaburi pamoja na Ayubu.

Johanan Bar Nappaha ni Rabbi aliyeeleza visa vingi sana kuanzia Babilonia pamoja na Mesopotamia. Alidai kuwa ukubwa wa Leviathan ni kati ya viumbe walio na ukubwa wa kutisha sana. Aliweza kufikisha mpaka maili zaidi ya mia 2 kwa urefu na upana zaidi ya mita 40. Kutokana na maneno ya Mwanazuoni huyu alidai Leviathan akikasirika basi joto lake linatosha kuchemsha maji ya bahari. (Ni ajabu eehh). Na akiachama mdomo wake basi hakuna mtu anayeweza kustahimilihi harufu ya kinywa chake.
Kichwa chake kinadaiwa kipo Bahari ya Mediterranean na maji ya Maporomoko ya Jordan yanaingia ndani ya mdomo wake.
Katika moja ya hadithi za zamani sana za Wayahudi inayoitwa Pirke de-Rabbi Eliezer inazungumzia kisa cha Nabii Yona aliyepewa maagizo ya kuelekea ninawi kuhubiri injili lakini akasepa kwa kutorokea ndani ya boti ambayo mwisho wa siku ilikumbwa na dhoruba kubwa na kuepelekea Yona kutupwa ili wengine waokoke na dhoruba hiyo. LAKINI tofauti na kwenye Biblia, humu ndani kisa hiki kinasema kuwa yule samaki aliyetumwa kumumeza Yona alipata kashi kashi kwani alikoswakoswa kuwa msosi wa Leviathan, kwani inaelezwa kuwa Leviathan hupata msosi wa Nyangumi mmoja kwa siku kama mlo wake.

Katika karne ya 11 shairi la Kidini linaloitwa Akdamut linarudia maneno ya kwenye Biblia kuwa Leviathan atachinjwa na Mwenyezi Mungu na nyama yake kufanywa kitoweo kwa wale wenye haki tu.
Kwa upande wa Wakikristo.
Madhehebu ya kikristo wanatumia sana Leviathan kama Shetani tu. Kwani hufanya uharibifu kwa viumbe vya Mungu. Mtakatifu Thomas Aquinas alimdadavua Leviathan kama jini la wivu. Na kama mmoja kati ya Wale Maprince Saba wa Kuzimu kumaanisha dhambi saba mbaya zaidi.

Leviathan anahusishwa sana na Hellmouth mwenye mdomo mkubwa sana na atakayechinjwa pia mwisho wa kiama. Ni kiumbe ambaye anapatikana katika nyaraka za kisanaa za Anglo-saxon za mwaka wa 800.

Dini za kishetani hazipo nyuma:
Bwana Anton Szandor LaVey kwenye Biblia yake ya mwaka wa 1969 anampamba Leviathan kama kiwakilishi cha maji na mwenye uelekeo wa magharibi. Pia Bwana Anton anadai na kuunga mkono kuwa Leviathan ni kati ya wana wa falme ya kuzimu ila anasema kuwa ni wapo wanne tu na sio saba. Kazi ya bwana huyu ilichochewa sana na maandiko ya kishentani kutoka katika kitabu cha The book of the Sacred Magic of Abra-Melin the Mage. Kanisa hili hutumia vizuri sana alama za Sigil za Baphomet kumuwakilisha Leviathan. Wanaanzia kwenye pointi ndogo kabsa ya Pentagram na
Abra-Melin the Mage . The
Church of Satan uses the Hebrew letters at each of the points of the Sigil of Baphomet to represent Leviathan. Starting from the lowest point of the Pentagram hivyo kufanya neno Leviathan kuwa " לויתן": kwa kihebrania.

Hiyo ni kwa leo sehemu ya kwanza. Maana mambo ni mengi sana nikipata muda na afya nitamaliza sehemu ya pili na ya tatu ya mada hii.
Asante sana wakuu kwa muda wenu.
Nakaribisha marekebisho,maswali, mijadala na mengine mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Weka picha sasa
Ni asilimia 4 tu ya tunayo yafahamu katika ulimwengu huu.
Joka lenye kuzongazonga
Mambo ni mengi ulimwengu huu.
maneno ya Mwanazuoni huyu alidai Leviathan akikasirika basi joto lake linatosha kuchemsha maji ya bahari. (Ni ajabu eehh). Na akiachama mdomo wake basi hakuna mtu anayeweza kustahimilihi harufu ya kinywa chake.
na maji ya Maporomoko ya Jordan yanaingia ndani ya mdomo wake.
akipanua kinywa hakuna atakaye stahimili harufu. Wakati huohuo kinywa chake kipo wazi na maporomoko ya Jordan yanaingia humo
ukubwa wote huo tusiweze kupata hata picha yake na kwakuzingatia teknolojia iliyopo sasa?
Stori ya kufikirika.
Mmh kama yupo kwel basi ni noma sana
Ndio pale ninapo hitimisha kuwa kweli nipo sahihi juu ya fikra zangu kuhusiana na hivi vitabu vya dini kuwa ni visasili na ngano za watu wa kale.

Mbona hizo picha zote hapo juu sio halisi ni animation & picha za kuchora tu.
Story kama story zingine
Naweza sema,hawa ni Viumbe wa rohoni zaidi..
Wapo lakini katika,ulimwengu mwingine usioonekana!!

Biblia ina tufunulia vitu vingi,lakini c kila kitu kwenye bible kipo mwilini hapana
Vingine n kwamba vipo rohoni,
Yapo masimulizi kwenye bible yana kosa maana/uhalisia wa Ki,Mwili coz ni Masimulizi/Habari za kiroho!

Laiti wanadamu wote,tungeweza kuishi rohoni na Mwilini basi siri na mambo mengi yangekuwa wazi kwetu!!!

Kinachofanyika na wajanja wachache Zama hizi,ni kutohoa mambo ya rohoni na kuyaleta katika ulimwengu unao onekana!!

Leo hii Tunapowaangalia Nchi za dunia Ya 1,watakuja na taarabuu nyingi na jinsi ya kujikwamua na kutoka kwenye umasikini,Lakini Jiulize Mbona huo Umasikini bado hatutoki?
(Hapa watu wataleta porojo na Facts zilizotengenezwa na wao).

Wamekuwa wanatutolea kafara/sadaka kwa kivuli cha misaada!
Je,tangu watutolee hadi leo bado tu hatujaweza kujikwamua?
Na kwanini hawachoki kututolea?

Na kumekuwa na usiri mkubwa hili watu wasielewe lolote wala kufahamu!!

Wamekuwa wanatoa Information/habari ambazo wao wanataka uzijue/kuzisikia
Ni kwamba Wengi wapo kwenye Magereza ya Fikra na bahati mbaya hawajafanikiwa kutoka na kuona jinsi ulimwengu ulivyo!!

Ni kama mtu ambaye tangu kuzaliwa,yupo ndani ya pango,yule mtu anaweza fikiri ndani ya lile pango na kuona kila
kitu kipo hivyo bt ikitokea akaja kutoka huko
Atashangaa na kustaajabu ya ulimwengu wa Nje ya pango..
Ndivyo Ambavyo Tunaishi na Dunia ni Zaidi ya Pango,Tukitoka Nje tutajua Mengi na Energy inayo
Tu Endesha+Nguvu zetu za Mwilini na Rohoni
 
Habarini za ijumaa wakuu. Natumaini mpo salama sana poleni kwa mihangaiko. Naomba niletee kwenu Uzi huu kuhusu huyu kiumbe ambaye nimeanza kumsikia kwenye biblia mpaka baadhi ya mitandao ya habark tofauti tofauti duniani.
Kiumbe Huyu anaitwa Leviathan. Nimejaribu kufuatilia kidogo kuhusu huyu kiumbe nimeshtuka na kuamua nije tujadili ndani huku maana JF ndo jukwaa huru la kifikria.
Karibuni.
Leviathan ni mnyama wa baharini ambaye amezungumzwa sana katika vitabu mbalimbali vya dini mfano: kitabu cha Ayubu, kitabu cha Isaya, pamoja na Zaburi bila kusahau Kitabu cha Amos. Mnyama huyu kazungumwa sana katika imani mbili nazo ni Wahebrania pamoja na na Wayahudi.

Katika kitabu cha Ayubu 3:8, na Ayubu 40:15, Ayubu 41:25, Zaburi 74:13-23, Zaburi 104:26 pamoja na Isaya 27:1. Ndani ya vitabu hivi kiumbe huyu anaonyesha sana. Mfano tu Ayubu 41:1-8 inasema "1 Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana?Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?
2 Je! Waweza kutia kamba puani mwake?Au kutoboa taya yake kwa kulabu?
3 Je! Atakusihi sana?Au, atakuambia maneno ya upole?
4 Je! Atafanya agano pamoja nawe,Umtwae kuwa mtumishi wako milele?
5 Je! Utamchezea kama ndege?Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako?
6 Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara?Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?
7 Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha,Au kichwa chake kwa vyusa?
8 Mwekee mkono wako;Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena."
Lakini Ndani ya sura hii ya kitabu cha Ayubu imeeleza kiumbe ambaye kwa sifa hizo sio kiumbe cha kawaida.
Lakini pia Zaburi ya 104:25-26 inasema "25 Bahari iko kule, kubwa na upana,Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika,Viumbe hai vidogo kwa vikubwa.
26 Ndimo zipitamo merikebu,Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo." Lakini pia kwenye Isaya 27:1 inasema"Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini."
Kutajwa kwa Leviathan ndani ya Vitabu hivi hasa hasa Zaburi inaonyesha kuwa huyu kiumbe sio wenye madhara na ni kama viumbe wengine wa bahari na kujumuishwa kama viumbe vya Mungu tu.
Kwa upande wa Wayahudi kupitia kitabu cha Tanak wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu aliumba Leviathan wawili yaani Leviathan wa kiume na wakike. Lakini aliona kuwa kutokana na asili yao na namna ya uumbaji wao akamfanya jike kutokuonana na Dume yaani kutokuingiliana kwa hofu ya kuzaliana Leviathan wengine. Hivyo alimuulia mbali Leviathan jike na kumuacha Leviathan dume. Lakini baadaye tena wazee wa dini walikuja na tafsiri mpya kuhusu Leviathan. Kwamba Leviathan ni dragoni ambaye anaishi kwenye vyanzo vya chini kabsa vya bahari ambapo huishi huko pamoja na Mnyama mwingine dume anayeitwa Behemoth. Kitabu cha Enock kinaelezea vyema sana huyu Leviathan Jike kuwa huyu Leviathan jike anaishi eneo linaloitwa Tiamat huku dume akiwa kwenye jangwa la Dunaydin (mashariki kwa Eden)
Kwa upande wa Wayuda (Judaism):
Kupitia maandiko kutoka katika Talmud Baba Bathra kuanzia aya ya 75 inasema "Halo ndipo Leviathan atakapochinjwa na nyama yake kufanya kitoweo kwa wale mwenye haki mbele ya Mungu wakati wa Messiah atakaporudi. Ngozi yake itafanyishwa tent mahali ambapo tukio hili litafanyika. Ndani ya Talmud Baba Bathra imeeleza vitu vyenye usawa na Zaburi pamoja na Ayubu.

Johanan Bar Nappaha ni Rabbi aliyeeleza visa vingi sana kuanzia Babilonia pamoja na Mesopotamia. Alidai kuwa ukubwa wa Leviathan ni kati ya viumbe walio na ukubwa wa kutisha sana. Aliweza kufikisha mpaka maili zaidi ya mia 2 kwa urefu na upana zaidi ya mita 40. Kutokana na maneno ya Mwanazuoni huyu alidai Leviathan akikasirika basi joto lake linatosha kuchemsha maji ya bahari. (Ni ajabu eehh). Na akiachama mdomo wake basi hakuna mtu anayeweza kustahimilihi harufu ya kinywa chake.
Kichwa chake kinadaiwa kipo Bahari ya Mediterranean na maji ya Maporomoko ya Jordan yanaingia ndani ya mdomo wake.
Katika moja ya hadithi za zamani sana za Wayahudi inayoitwa Pirke de-Rabbi Eliezer inazungumzia kisa cha Nabii Yona aliyepewa maagizo ya kuelekea ninawi kuhubiri injili lakini akasepa kwa kutorokea ndani ya boti ambayo mwisho wa siku ilikumbwa na dhoruba kubwa na kuepelekea Yona kutupwa ili wengine waokoke na dhoruba hiyo. LAKINI tofauti na kwenye Biblia, humu ndani kisa hiki kinasema kuwa yule samaki aliyetumwa kumumeza Yona alipata kashi kashi kwani alikoswakoswa kuwa msosi wa Leviathan, kwani inaelezwa kuwa Leviathan hupata msosi wa Nyangumi mmoja kwa siku kama mlo wake.

Katika karne ya 11 shairi la Kidini linaloitwa Akdamut linarudia maneno ya kwenye Biblia kuwa Leviathan atachinjwa na Mwenyezi Mungu na nyama yake kufanywa kitoweo kwa wale wenye haki tu.
Kwa upande wa Wakikristo.
Madhehebu ya kikristo wanatumia sana Leviathan kama Shetani tu. Kwani hufanya uharibifu kwa viumbe vya Mungu. Mtakatifu Thomas Aquinas alimdadavua Leviathan kama jini la wivu. Na kama mmoja kati ya Wale Maprince Saba wa Kuzimu kumaanisha dhambi saba mbaya zaidi.

Leviathan anahusishwa sana na Hellmouth mwenye mdomo mkubwa sana na atakayechinjwa pia mwisho wa kiama. Ni kiumbe ambaye anapatikana katika nyaraka za kisanaa za Anglo-saxon za mwaka wa 800.

Dini za kishetani hazipo nyuma:
Bwana Anton Szandor LaVey kwenye Biblia yake ya mwaka wa 1969 anampamba Leviathan kama kiwakilishi cha maji na mwenye uelekeo wa magharibi. Pia Bwana Anton anadai na kuunga mkono kuwa Leviathan ni kati ya wana wa falme ya kuzimu ila anasema kuwa ni wapo wanne tu na sio saba. Kazi ya bwana huyu ilichochewa sana na maandiko ya kishentani kutoka katika kitabu cha The book of the Sacred Magic of Abra-Melin the Mage. Kanisa hili hutumia vizuri sana alama za Sigil za Baphomet kumuwakilisha Leviathan. Wanaanzia kwenye pointi ndogo kabsa ya Pentagram na
Abra-Melin the Mage . The
Church of Satan uses the Hebrew letters at each of the points of the Sigil of Baphomet to represent Leviathan. Starting from the lowest point of the Pentagram hivyo kufanya neno Leviathan kuwa " לויתן": kwa kihebrania.

Hiyo ni kwa leo sehemu ya kwanza. Maana mambo ni mengi sana nikipata muda na afya nitamaliza sehemu ya pili na ya tatu ya mada hii.
Asante sana wakuu kwa muda wenu.
Nakaribisha marekebisho,maswali, mijadala na mengine mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Leviathan ni kiumbe kilichokua kimepewa nguvu ya kutawala baharini na behemoth ni kiumbe kilichokua kimepewa nguvu ya kutawala nchi kavu,ila vilikuja vikamuasi Mungu,shetani alipotupwa duniani vikaasi vikaungana na shetani.vipo!..
 
Ukweli ni kwamba ,kuna viumbe vingi sana vilikuwepo hapa duniani ambavyo kwa sasa havipo, na hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa na shughuri za binadamu zinazopelekea viumbe hawa kutokuweza kukabiliana na mazingira ya kuishi.

Miaka ya zamani walikuwepo wanyama wakubwa zaidi ya tembo, ila leo tunaona tembo ndo mkubwa, na kadri siku zinavyoenda huenda tembo nae akabaki katika historia tu.

Kushindwa kupata picha kamili za hao viumbe inatokana na technologia ya wakati huo na hivyo haya mambo yakabaki kama nadharia tu. Zamani watu walikuwa wakiona vitu vingi na wanahifadhi picha ya hayo matukio ama vitu katika vichwa vyao, na wengine waliweza kuchora katika mawe au katika magome ya miti.

Kama tunavyojua, dunia haijaanza leo, kuna mamilioni ya miaka imepita hivyo kumbu kumbu hizi si rahisi kuzipata wala mabaki ya hao viumbe. Imebaki kama historia tu isiyo na ushaidi ila kikawaida hao viumbe waliweza kutokea hapa duniani mana hata sasa kuna viumbe ambao bado ukiwatazama utashangaa,

Pia kuna nadharia moja inasema kuna viumbe walikuwepo hapa duniani ambao walikuwa ni hatari zaidi ya simba ama chui ama tembo, na hao waliteketezwa kwa utashi wa Mungu tu, kwani mwanadamu hakuwa na uwezo kwa kuwa control, hivyo walijifia bila sababu maalumu na hatimae kupotea kabisa katika uso huu wa dunia.

Nazani kila jambo unalolisika hapa duniani lilikuwepo, ila kutokana na wingi wa miaka unaweza kuzani ni story tu,ila mambo mengi yalikuwepo kabla ya uwepo wetu sisi, mimi na wewe.
 
Habarini za ijumaa wakuu. Natumaini mpo salama sana poleni kwa mihangaiko. Naomba niletee kwenu Uzi huu kuhusu huyu kiumbe ambaye nimeanza kumsikia kwenye biblia mpaka baadhi ya mitandao ya habark tofauti tofauti duniani.
Kiumbe Huyu anaitwa Leviathan. Nimejaribu kufuatilia kidogo kuhusu huyu kiumbe nimeshtuka na kuamua nije tujadili ndani huku maana JF ndo jukwaa huru la kifikria.
Karibuni.
Leviathan ni mnyama wa baharini ambaye amezungumzwa sana katika vitabu mbalimbali vya dini mfano: kitabu cha Ayubu, kitabu cha Isaya, pamoja na Zaburi bila kusahau Kitabu cha Amos. Mnyama huyu kazungumwa sana katika imani mbili nazo ni Wahebrania pamoja na na Wayahudi.

Katika kitabu cha Ayubu 3:8, na Ayubu 40:15, Ayubu 41:25, Zaburi 74:13-23, Zaburi 104:26 pamoja na Isaya 27:1. Ndani ya vitabu hivi kiumbe huyu anaonyesha sana. Mfano tu Ayubu 41:1-8 inasema "1 Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana?Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?
2 Je! Waweza kutia kamba puani mwake?Au kutoboa taya yake kwa kulabu?
3 Je! Atakusihi sana?Au, atakuambia maneno ya upole?
4 Je! Atafanya agano pamoja nawe,Umtwae kuwa mtumishi wako milele?
5 Je! Utamchezea kama ndege?Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako?
6 Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara?Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?
7 Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha,Au kichwa chake kwa vyusa?
8 Mwekee mkono wako;Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena."
Lakini Ndani ya sura hii ya kitabu cha Ayubu imeeleza kiumbe ambaye kwa sifa hizo sio kiumbe cha kawaida.
Lakini pia Zaburi ya 104:25-26 inasema "25 Bahari iko kule, kubwa na upana,Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika,Viumbe hai vidogo kwa vikubwa.
26 Ndimo zipitamo merikebu,Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo." Lakini pia kwenye Isaya 27:1 inasema"Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini."
Kutajwa kwa Leviathan ndani ya Vitabu hivi hasa hasa Zaburi inaonyesha kuwa huyu kiumbe sio wenye madhara na ni kama viumbe wengine wa bahari na kujumuishwa kama viumbe vya Mungu tu.
Kwa upande wa Wayahudi kupitia kitabu cha Tanak wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu aliumba Leviathan wawili yaani Leviathan wa kiume na wakike. Lakini aliona kuwa kutokana na asili yao na namna ya uumbaji wao akamfanya jike kutokuonana na Dume yaani kutokuingiliana kwa hofu ya kuzaliana Leviathan wengine. Hivyo alimuulia mbali Leviathan jike na kumuacha Leviathan dume. Lakini baadaye tena wazee wa dini walikuja na tafsiri mpya kuhusu Leviathan. Kwamba Leviathan ni dragoni ambaye anaishi kwenye vyanzo vya chini kabsa vya bahari ambapo huishi huko pamoja na Mnyama mwingine dume anayeitwa Behemoth. Kitabu cha Enock kinaelezea vyema sana huyu Leviathan Jike kuwa huyu Leviathan jike anaishi eneo linaloitwa Tiamat huku dume akiwa kwenye jangwa la Dunaydin (mashariki kwa Eden)
Kwa upande wa Wayuda (Judaism):
Kupitia maandiko kutoka katika Talmud Baba Bathra kuanzia aya ya 75 inasema "Halo ndipo Leviathan atakapochinjwa na nyama yake kufanya kitoweo kwa wale mwenye haki mbele ya Mungu wakati wa Messiah atakaporudi. Ngozi yake itafanyishwa tent mahali ambapo tukio hili litafanyika. Ndani ya Talmud Baba Bathra imeeleza vitu vyenye usawa na Zaburi pamoja na Ayubu.

Johanan Bar Nappaha ni Rabbi aliyeeleza visa vingi sana kuanzia Babilonia pamoja na Mesopotamia. Alidai kuwa ukubwa wa Leviathan ni kati ya viumbe walio na ukubwa wa kutisha sana. Aliweza kufikisha mpaka maili zaidi ya mia 2 kwa urefu na upana zaidi ya mita 40. Kutokana na maneno ya Mwanazuoni huyu alidai Leviathan akikasirika basi joto lake linatosha kuchemsha maji ya bahari. (Ni ajabu eehh). Na akiachama mdomo wake basi hakuna mtu anayeweza kustahimilihi harufu ya kinywa chake.
Kichwa chake kinadaiwa kipo Bahari ya Mediterranean na maji ya Maporomoko ya Jordan yanaingia ndani ya mdomo wake.
Katika moja ya hadithi za zamani sana za Wayahudi inayoitwa Pirke de-Rabbi Eliezer inazungumzia kisa cha Nabii Yona aliyepewa maagizo ya kuelekea ninawi kuhubiri injili lakini akasepa kwa kutorokea ndani ya boti ambayo mwisho wa siku ilikumbwa na dhoruba kubwa na kuepelekea Yona kutupwa ili wengine waokoke na dhoruba hiyo. LAKINI tofauti na kwenye Biblia, humu ndani kisa hiki kinasema kuwa yule samaki aliyetumwa kumumeza Yona alipata kashi kashi kwani alikoswakoswa kuwa msosi wa Leviathan, kwani inaelezwa kuwa Leviathan hupata msosi wa Nyangumi mmoja kwa siku kama mlo wake.

Katika karne ya 11 shairi la Kidini linaloitwa Akdamut linarudia maneno ya kwenye Biblia kuwa Leviathan atachinjwa na Mwenyezi Mungu na nyama yake kufanywa kitoweo kwa wale wenye haki tu.
Kwa upande wa Wakikristo.
Madhehebu ya kikristo wanatumia sana Leviathan kama Shetani tu. Kwani hufanya uharibifu kwa viumbe vya Mungu. Mtakatifu Thomas Aquinas alimdadavua Leviathan kama jini la wivu. Na kama mmoja kati ya Wale Maprince Saba wa Kuzimu kumaanisha dhambi saba mbaya zaidi.

Leviathan anahusishwa sana na Hellmouth mwenye mdomo mkubwa sana na atakayechinjwa pia mwisho wa kiama. Ni kiumbe ambaye anapatikana katika nyaraka za kisanaa za Anglo-saxon za mwaka wa 800.

Dini za kishetani hazipo nyuma:
Bwana Anton Szandor LaVey kwenye Biblia yake ya mwaka wa 1969 anampamba Leviathan kama kiwakilishi cha maji na mwenye uelekeo wa magharibi. Pia Bwana Anton anadai na kuunga mkono kuwa Leviathan ni kati ya wana wa falme ya kuzimu ila anasema kuwa ni wapo wanne tu na sio saba. Kazi ya bwana huyu ilichochewa sana na maandiko ya kishentani kutoka katika kitabu cha The book of the Sacred Magic of Abra-Melin the Mage. Kanisa hili hutumia vizuri sana alama za Sigil za Baphomet kumuwakilisha Leviathan. Wanaanzia kwenye pointi ndogo kabsa ya Pentagram na
Abra-Melin the Mage . The
Church of Satan uses the Hebrew letters at each of the points of the Sigil of Baphomet to represent Leviathan. Starting from the lowest point of the Pentagram hivyo kufanya neno Leviathan kuwa " לויתן": kwa kihebrania.

Hiyo ni kwa leo sehemu ya kwanza. Maana mambo ni mengi sana nikipata muda na afya nitamaliza sehemu ya pili na ya tatu ya mada hii.
Asante sana wakuu kwa muda wenu.
Nakaribisha marekebisho,maswali, mijadala na mengine mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
thanks mkuu
 
zitto junior anayajua sana Mythology!..
🤣🤣 naona wantupia zigo la lawama! Ina maana bible ni mythology?? Naona una utani na wafia dini.

Mkuu nilikuitaga huku sijui kama ulipita maana kuna hadi farasi mtu wapo kwenye Bible!!

Cc Damaso
 
Siku hizi tag hazifanyi kazi kabisa, unakuwa tagged lakini hupati notification..

Biblia bana ni kitabu kimoja amazing!:D
 
Sasa kaka hizi picha si za kubuni mzee ?Vipi tuamini kama kweli huu ndio muonekano wake ?

Unaweza kututhubitishia kwamba ndio huyo kweli ?
Asante sana mkuu kwa dukuduku lako. Naomba kukujibu kuwa picha halisi za hawa viumbe hazipo na kilichobaki ni kuzichora kutokana na fasili ya maandiko tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom