Je, ni kweli kwamba ulaji papai kuzidi kawaida huhatarisha nguvu za kiume?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Kuna hoja kwamba papai lina nguvu sana

Papai huweza kulainisha nyama ili iive kwa haraka na ina uwezo mkubwa kulainisha nyama mbichi kuliko hata tangawizi.

Sasa wanaotoa hoja wanasema ikiwa papai linalainisha nyama kabla ya kuoka kwenye matumbo si itakuwa zaidi.

Wanadai kwamba papai hulegeza misuli ya uume kutokana na ile nguvu ya kuflash matumbo hasa kwa wenye matatizo ya kukwama kwa choo.

Ukila papai haizidi dakika 30 utaenda toileti kujisaidia haja kubwa

Sasa MDs na wajuvi wengine, ni kweli papai lina athari hizi zinazohisiwa?
 
Inaonesha umeyafakamia sana, sasa hofu imetanda... hebu tupatie mrejesho!
 
Kuna sababu nyingi za kufanya Bendera kugoma kufuata upepo au kupepea nusu mlingoti . Ila hii ya papai kwa kweli tokea nizaliwe sijawahi kusikia.
 
Mambo mengine inabidi utumie akili ya kuzaliwa, ipo siku utaambiwa ugali unapunguza Nguvu za kiume na utakubali.

Kila kitu ni sumu ukitumia vibaya.
 
Back
Top Bottom