KAMUGUNGA
JF-Expert Member
- Mar 25, 2013
- 238
- 269
Nimetafakari kwa kina maamuzi yaliyotolewa jana na Naibu Spika Dr Tulia kuhusu wabunge wa UKAWA wanaosusia vikao ambavyo yeye ana viongoza. Maswali yangu yalilenga mambo yafuatayo;
1. Je wabunge hawatalipwa posho za vikao hata kama Naibu Spika akitoka kwenye kiti na kumwachia mwenyekiti wa bunge kiti mara tu baada ya Maswali na Majibu.
Hapa namaanisha bunge linaanza saa tatu, wabunge watakuwa wamesaini mahudhulio mara Naibu ataingia, wabunge wa UKAWA watatoka bungeni mara baada ya Maswali na Majibu Naibu atamwachia kiti Mwenyekiti na wabunge wa UKAWA watarudi bungeni.
Je, kwenye hili kanuni ama haya tunayoyaita maamuzi yaliyokwisha kupitishwa zamani na spika wengine yanasemaje kwenye hali kama hii?
2. Baada ya kusitishwa kuonyeshwa live kwa bunge tumeshuhudia kupitia vyombo vingine vya habari kuwa wabunge wamekuwa hawahudhurii vikao, viti vingi upande wa ccm vimeonekana vikiwa wazi muda wote wa mijadala. Je kwa hawa ambao hawagomi na hawana mgogoro na mtu lakini wanafika bungeni asubuhi, wanasaini na kuondoka kiasi kwamba bunge linabaki wazi wao kanuni inasemaje? Ni kweli spika au naibu huwa anatoa ruhusa kwa nusu ya wabunge wa ccm kwa siku?
Mimi naona kuna suala la kisheria ambalo UKAWA wanaweza kulifanyia kazi na kushinda ubabe huu wa Naibu Spika.
Kwakuwa mnawapiga picha wa kutosha na kuna namna ya kupata taarifa za waliosaini asubuhi; sasa kazi ifanyike ya kuhakikisha wabunge wote wa ccm wanaosaini na kuondoka wasipate posho daima.
Na kama spika ama naibu wake atajitokeza na kusema wote amewapa ruhusa basi Tanzania tujue kwamba spika anashiriki kuhujumu taifa kwa kulipa watu wasiofanya kazi waliyotumwa na wananchi ambayo ni kinyume cha kanuni alizotusomea.
Uwezo wa hawa wanaobaki bungeni akiingia Naibu ni mdogo sana bado UKAWA mnayo nafasi ya kuonyesha madhaifu yao makubwa kwa taifa hili.