Je, ni kweli kwamba mtu akiuawa basi zile dhambi zake zote anabeba muuaji wake?

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Nina imani humu Jamii forum kuna wajuvi wengi sana ,
Leo sijaja na maelezo mengi sana bali nimekuja tu na maswali haya machache wajuvi wanaojua waje wanijibu ,

Je ni kweli kwamba mtu akiuawa basi yule aliyemuua ndiye anabeba dhambi zake?

Vitabu vya imani(Dini) vinaelezaje kuhusu hilo?

Au ukweli wote ni kwamba mtu akiuawa anaenda na dhambi zake ila yule aliyeua ndio anabeba dhambi yake tu ya kuua na siyo dhambi za yule aliyemuua(marehemu) ?

Nahitaji kufahamu kuhusu hilo wakuu.
 
Utahukumiwa kwa yale uliyofanya sio uliofanyiwa
Jiulize tangu kuumbwa kwa ulimwengu ni watu wangapi wameuawa vitani je wote wanaenda mbinguni?
 
Nina imani humu Jamii forum kuna wajuvi wengi sana ,
Leo sijaja na maelezo mengi sana bali nimekuja tu na maswali haya machache wajuvi wanaojua waje wanijibu ,

Je ni kweli kwamba mtu akiuawa basi yule aliyemuua ndiye anabeba dhambi zake?

Vitabu vya imani(Dini) vinaelezaje kuhusu hilo?

Au ukweli wote ni kwamba mtu akiuawa anaenda na dhambi zake ila yule aliyeua ndio anabeba dhambi yake tu ya kuua na siyo dhambi za yule aliyemuua(marehemu) ?

Nahitaji kufahamu kuhusu hilo wakuu.
haya mambo huenda na imani, kwani huko ktk imani yako inasemaje ktk hili?
 
Kila mtu anahusika na dhambi zake mwenyewe!
Kumbukumbu la sheria 24:16 "Wazazi wasiuawe kwa makosa ya ya watoto wao wala watoto wao wasiuawe kwa ajili ya makosa ya wazazi wao. Kila mtu atauawa kwa makosa yake mwenyewe"
Kwa mujibu wa hiko kifungu tu hapo juu tayari ushapata jibu kuwa kila mtu atahusika na makosa/dhambi zake yeye mwenyewe. Soma Zaidi 2 Mambo ya Nyakati 25:4!

Isipokua tu dhambi za kurithi ambazo hupatilizwa toka kizazi kimoja mpaka kizazi cha 4 hadi dambi hiyo iwe imelipwa "Kutoka 34:7 na Kumbukumbu la sheria 5:9".
MUNGU ndie pekee anaepatiliza hizo dhambi za vizazi na vizazi.
Cc davisoni Mnyongeni Mnyonge
 
Kila mtu atabeba fulushi lake,Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu,hakuna kubebeana wala kusaliana ili Mungu apunguze au kumsamehe mtu,Kila mmoja anapaswa kutengeneza na Mungu wake kabla jua la mauti halijamkuta.
Mkuu unaudhibitisho wa yeyote aliyebeba furushi lake
 
Tena wanasema dhambi haina mzani et muongo na muuaji wote wako sawa hakuna alomzidi mwenzake ukubwa wa dhambi
 
Tena wanasema dhambi haina mzani et muongo na muuaji wote wako sawa hakuna alomzidi mwenzake ukubwa wa dhambi
Nikuambie tuu dhambi zinatofautiana kwa mfano dhambi ya kumtukana Roho Mtakatifu haisameheki kamwe!
Lakini nyingine zinasameheka!
Sasa ndugu yangu utasemaje dhambiz zote ni sawa.

NB: Ni kwa mujibu wangu lakini.
 
Tena wanasema dhambi haina mzani et muongo na muuaji wote wako sawa hakuna alomzidi mwenzake ukubwa wa dhambi
Dhambi zina tofauti, kwa mujibu wa Uislam kuna dhambi kubwa kama Ushirikina,Uchawi,Kuua,Kula mali ya yatima,Riba,Zinaa n.k
 
Back
Top Bottom