Je, ni kweli kwamba matumizi ya majani ya chai ya muda mrefu huharibu kongosho?

commm

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
1,674
1,905
Leo katika pita pita zangu maeneo ya sokoni.

Nikiwasikia wamama wawili wakishauriana kwamba waache Matumizi ya majani ya chai na wajikite zaidi katika Matumizi ya viungo vya chai kama mdalasini na vinginevyo kwa sababu majani ya chai eti yanaharibu "kongosho"

Je, wakuu hili jambo ni la kweli?
 
Ni sawa hata bia kwa muda mrefu huaribu maini lakini watu hatuachi kunywa,kwani unataka uishi milele mkuu.
 
Hakika! Majani ya chai hasa 'Black Tea' yanazo athari mbalimbali kiafya. Majani haya tunaweza kuyaingiza katika kundi la madawa ya kulevya daraja la 3.

Utumiaji wa majani ya chai uathiri na kuvuruga mfumo wa kongosho, afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake, mfumo wa afya ya utambuzi (Senses) na ni hatari wakati wa ujauzito.

Majani haya unapozidi kuyatumia ukupatia arosto ya kuhitaji muendelezo, miaka ya hivi karibuni yamekuwa yakitumika kama njia ya kuondosha/utoaji mimba.

Nashauri watumiaji wa majani ya chai kuacha mara moja na kuanza kutumia viungo vifuatavyo;- Mchaichai, Iliki, Tangawizi, Mdarasini, Karafuu na Ovia.
 
Back
Top Bottom