Je ni kweli kuwa wanasiasa wa Tanzania ni wezi wa mali ya umma zaidi ya wakina Mobutu na Marcos?

Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,264
2,000
Nilikuwa nasoma mtandaoni leo gazeti moja la kiingereza lililoandika habari ya jinsi fedha zilizotarajiwa kufufua kiwanda cha nguo cha Urafiki lakini zikaliwa na wajanja!!

Pia habari kama hizo hizo zimeeleza jinsi viwanda vyetu vilivyobinafsishwa kugeuzwa maghala na huku waliouziwa mpaka sasa wengine hawajamaliza kuvilipia kama vile kiwanda cha madawa Moshi na Moproco Morogoro.

Sasa msomaji mmoja ameandika comment baada ya habari hizi kwenye hilo gazeti kuwa eti wanasiasa wa Tanzania ni wezi na wabadhilifi wa mali za umma kuliko aliyekuwa mtawala wa Zaire Mobutu Sese Seko na yule wa Phillipines Marcos na familia yake.

Je ni kuwa kweli hawa watawala wetu wametuibia mpaka wakawa na utajili wa namna hiyo?
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Ni vigumu kukadiria kiwango cha wizi wao, maana itatulazimu tumfuate mmojammoja na kuanza kumwuliza ameiba kiasi gani na anamiliki nini na nini! Ila jambo moja ni wazi. Kuwa hata wao hawabishi kuwa ni wezi wa mali za umma na pia kwa sasa hata hawahangaiki kujitetea inapotokea wanaambiwa waliua viwanda na mashirika ya umma kwa makusudi na tamaa.

Kwa hiyo vyovyote vile, bila kujali waliiba kama kina Seseseko au la, bado ni wezi. Na sidhani kama kuna anayeweza kuniambia wizi ni sifa njema kwa kiongozi. Kwa hiyo mimi nadhani kuna haja ya wananchi kukubaliana kuwawajibisha.

Najua viongozi wa nchi hii wanafikiria wako salama, kwa kuwa hicho kichaka chao cha ujinga wa wananchi bado kinawasitiri, But kama wanaakili wanatakiwa wajue afya ya hivyo vichaka siyo ya kujivunia sana. Muda si mwingi sana watakuwa wanaonekana tu.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Naomba mleta uzi aulizie, hivi George Hala, Mlebanoni aliyeiuzia midege mibovu Air Tanzania na kupelekea kuifilisi aliidhinisha nani hayo manunuzi kinyume na ushauri wa wataalamu?

Usije ukastuka jibu likiwa ni Nyerere.
 
figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,677
2,000
Nilikuwa nasoma mtandaoni leo gazeti moja la kiingereza lililoandika habari ya jinsi fedha zilizotarajiwa kufufua kiwanda cha nguo cha Urafiki lakini zikaliwa na wajanja!! Pia habari kama hizo hizo zimeeleza jinsi viwanda vyetu vilivyobinafsishwa kugeuzwa maghala na huku waliouziwa mpaka sasa wengine hawajamaliza kuvilipia kama vile kiwanda cha madawa Moshi na Moproco Morogoro. Sasa msomaji mmoja ameandika comment baada ya habari hizi kwenye hilo gazeti kuwa eti wanasiasa wa Tanzania ni wezi na wabadhilifi wa mali za umma kuliko aliyekuwa mtawala wa Zaire Mobutu Sese Seko na yule wa Phillipines Marcos na familia yake; je ni kuwa kweli hawa watawala wetu wametuibia mpaka wakawa na utajili wa namna hiyo?

Gazeti gani na mimi nilisome? mia
 
Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,264
2,000
Naomba mleta uzi aulizie, hivi George Hala, Mlebanoni aliyeiuzia midege mibovu Air Tanzania na kupelekea kuifilisi aliidhinisha nani hayo manunuzi kinyume na ushauri wa wataalamu?

Usije ukastuka jibu likiwa ni Nyerere.

Je ni nani aliyeshinikiza ATC mpaka wakakodisha ndege AIRBUS mbovu ambayo haikuruka hata siku moja na mpaka sasa serikali inalipa deni la mabillioni? Yule broker mchina alikuwa anakwenda Ikulu alikuwa anaonana na nani?
 
idoyo

JF-Expert Member
Jan 13, 2013
3,020
2,000
Naomba mleta uzi aulizie, hivi George Hala, Mlebanoni aliyeiuzia midege mibovu Air Tanzania na kupelekea kuifilisi aliidhinisha nani hayo manunuzi kinyume na ushauri wa wataalamu?

Usije ukastuka jibu likiwa ni Nyerere
.
naona unataka kumtusi muasisi wa muungano.
 
bona

JF-Expert Member
Nov 6, 2009
3,801
1,250
Naomba mleta uzi aulizie, hivi George Hala, Mlebanoni aliyeiuzia midege mibovu Air Tanzania na kupelekea kuifilisi aliidhinisha nani hayo manunuzi kinyume na ushauri wa wataalamu?

Usije ukastuka jibu likiwa ni Nyerere.

hili ndio swali alilouliza mleta mada? kwani umepigwa ban kuleta thread mpya? kama una hoja tofauti c ulete thread yake kuliko kututoa ktk mjadala tunaoendelea nao? kama umesoma elimu yako imekuletea ukombozi kweli au umeaulu tu una kazi ya kulisha familia nk
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
77,506
2,000
Naomba mleta uzi aulizie, hivi George Hala, Mlebanoni aliyeiuzia midege mibovu Air Tanzania na kupelekea kuifilisi aliidhinisha nani hayo manunuzi kinyume na ushauri wa wataalamu?

Usije ukastuka jibu likiwa ni Nyerere.

OK , nimekuelewa , unachomaanisha ni kwamba chama chenu kimeruhusu ufisadi !
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
hili ndio swali alilouliza mleta mada? kwani umepigwa ban kuleta thread mpya? kama una hoja tofauti c ulete thread yake kuliko kututoa ktk mjadala tunaoendelea nao? kama umesoma elimu yako imekuletea ukombozi kweli au umeaulu tu una kazi ya kulisha familia nk

Tazama swali halafu ujionee hapo nilipojibu kuna mwanasiasa au hakuna. Ukipata jibu usimwambie mtu, atakucheka.
 
Mandown

JF-Expert Member
Apr 8, 2012
1,669
1,500
Naomba mleta uzi aulizie, hivi George Hala, Mlebanoni aliyeiuzia midege mibovu Air Tanzania na kupelekea kuifilisi aliidhinisha nani hayo manunuzi kinyume na ushauri wa wataalamu?

Usije ukastuka jibu likiwa ni Nyerere.

Kweli ufsadi zaidi ya Zaire ya MOBUTU. We fikiria ule mradi wa spidi Gavana ulianzishwa na nani na ulifia wapi? Na nani anaye saplai TOCH za kugundulia wanao zidisha mwendo!@!@!!!!
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,819
2,000
Tanzania yetu,, me nimetenda kusupply v20 mpya 20,,, na ndege 2 za kivita.. nimeambiwa hata mkila nyasi poa tu,,, hapa kwetu nafikili kuna matajiri zaidi ya Bill gate wewe Billion 200 mchezo,, Bill gate hana hizi!!! We mtu analipwa 150mil kwa siku au mmesahau dowans, kweli wajinga ndio waliwao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom