Je, ni kweli kuwa Wabunge wote wa Tanzania ni wanasiasa?

JACADUOGO2.

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
930
217
Ningependwa kufahamishwa na wana jf wenzangu kama ni kweli kwamba wabunge wote wa Tanzania ni wanasiasa? Mfano, mbunge wa Rorya Lameck Airo hajawahi kufungua kinywa bungeni kuuliza swali hata kuchangia hoja tofauti na siku ya kuapishwa tangu alipoingia 2010 na hata kwenye kampeni alikuwa anapanda jukwaani na kusema "darasa la saba oyee, naombeni kura zenu"!
Je, ni kweli kuwa wabunge wote wa Tanzania ni wanasiasa?
 
Darasa la saba oyeeeeee, CCM oyeeeee, wasomi ndio wananibebea begi wakati nikipanda ndege kwenda ulaya, CCM oyeee! Akishuka anagawa pesa pesa anasonga mbele. Narubongo upo? Muone JACADUOGO2. anavyosema.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Jacoduogo2. wengi wa wabunge wetu si wanasiasa. Kuna wanasiasa wachache sana wengi wa wabunge ni wachumia tumbo. Wengine wanatumia kichaka cha ubunge kujificha tu kama akina Airo na wafanyabiashar kadhaa ambao ni wabunge. Nilikuwa huko Rorya siku za karibuni nikiwatumikia walipa kodi watu wamemchoka Airo. Nasikia na yeye hautaki tena Ubunge. Kama kuna wanaRorya vijana wahamasisheni wakatwae kiti kiko wazi for grabbing.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom