Je, ni kweli kuwa uwepo wa wakimbizi nchini ni miradi ya watu? naombeni ufafanuzi

5997

JF-Expert Member
Jan 19, 2019
514
1,204
Miezi kadhaa iliyopita kulikua na ishu inayohusu kuwarudisha wakimbizi Burundi,
Baada ya Waziri Kangi kutiliana saini ya makubaliano kati yake na waziri wa burundi, UNHCR walichachamaa mpaka kutishia kuishtaki Tanzania umoja wa mataifa.

Juzi kati hapa kulikua na mechi ya Burundi, nilikua nimekaa na Bwana mmoja mzito hapa nchini alishawai kuwa mbunge miaka ya nyuma, nilikua nikiangalia mashabiki wa timu ya burundi walikua na furaha kweli, Nikamuuliza bwana huyu mbona wanasema burundi hakuna amani wakati mi naona watu wanschangamka kama kawaida tu na maisha kama kawa,

Akanijibu, wee acha tu hao wakimbizi ni miradi ya watu,

Sikutaka kuzungumza naye zaidi

Nilijiuliza sana kumbe hawa watu weupe wanajitia wanatusaidia kumbe wako kwenye biashara?
Na kama wanapata faida inawezekana kabisa wakawa sehemu ya machafuko kwenye nchi zinazotoa wakimbizi,

Lakini je Tanzania inapata faida au hasara kuhifadhi wakimbizi?

Je, wazungu wananufaikaje na wakimbizi wakati wao ndio wanawagharamia kila kitu?

Kama Tanzania pia inanufaika na wakinbizi kwanini inataka kuwarudisha kwa nguvu?

Mnijibu wakuu wangu
 
Back
Top Bottom